Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Friday, March 2, 2012

Aukata Uume Wake Kuwakomoa Wanawake Wanaomgombania


NewsImages/6292030.jpg
Wednesday, February 29, 2012 8:54 PM
Rombo Moshi Kilimanjaro, Bw. Priva Elian (29) amekata sehemu zake za siri na kuziondoa kabisa kwa kutumia kitu chenye ncha kali. Amefanya hilo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kugombaniwa na wanawake wawili.
Wanawake wawili wanaomgombea Priya kiasi cha kumkera na kumfanya afikie uamuzi huo wa ajabu kwa watu wengi. Tukio hilo limetokea Februari 27, mwaka huu saa 1:30 asubuhi baada ya kupandwa na hasira kutokana na usumbufu mwingi aliokuwa akiupata kutoka kwa wanawake hao.

Mara baada ya kuchukua uamuzi huo, alimwita mdogo wake na kumweleza kuwa achukue nyeti hiyo na kuwapelekea wanawake hao ili waigombee. Wakati huo huo, kutokana na kuvuja damu nyingi, majeruhi huyo alipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Huruma iliyopo wilayani humo akiwa amepoteza fahamu na hawezi kuzungumza. 
  

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.