Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Friday, December 9, 2011

Makamu Wa Rais Mgeni Rasmi Mkesha Wa Maadhimisho Ya Miaka 50 Ya Uhuru


|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza kuwahutubia wananchi waliohudhuria mkesha wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo Desemba 8 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Koba, baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo kuhudhuria Mkesha wa Sherehe za Maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru.


Mafataki yakifyatuka baada ya kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibonyesha Rimoti  kufyatua Mafataki ikiwa ni sehemu ya kuzindua rasmi Mkesha wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 50 Uhuru zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja usiku wa kuamkia leo. Kutoka (kushoto) ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mke wa Makamu wa Rais, Mama Zakhia Bilal na (kulia) ni Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilal.
Rapa na mwimbaji wa Bendi ya TOT Plus, Jua Kali, akighani rap zake jukwaani wakati wa mkesha wa sherehe hizo.
Wasanii wa Kundi la Sanaa la Safi Theatre, wakionyesha umahiri wao jukwaani wa kucheza Sarakasi.
Baadhi ya Vijana waliohudhuria sherehe hizo
Baadhi ya Viongozi wa Kisiasa na wananchi waliohudhuria sherehe hizo
Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha JKT Mgulani, wakishambulia jukwaa kwa kucheza ngoma ya Bugobogobo ya Kabila la Wasukuma, wakati wa sherehe hizo.

HAPPY UHURU DAY: TANGANYIKA 50 YEARS!

|

Ndugu zangu,
Mjengwablog inawatakia WaTanzania furaha ya uhuru wa Tanganyika ambayo sasa ni Tanzania. Hii ni siku kubwa. Ni siku ya kutafakari kwa bidii. Miaka hamsini ijayo, wakati wengi wetu hatutakuwa duniani tena, watoto na wajukuu zetu watasheherekea jubilei ya Tanganyika kutimiza miaka 100!
Tujiulize sasa tulikotoka, tulipo sasa na tunakokwenda?
Siku Njema ya Uhuru kwenu nyote.
Maggid Mjengwa,
Iringa, Desemba 9, 2011.

Sherehe Za Miaka 50 Ya Uhuru Ujerumani

|

FFU wa Ngoma Africa Band kutoa burudani ya kukata na Mundu
CD ya "50 Uhuru Anniversary" inatamba Redioni
Watanzania wanaoishi Ujerumani ! na Full Shangwe ya Miaka 50 ya Uhuru !
Berlin Chereko !Chereko !

Umoja wa Tanzania Ujerumani (UTU) kuzinduliwa rasmi ! 10-12-2011 Berlin!

Kikosi Kazi cha Ngoma Africa band aka FFU,kimeshatua mjini Berlin kwa kazi moja tu,
nayo ni kushambulia na muziki wake katika kusherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania.

Kuanzia 9 hadi 10-Dec-2011 mjini Berlin ambako ndipo hupo Ubalozi wa Tanzania na ndio
mji mkuu wa Ujerumani,kutakuwa hapatoshi kwani sherehe hizo zitaambatana na ufunguzi
wa UMOJA WA WATANZANIA UJERUMANI (UTU) siku ya jumamosi 10-12-2011,umoja
huo unawaunganisha watanzania wote waishio ujerumani,ulitiliwa nguvu na balozi Mh.Ngemera, umeshasajiliwa na viongozi wake ni Bw.Mfundo Peter Mfundo(mwenyekiti) na
Bi.Tullalumba Mloge (katibu),utaratibu unaonyesha kuwa sherehe hizo mjini Berlin zitaanza saa 9 mchana hadi usiku usio kwisha ambapo Ngoma Africa Band aka FFU,watatumbuiza na muziki wao,mahala patakapo fanyika sherehe Apostelkirche 1, 10738 Berlin,
UMOJA NI NGUVU WATANZANIA JITOKEZENI ! KUSHREKEA MIAKA 50 YA UHURU !
sikiliza muziki at www.ngoma-africa.com

WaTanganyika Walijawa Na Furaha Kuu Siku Kama Ya Leo......!

|


Desemba 9, 1961. Ni miaka 50 iliyopita. Nasi tunapaswa kufurahia na kutafakari, kwa bidii.

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.