Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Friday, March 2, 2012

STARS NA MAMBAS YA MSUMBIJI ZAINGIZA MIL 64/-

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mechi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika-
AFCON 2013 kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Msumbiji (Mambas) iliyochezwa jana
(Februari 29 mwaka huu) imeingiza sh. 64,714,000.
Fedha hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 16,776 waliokata tiketi kushuhudia
pambano hilo lililochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Sehemu iliyoingiza watazamaji wengi ilikuwa viti vya bluu na kijani ambapo 14,403
walikata tiketi kwa kiingilio cha sh. 3,000 kwa kila mmoja. Viingilio vingine katika
mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C,
sh. 15,000 viti vya VIP B wakati VIP A iliyoingiza watazamaji 91 kiingilio kilikuwa
sh. 20,000.
Mgawanyo wa mapato hayo ni kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) ilikuwa sh. 9,871,627, gharama ya kuchapa tiketi sh. 4,500,000, malipo
kwa waamuzi wane na kamishna wa mchezo huo sh. 12,180,000 na ulinzi na usafi kwa
Uwanja wa Taifa sh. 2,350,000.
Malipo kwa Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000, maandalizi ya uwanja (pitch
marking) sh. 400,000 wakati asilimia 20 ya gharama za mchezo ni sh. 6,682,475.
Mgawo mwingine ni asilimia 10 ya uwanja sh. 3,341,237, asilimia 5 ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 1,670,136 na asilimia 65 ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) sh. 21,718,042.

Source:
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.