Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Friday, March 2, 2012

SHAROBARO ABAKA

Na Richard Bukos
KIJANA Juma Shaaban almaarufu Sharobaro (20) Mkazi wa Kijiji cha Kidugalo, wilayani Kisarawe mkoani Pwani amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti na kumbaka kisha kumsokomeza kijiti sehemu za siri bibi kizee chenye umri wa miaka 80 (Jina linahifadhiwa).
Mwendesha mashitaka katika Mahakama ya  Wilaya ya Kisarawe, ASP Gumbo alisema mshitakiwa anadaiwa kuwa mnamo Agosti 11, mwaka 2011 saa 10 jioni, katika Kijiji cha Kidugalo wilayani Kisarawe mkoani Pwani alimbaka bibi kizee huyo kisha kumsokomeza mti ukeni.
ASP Gumbo alisema baada mshitakiwa kumbaka kikongwe huyo alimuambukiza Virusi Vya Ukimwi.
Kufuatia mashitaka hayo hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Timothy Lyon alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri  na ule wa utetezi, alimtia hatiani mshitakiwa na kumhukumu kifungo cha maisha jela.
Hakimu akaongeza kuwa mshitakiwa ana nafasi ya kukata rufaa ikiwa ataamua kufanya hivyo.
Baada ya hukumu hiyo, mshitakiwa alianza kuangua kilio mahakamani hapo na kuwaponyoka askari magereza  waliokuwa wakimlinda lakini walifanikiwa kumkamata kwenye lango kuu la mahakama hiyo kisha kumpeleka katika Gereza la Ukonga kuanza maisha mapya.

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.