Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Friday, February 10, 2012

Kazi afanye mume, mshahara kupewa mke


Mshahara
Mshahara sasa kwenda kwa mke
Maafisa katika jimbo la Gorontalo nchini Indonesia wamepata njia mpya ya kuhakikisha wake wa wafanyakazi wa serikali wanapata mgao wa kutosha wa mshahara wa waume zao.
Mpango huo ni kuweka fedha za mishahara katika akaunti za benki za wake wa wafanyakazi wa serikali. Mpango huo unatazamiwa kuanza mwezi Machi na unatarajiwa kuweka familia pamoja, kutokana na kongezeka kwa vitendo vya wanaume kutumia fedha za ziada kwa wanawake wa nje.
Hatua hiyo ni ya kuzuia matumizi "mabaya" ya fedha. Maafisa wanasema wamepokea malalamiko mengi mwezi uliopita kutoka kwa wake wa wafanyakazi wa serikali, ambao wanasema hwapati fedha za kutosha kutoka kwa waume zao kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Msemaji wa jimbo la Gorontalo Rudy Iriawan amesema kanuni hiyo mpya ina lengo la kulinda familia zisimeguke. "Tuna wasiwasi kwa kuwa mwanaume ndio anadhibiti fedha za familia.
Na tunataka kuhakikisha mishahara ya wafanyakazi wa serikali inatumika kujenga familia na sio kwa ajili ya mambo mengine hasa wanawake wa nje".
Hata hivyo maafisa hao pia wameonya kuwa wake wa wafanyakazi hao wa serikali wasitumie fedha kujinunulia vitu vya kifahari.
Wametakiwa kuzingatia hatua hiyo kama kazi, zimesema mamlaka, katika kutazama fedha za familia za nyumba zao.
source BBC

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.