NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Bara, John Chiligati juzialitaka kujiuzulu ujumbe wa Sekretarieti ya chama hicho mbele ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete kutokana na kukerwa na kile alichokiita kuvuja kwa siri za kikao cha sekretarieti hiyo iliyoketi mwishoni mwa wiki kujadili mchakato wa kura za maoni kuelekea uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki.

Sekretarieti hiyo ambayo ilitoa mapendekezo hayo kwa Kamati Kuu (CC) ya CCM,pia ilitoa angalizo kwamba kama Sioi angepitishwa, chama kingekuwa katika hatari ya kuwekewa pingamizi kutokana na madai hayo ya utata wa uraia na pia,vigogo wengine wangekisaidia Chadema ili kishinde uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Aprili Mosi, mwaka huu.

Siku iliyofuta mkakati huo ulivuja katika vyombo vya habari siku ambayo pia kulikuwana kikao cha CC na ndipo Chiligati alipolalamika mbele ya Mwenyekiti Kikwete akidaiwa kusema: “Haiwezekani mambo tuliyojadili jana (siku ya kikao) yaandikwekatika magazeti neno kwa neno.”

Wakati Chiligati akijibu hayo, taarifa kutoka ndani ya kikao hicho cha CC,zilisema kwamba baadaye Rais Kikwete aliitaka sekretarieti hiyo yenye watu tisa ijiangalie yenyewe kujua nani anavijisha taarifa za vikao.

Source: Mwanachi