Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Thursday, March 1, 2012

MASTAA WAHUSISHWA NA USAGAJIHalima.
Isabela.
Rose Ndauka na Maya.
Maya.


Musa Mateja na Erick Evarist
AMA kweli dunia imekwisha! Imebainika kuwa baadhi ya mastaa wa kike wa tasnia mbalimbali Bongo, wamejiingiza kwenye magenge ya kufanya vitendo vya ngono vya wenyewe kwa wenyewe (usagaji), Amani limezama kwenye uchunguzi wa kina.
Kwa mujibu wa uchunguzi wetu, baadhi ya mastaa hao wamekuwa malimbukeni kwa kufanya vitendo vilivyo nje ya maadili ya Kitanzania likiwemo hili la usagaji.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, wanachokifanya mastaa hao kwa sasa ni kuzungukana wao kwa wao wakifanya dhambi hiyo.

VIASHIRIA
Amani limebaini kuwa mastaa wa kike wenye ukaribu zaidi wana mambo ya ajabu nyuma ya pazia.
Mastaa hao ambao wanakuwa pamoja kwenye kumbi za starehe huku wakinywa na kuishi chumba kimoja ‘geto’, ndiyo wanaoongoza katika uhusiano huo mchafu.
Imebainika kuwa wengi wa mastaa hao huanza kwa kuiga baadhi ya tabia za mastaa wengine hasa wale wa nje na kujikuta wakijiingiza katika vitendo hivyo.
Wengi huanza kwa kuigiza mavazi yasiyo na staha, kunywa pombe, kuvuta sigara na madawa ya kulevya kisha baadaye hufikia hatua ya kufanya vitendo hivyo.

WAKIMBIA MAKWAO
Mara nyingi mastaa wanaokaa pamoja huwa wanakimbia maisha ya kubanwa na wazazi nyumbani kwao na kuutafuta uhuru kwa kuhamia kwa mastaa wenzao.

 MAGENGE
Imebumburuka kuwa magenge hayo ya usagaji yanazidi kukua kwa kasi kutokana na wasanii wachanga wanaoingia katika tasnia za muziki na filamu kuiga tabia za waliowatangulia.
Imedaiwa kuwa hata kugombana kwa baadhi ya mastaa wa kike Bongo kutokana na wivu wa mapenzi kati yao, jambo linalosababisha kuwepo kwa makundi yanayopingana.

KUNA WANANDOA
Imefahamika kuwa baadhi ya mastaa wenye majina makubwa waliopo katika makundi hayo wapo katika uhusiano na wanaume na wengine wamechumbiwa au kuolewa kabisa.
Uchunguzi huo ulibaini kuwa, mastaa wenye ndoa wamefikia hatua ya kukubali ndoa zao zivunjike ili waendelee kufanya mambo yao kwa uhuru.

MAMBO HADHARANI
Ripoti ya Amani inathibitisha kuwa imefikia hatua, mastaa hao hawaoni aibu kufanya vitendo vyenye viashirio vya kisagaji hadharani pale mzuka unapowapanda. Gazeti hili limewabamba wengi wakifanya vitendo hivyo vinavyotia kinyaa (ushahidi wa picha za kumwaga upo).
Pamoja na mastaa, pia baadhi ya wasichana wanaojiita wa mjini nao wameingia katika mkumbo huo wa kuiga tabia za mastaa hao.
Mastaa waliowahi kubambwa wakifanya vitendo vya usagaji ni Jacqueline Pentezel ‘Jack wa Chuz’ akiwa na Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, Isabella Mpanda na msichana aliyetajwa kwa jina moja la Jack, Nelly Kamwelu, Mayasa Mrisho (pichani) na Rose Ndauka, Latifa Idabu ‘Badra’ na tukio bichi la staa wa filamu, Halima Madiwa aliyenaswa wikiendi iliyopita akiwa chobingo na msichana mwenzake.

KALAMU YA AMANI
Mastaa wa kike Bongo wanapaswa kutambua kuwa wao ni kioo cha jamii hivyo watumie nafasi hiyo kuifunza jamii mambo yanayofaa kuigwa na siyo uchafu.

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.