Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Friday, March 2, 2012

Chama cha ANC chamtimua Malema

 
Julius Malema anatarajiwa kukata rufaa ya kumtimua chamani


Kiongozi wa mrengo wa vijana katika chama tawala cha ANC nchini Africa Kusini, Julius Malema, sasa ametimuliwa rasmi kutoka chama cha ANC baada ya rufaa ya kupinga uamuzi wa kutimuliwa kwake hapo awali, kutupiliwa mbali.
Kamati ya nidhamu ya chama cha ANC ilitoa uamuzi huo baada ya kusikiliza rufaa iliyowasilishwa na Malema dhidi ya kutimuliwa kwake chamani kwa kipindi cha miaka mitano kwa makosa ya kuleta mgawanyiko katika ANC.
Kamati hiyo ikiongozwa na kiongozi mkongwe na mfanyibishara Cyril Ramaphosa, iliangalia tena rufaa aliyokata Bw Malema na bado ikampata na makosa ya kukigawanya chama cha ANC pamoja na kukitia aibu.
Hata hivyo, Malema katika siku za awali ameelezea wazi kwamba atakata rufaa iwapo kamati hiyo itamsimamisha kujihusisha na shughuli za chama tawala cha ANC.
Bw Malema bado anaweza kukata rufaa katika kipindi cha miaka 14.
Julius Malema amekuwa akisisitiza kuwa anaonewa kwa sababu anataka chama hicho kutaifisha migodi ya nchi hiyo.
Pia anasema baadhi ya watu katika chama cha ANC hawamtaki kwa sababu anataka chama hicho kupata kiongozi mpya katika mkutano wake baadaye mwaka huu ili kuchukua nafasi ya Rais Jacob Zuma kuondoka

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.