Na: Patrick Sanga
Septemba mwaka huu, Mwanafunzi mmoja wa shule ya Sekondari alinitembelea nyumbani kwangu hapa Dodoma. Alipofika nilimkaribisha ndani nikajua amekuja kunisalimia tu. Baada ya muda akaniambia kaka Sanga nina swali nahitaji msaada wako sana. Tukatoka nje mahala penye utulivu ndipo akaniambia tamaa za mwili kwa maana ya uasherati/zinaaa zinanitesa nifanye nini ili kushinda? Jambo hili linanitesa kiasi kwamba nahisi kama vile sijaokoka kutokana na vita niliyonayo katika fahamu zangu na mwilini mwangu?Kwa kuwa vijana wengi wamekuwa wakiuliza swali hili kwa namna tofauti tofauti na kwa njia mbalimbali, nimeona ni vema nikaliweka somo hili kwenye ‘blog’ hii kwa kuwa tunao vijana wengi ambao changamoto hii inawakabili pia. Naam yafuatayao ni mambo ya msingi kuzingatia ili kijana aweze kuwa na ushindi dhidi ya tamaa za mwili (dhambi) nk.
- Kwa kutii na kulifuata neno la Mungu
Naam hii ina maana ni lazima kwanza kijana achukua hatue ya kuliweka neno la Mungu moyoni mwake kwa wingi, maana hawezi kutii neno ambalo halimo ndani yake au hajalisoma na kulitafakari. Zaburi 119:11 inasema ‘Moyoni mwangu nimeleiweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi’. Maana yake ni kwamba, kama kijana atajijengea tabia ya kuhakikisha analiweka neno la Bwana moyoni mwake kwa kulitafakari kila siku, kwa vyovyote vile lazima atakuwa na ushindi dhidi ya tamaa za mwili na kazi zote za Shetani. Naam usiishie tu kuliweka moyoni mwako bali fuatilia sauti ya neno uliloliweka ndani yako, ukaiitii.
- Kuacha michezo ya mapenzi na kuwa makini na nini unatazama/unasikia.
Zaidi Katika dunia ya sasa Shetani ametumia teknolojia iliyopo kuteka fikra za vijana wengi. Vijana wengi kupitia simu, computer, video nk wanaangalia picha chafu za ngono na kusoma jumbe za aina hiyo kitu ambacho kinaharibu fahamu zao bila wao kujua. Na kwa kufanya hivyo wanakuwa wanayachochea mapenzi na kuamsha tamaa zao za mwili. Naam mambo haya ni hatari tena kinyume na mapenzi ya Mungu. Na kwa bahati mbaya vijana wetu tena waliokoka baadhi yao bado wamefungwa katika kufanya mambo haya.
Katika kile kitabu cha Wimbo Ulio Bora 2:7 Biblia inasema ‘Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe’. Kulingana na mstari huu tunajua kwamba, kumbe mapenzi yanaweza kuchochewa na kuamshwa, naam na hili ni jambo hatari sana kama litafanywa na wahusika ambao si wanandoa kwa maana ya (foreplay) hata kama wana kiroho cha iana gani.
Jambo la msingi kuepuka hapa ni kuwa kwenye mazingira ambayo yanaweza yakawashawishi kufanya mambo haya. Vijana ambao si wanandoa kutembeleana mahali wanaposihi kwa maana ya eneo ambalo wako pekee yao, au kwenda guest na maeneo yote ya namna hii eti kwa lengo la kupanga mipango yenu. Fahamu kwamba kitendo cha vijana wawili ambao si wanandoa kukaa katika mazingira ya aina hii ni kumpa Iblisi nafasi ya kuwamaliza, naam kijana uwe makini usifanye ujinga huu, Shetani asije akakumaliza.
- Kuenenda kwa Roho.
- Kujitenga na marafiki/makundi mabaya
Mtume Paulo akizungumza na kijana wake Paulo alimwambia hivi ‘Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi’ 1 Timotheo 4:12. Wazo ninalotaka ulipate hapa ni kwamba kama Paulo angejua kwamba vijana hawawezi kuishi maisha ya utakatifu na yenye ushuhuda katika dunia hii, asingemwambia Timotheo afanye haya. Basi kwa kuwa alijua inawezekana, ndiyo maana Roho Mtakatifu alimwongoza kuandika haya ili kumwagiza Timotheo na sisi vijana wa leo katika jambo hili. Naam uwe kielelezo katika shule, chuo, kanisa, kazini nk ili Mungu aone sababu ya kuendelea kukutumia kwa utukufu wake.
Neema ya Mungu iwe nanyi
No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.