Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Thursday, March 1, 2012

MAMA ZETU NAO WAFUMWA WAKIJIUZA





Na Richard Bukos
INASIKITISHAJE? Wakati wenzao wakijituma kufanya kazi ili kusukuma mbele gurudumu la maisha, akina mama wenye umri uliosogea, ambao ni mama zetu, wamenaswa laivu wakifanya biashara haramu ya kuuza miili yao.
WANASWA ENEO LA WAZI
Katika oparesheni iliyoendeshwa na jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita, akina mama hao walitiwa nguvuni baada ya kukutwa wakijiuza katika eneo la wazi, Buguruni Kimboka jijini Dar es Salaam.
Majina ya wanawake hao na umri wao katika mabano ni Sauda Mussa (52), Jacqueline Francis (40), Laurencia Rafael (40) na Grace Robinson (40).

WANA BIFU NA MABINTI WADOGO
Kwa mujibu wa wenzao ambao hawakunaswa, waliozungumza na paparazi wetu bila kujua, akina mama hao wamekuwa wakijihusisha na biashara hiyo tangu kitambo na kwamba huwa wana bifu na mabinti wadogo wanaojiuza.

PURUKUSHANI ZA KUKAMATWA
Uchunguzi wa Amani ulibaini kuwa katika eneo hilo, kuna akina mama wengi wanaojiuza na hao waliokamatwa ni wale walioshindwa kuwakimbia polisi katika purukushani ya kukamatwa.

INASIKITISHA
Kwa umri wa akina mama hao, vijana wa Kamanda Suleiman Kova waliowanasa walisema kuwa ni tukio la aibu na la kusikitisha kwani walipaswa kutulia nyumbani na kula matunda ya watoto wao au kujihusisha na shughuli nyingine za ujenzi wa taifa.

KUPANDISHWA KIZIMBANI
Baada ya kukamatwa, akina mama hao walitarajiwa kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Jiji la Dar es Salaam, Sokoine Drive, Februari 27, mwaka huu kujibu shitaka hilo.

KUTOKA AMANI
Kwetu sisi tunaamini hakuna linaloshindikana chini ya jua hivyo sote kwa pamoja, katika umoja wetu, tuipige vita biashara hii haramu inayoshika kasi katika jamii yetu.

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.