Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Friday, December 9, 2011

MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA UWANJA WA UHURU MAMBO YAMEIVA

Friday, December 9, 2011


Mabalozi mbalimbali wakishuka katika basi maalum la Wizara ya Mambo ya Nje mara baada ya kuwasili katika sherehe za Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania ,zinazofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam zikihudhuriwa na wageni mbalimbai, mabalozi wakuu wa nchi kadhaa za Afrika, Asia na Ulaya na viongozi wa Serikali wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk Jakaya Kikwete. Fullshangwe iko katika eneo la tukio ikikumuvuzishia matukio mbalimbali yanayojiri katika sherehe hizo.
Waheshimiwa wabunge na makatibu wakuu wa Wizara mbalimbali wakiteremka kwenye mabasi yaliyowabeba kwa ajili ya kushiriki katika sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania
Mambo yameiva katika sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania kama unavyoona kundi la bendi ya Msondo ngoma likiwatumbuiza wageni waalikwa mbalimbali katika sherehe hizo
Watu mbalimbali wakiwa wamefurika katika uwanja wa Uhuru.
Vijana wa halaiki wakiwa katika staili maalum ya ukaaji katika sherehe hizo.
Mwanamuziki mpiga gitaa la Solo wa bendi ya Msondo akipiga gitaa lake katika sherehe hizo wakati bendi hiyo ikitoa burudani.

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.