Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Friday, December 9, 2011

1961-2011
M. M. Mwanakijiji Utenzi wa Miaka Hamsini ya Tanzania
UTENZI WA TANZANIA
KUTAMALAKI KWA TAIFA
Miaka 50 ya Uhuru
Utangulizi
Nilipata wazo la kuandika utenzi huu kuanzia mwaka jana. Nilikuwa nimekusudia kuandika Utenzi wenye beti 1000 kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Lakini katika uvivu wangu na mihangaiko ya dunia nimejikuta nimeishia kwenye hizi beti 100 za utenzi huu wa Tanzania.
Maadhimisho ya miaka hamsini ya Uhuru ni maadhimisho siyo ya mipaka ya nchi, siyo ya jina na kwa hakika kabisa siyo maadhimisho ya kupita kwa muda. Ni maadhimisho – naamini- ya utu wetu. Kwamba, katika miaka hamsini iliyopita tumeweza kufanya kile ambacho hakikuwahi kufanywa kwa miaka 2000 iliyopita katika eneo letu. Yaani, kuwaunganisha watu watu wetu wote, chini ya mipaka ile ile, wakiwa huru na haki sawa.
Katika utenzi huu nimeelezea jinsi eneo letu lilivyojulikana kama Azania katika masimulizi ya Wagiriki au kama Zenji kwa Waarabu na wakati mwingine kuhusiana na majina ya maeneo ya Kushi na Nubia katika Biblia. Kama jamii ya watu tumepitia mambo karibu yote ambayo yamepitiwa na jamii nyingine za dunia. Kuanzia maisha ya ujima, utumwa, vita, mapigano, na hatimaye uhuru. Kumbe basi historia yetu haina tofauti sana na historia ya jamii nyingine za watu ambazo zimesimama katika pande za dunia.
Unaposoma utenzi huu ni matumaini yangu utakufanya ujisikie fahari kuwa wewe kama vile mimi ni zao la historia hii. Tumefungamanishwa na historia kiasi kwamba haiwezi kufunguka. Mbele yetu wametutangulia wengi katika historia ambao nao walisimama kutambua utu wao na kuudai mbele ya watawala wa zama zao. Ni hiki ndicho tunachokifurahia kwamba leo tuko huru kuwa watu sawa na wengine – kwa kila hali. Ni utu wetu ndio ulikuwa msingi wa kupigania uhuru wetu na unatakiwa kuwa ndio kiini cha kushangilia uhuru huo.
Ni vipi tumetumia uhuru huo kuinua utu wetu hili ni swali jingine ambalo kizazi chetu kama kizazi kinachokuja kitahiji kujibu. Je, mambo tunayoyafanya na kufanyiana yanalingana na utu huo? Je, tunatendeana kama watu wenye utu katika sera, sharia, mipango, na mambo tunayoyafanya? Utenzi huu basi ni kukumbushia utu wetu.
MMM
Disemba 5, 2011
SIFA KWA MUNGU!
1. Ee Mola ninakujia
Kwako ninasujudia
Sifa nakurudishia
Utukufu enzi pia
2. Ewe uliye Jalia
Mmiliki wa Dunia
Hukumu ni zako pia
Na adhabu ya Jehania
UTANGULIZI
3. Kalamu naishikia
Naandika beti mia
Kwa tungo nazipangia
Zinasifu Tanzania
4. Ni tungo za historia
Ni wapi tulianzia,
Na wapi tumefikia,
Lengo ni kukumbushia
5. Nataka kusimulia,
Kwa hizi tungo mia,
Huku nawahisabia,
Mpaka zitapotimia,
6. Tangu walipoingia
Wageni toka Asia,
Na wale wa Yuropia,
Makabila yalohamia.
7. Ishirini na mia,
Makabila ya Tanzania,
Makubwa madogo pia
Hapa nawasimulia
8. Na beti zikitimia
Zikifika hizo mia
Kalamu nitaachia
Lengo nitalifikia.
9. Ujumbe nauanzia
Wa hizi beti mia
Kwa kina nitagusia
Ni wapi tulianzia
HISTORIA YA AZANIA
10. Kwanza ni jiografia
Iko wapi Tanzania
Ni bara la Afrikiya
Upande wa Masharikia!
11. Ethiopia na Somalia
Juu zimetangulia
Kenya nayo yafuatia
Halafu ni Tanzania
12. Na katika historia
Hakuna jina Tanzania
Jina tumejipatia
Muungano tulipoingia
13. Wagiriki waliitia
Eneo letu Azania
Ni kabla ya kuingia
Kwa ukoloni Afrikiya
14. Kama vile wa Misria
Au watu wa Nubia
Na wale Wahabeshia
Sisi ni wa Azania!
15. Hivyo nawasimulia
Ni wapi tulianzia
Katika Historia
Hadi kuwa Tanzania
WATU WA AZANIA
16. Makabila yaliingia
Toka pande za dunia
Ni mengi kuwatajia
Alama zimebakia
17. Watu toka Arabia
Na pia Nigeria
Wakushi waliingia
Waliipenda Azania
18. Wangoni waliingia
Wana wa Zulu kwa mamia
Kutoka Kongo na Nubia
Wakatua Azania
19. Kwa miaka kwa mamia
Historia yatuambia
Mahusiano yalitulia
Wageni na Waafrikia
20. Ishirini zimefikia
Kati ya zile beti mia
Sasa nitasimulia
Ni nini kilitukia!
21. Biashara ya Azania
Uchina hadi India
Kilwa ilifanyikia
Shahidi ni historia
22. Waarabu walipofikia
Karne ya saba ilipotimia
Waliikuta Azania
Jamii iliyotulia
23. Walikuja na kuhamia
Nchi ilivyowavutia
Wakaishi na kuzalia
Na watu wa Azania
24. Jina wakatupatia
Kwa lugha ya Arabia
Ni ‘Zenji’ waliitia
Palipoitwa Azania
25. Sultani Selemania
Kutoka Ushirazia
Na meli kede kafikia
Pale Kilwa kahamia
26. Mrimba kampatia
Kisiwani ardhia
Utawala ukaingia
Na utamaduni wa Arabia
27. Lugha wakachangia
Misamiati ikaingia
Lugha ya Waswahilia
Utamaduni na dini pia
28. Jina waliitia
Ni ‘Zenji’ Naawambia
Mbali wakalifutia
Lile jina Azania!
29. Ni la kale Arabia
Al-Jahiz katuambia
Yule wa Mesopotamia
Siku hizi Iraqiya
30. Al-Muqadasi pia
Naye kayasimulia
Chuki hakuifichia
Ya Wazenj Arabia
31. Thelatha zimetimia
Ya tenzi zangu mia
Aroba nakimbilia
Hapa nawakumbushia
32. Ibn Batuta kajia
Kilwa akaifikia
Kafika kashuhudia
Kwa maneno kasifia!
33. Mji ulivyotulia
Umepangwa kuvutia
Na utumwa upo pia
Batuta kasimulia
KUKUA KWA UTUMWA
34. Zama za Waazania
Utumwa uliingia
Enzi za Waarabia
Kilele ulifikia
35. Wazee wetu mamia
Maelfu ya mia na mia
Nchi waliiachia
Kuchukuliwa Asia
36. Utumwa ukaivunjia
Familia ya Afrikiya
Mwangwi tukausikia
Ukipasua historia
37. Dini hawakuishikia
Utumwa kushikilia
Utu walituvunjia
Laana wakajipatia
38. Leo wanailipia
Na sisi tumetulia
Wao sasa wanalia
Maskini Arabia
KUINGIA KWA WARENO
39. Wareno walipoingia
Da Gama katungulia
Safari akipania
Ili afike India
40. Mombasa kaipitia
Malindi Sofala pia
Na pia akafikia
Kilwa iliyotulia
41.. Mara ya pili kajia
Na bunduki kashikia
Kilwa ikaangukia
Wazungu wakaingia
42. Miaka ikapitia
Na karne zikaishia
Mwarabu kajishindia
Mreno akakimbia
UTAWALA WA OMANI NA TAWALA ZA JADI
43. Omani ikashikia
Pwani ikashikilia
Malindi Zanzibar pia
Mombasa na Kilwa pia
44. Pwani ikiangukia
Kwa wale wa Arabia
Bara nawasimulia
Ni nini kilitukia
45. Jamii zilitulia
Za Wabantu asilia
Tawala kujiundia
Makabila kwa mamia
46. Imani walishikia
Za jadi kuabudia
Kazi wakajifanyia
Familia kujitunzia
47. Wachagga Wapare pia
Wanyakyusa wa Nubia
Wangoni waliingia
Kina Bambu kwa mamia
48. Wasukuma wakatulia
Maelfu ya Mamia
Biashara wakafanyia
Shahidi ni historia
49. Bara na Pwani pia
Falme na tawala mia
Ndivyo ilivyotukia
Hadi Mdachi kuingia!
50. Hamsa zimetimia
Kwenye zile beti mia
Pumzi naishushia
Nusu imenibakia
UJIO WA MJERUMANI
51. Mjerumani kuingia
Ni upya wa historia
Nchi akajigawia
Mikataba akaingia
52. Karli Petero kapitia
Uzigua kafikia
Usagara nako pia
Wazee kahadaia
53. Mikataba wakaingia
Nchi wakampatia
Na walipozindukia
Nchi wameiachia!
MASHUJAA MABABU
54. Wazee wakanuia
Mdachi kumpingia
Harakati kuanzia
Dhulma kuikatalia
55. Bushiri alianzia
Wadachi kushambulia
Ndipo walimvamia
Kwa kamba kaning’inia
56. Bwana Heri kaingia
Uzigua akipigania
Mdachi akamjia
Heri akasalimia
57. Kilwa ikaibukia
Hapa nawakumbushia
Makunganya na mamia
Mdachi kumpigia
58. Mdachi karudishia
Chifu akakimanyia
Kilwa ikaangukia
Kivinje akaning’inia
59. Wayao wakapigia
Machemba katangulia
Miaka kenda ikapitia
Na mwisho kasalimia
60. Isike kapigania
Tabora kuizuia
Mdachi kamzidia
Isike akakimbia
61. Kuliko kusalimia
Amori kajifungia
Shujaa kawaapia
Baruti kajipigia!
62. Sasa nawasimulia
Mwana wa Mtwa sikia
Uhehe kairithia
Mkwawa nawaambia
63. Lugalo akavamia
Wadachi kawazidia
Silaha kazipakia
Kalenga katimkia
64. Vita kavipigania
Na mwaka ukapitia
Wadachi wakamhofia
Sifa kumtangulia
65. Wa tatu ulipoingia
Wadachi wameumia
Ndipo wakajipangia
Mtwa kummalizia
66. Kalenga wakavamia
Mkwawa kawakimbia
Msituni kaingia
Bado kawang’ang’ania
67. Wadachi wanasimulia
Jinsi walimhofia
Tuzo waliahidia
Hakuna msalitia
68. Miaka ikapitia
Minne nawaambia
Ndipo wakampatia
Jeshi kumzungukia
69. Mkwawa kadhamiria
Uhai kuuachia
Kuliko kuabia
Risasi kajipigia!
70. Kwenye zile beti mia
Sabini zimetimia
Zinahusu Tanzania
Ni wapi ilianzia
VITA VYA MAJIMAJI
71. Wadachi hawakutulia
Amani hawakujulia
Kusini uliibukia
Uasi wa kihistoria
72. Mdachi katangazia
Kila kijiji kusikia
Pamba kujilimia
Na kodi kulipia
73. Mababu wakachukia
Jerumani kumtumikia
Kinjekitile kusikia
Mizimu kumshukia
74. Uasi ukalipukia
Mahenge na Kilwa pia
Rufiji ulifikia
Umatumbi kuingia
75. Chabruma kaingia
Lumecha kapigania
Na mashujaa mamia
Nchi walipigania!
76. Mdachi kawazidia
Silaha alitumia
Bunduki mabomu pia
Mbali kawamalizia
77. Mwisho ulipofikia
Songea kasalimia
Kama waliotangulia
Shujaa kaning’inia!
VITA YA KWANZA YA DUNIA
78. Kwa muda tulitulia
Miaka ikapitia
Ndipo nchi kuingia
Vita ya kwanza ya dunia
79. Mdachi kaachilia
Vita hakujishindia
Mwingereza kuingia
Nchi kuidhaminia
HARAKATI ZA UHURU
80. Miaka ikipitia
Watu wakiamkia
Fikra kuzikumbatia
Utu kuupigania
81. Jumuiya wakajiundia
Na vyama vya kushirikia
Mwanza na Moshi Pia
Tanga na vilifikia
82. TAA ilipoanzia
Mashujaa kuingia
Uhuru kupigania
Wakati ulipotimia
83. Vita ya pili ya dunia
Mwamko uliwazidia
Kutaka kujitawalia
Hilo walitamania
84. Mwingereza kumkatalia
Meru hadi Mwanza pia
Makuli kuwakatalia
Utu wao kudaia
85. Nyerere anaingia
Wakati ulitimia
Abdulwahid katulia
Yupo Mzee Rupia
86. Mengine nawatajia
Wale waliotangulia
Mashujaa wa Tanzania
Wachache nakumbushia
87. Dossa Azizi naanzia
Stephen Mhando pia
Kyaruzi kaingia
Na Shehe Amir Pia
88. TANU ilipoanzia
Yumo Mohammed Ramia
Jumbe Tambaza pia
Bibi Titi nawaambia
89. Nchi wakazungukia
Taifa kuamshia
Umoja kuupigania
Uhuru wakililia!
90. Muda ulipofikia
Mwingereza kaachia
Disemba tisa kuingia
Uhuru kutangazia
MUNGU IBARIKI TANZANIA
91. Tisini zimeishia
Kwenye zile beti mia
Mengi nimekumbushia
Ni wapi tuliianzia.
92. Mengi tumeyapitia
Ya machungu na kulia
Muungano tukaingia
Umoja kuurudishia
93. Tukaunda Tanzania
Mkoloni hakutupatia
Hila wamezitumia
Wengine wamedandia
94. Leo wanapigania
Kuivunja Tanzania
Ati wanakililia
Mkoloni alituachia
95. Damu ilimwagikia
Kuilinda Tanzania
Vipi tunawaachia
Wasotaka Tanzania?
96. Yote tuliyopitia
Sehemu ya historia
Makosa yalotukia
Hatuwezi kukimbia
97. Sasa tunashangilia
Tulipofika tumefikia
Na mengi yamebakia
Vizazi twaviachia
98. Wito ni kuwaachia
Ilo bora Tanzania
Waje kuifurahia
Mema tukiwaachia
99. Mwisho ninaufikia
Wa zile beti mia
Ee Mola ibarikia
Nchi yetu Tanzania
100. Iishi na kubakia
Nchi moja Tanzania
Kalamu naiachia
Zimetimu betie mia!
Ω
1961-2011
M. M. Mwanakijiji Utenzi wa Miaka Hamsini ya Tanzania
UTENZI WA TANZANIA
KUTAMALAKI KWA TAIFA
Miaka 50 ya Uhuru
Utangulizi
Nilipata wazo la kuandika utenzi huu kuanzia mwaka jana. Nilikuwa nimekusudia kuandika Utenzi wenye beti 1000 kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Lakini katika uvivu wangu na mihangaiko ya dunia nimejikuta nimeishia kwenye hizi beti 100 za utenzi huu wa Tanzania.
Maadhimisho ya miaka hamsini ya Uhuru ni maadhimisho siyo ya mipaka ya nchi, siyo ya jina na kwa hakika kabisa siyo maadhimisho ya kupita kwa muda. Ni maadhimisho – naamini- ya utu wetu. Kwamba, katika miaka hamsini iliyopita tumeweza kufanya kile ambacho hakikuwahi kufanywa kwa miaka 2000 iliyopita katika eneo letu. Yaani, kuwaunganisha watu watu wetu wote, chini ya mipaka ile ile, wakiwa huru na haki sawa.
Katika utenzi huu nimeelezea jinsi eneo letu lilivyojulikana kama Azania katika masimulizi ya Wagiriki au kama Zenji kwa Waarabu na wakati mwingine kuhusiana na majina ya maeneo ya Kushi na Nubia katika Biblia. Kama jamii ya watu tumepitia mambo karibu yote ambayo yamepitiwa na jamii nyingine za dunia. Kuanzia maisha ya ujima, utumwa, vita, mapigano, na hatimaye uhuru. Kumbe basi historia yetu haina tofauti sana na historia ya jamii nyingine za watu ambazo zimesimama katika pande za dunia.
Unaposoma utenzi huu ni matumaini yangu utakufanya ujisikie fahari kuwa wewe kama vile mimi ni zao la historia hii. Tumefungamanishwa na historia kiasi kwamba haiwezi kufunguka. Mbele yetu wametutangulia wengi katika historia ambao nao walisimama kutambua utu wao na kuudai mbele ya watawala wa zama zao. Ni hiki ndicho tunachokifurahia kwamba leo tuko huru kuwa watu sawa na wengine – kwa kila hali. Ni utu wetu ndio ulikuwa msingi wa kupigania uhuru wetu na unatakiwa kuwa ndio kiini cha kushangilia uhuru huo.
Ni vipi tumetumia uhuru huo kuinua utu wetu hili ni swali jingine ambalo kizazi chetu kama kizazi kinachokuja kitahiji kujibu. Je, mambo tunayoyafanya na kufanyiana yanalingana na utu huo? Je, tunatendeana kama watu wenye utu katika sera, sharia, mipango, na mambo tunayoyafanya? Utenzi huu basi ni kukumbushia utu wetu.
MMM
Disemba 5, 2011
SIFA KWA MUNGU!
1. Ee Mola ninakujia
Kwako ninasujudia
Sifa nakurudishia
Utukufu enzi pia
2. Ewe uliye Jalia
Mmiliki wa Dunia
Hukumu ni zako pia
Na adhabu ya Jehania
UTANGULIZI
3. Kalamu naishikia
Naandika beti mia
Kwa tungo nazipangia
Zinasifu Tanzania
4. Ni tungo za historia
Ni wapi tulianzia,
Na wapi tumefikia,
Lengo ni kukumbushia
5. Nataka kusimulia,
Kwa hizi tungo mia,
Huku nawahisabia,
Mpaka zitapotimia,
6. Tangu walipoingia
Wageni toka Asia,
Na wale wa Yuropia,
Makabila yalohamia.
7. Ishirini na mia,
Makabila ya Tanzania,
Makubwa madogo pia
Hapa nawasimulia
8. Na beti zikitimia
Zikifika hizo mia
Kalamu nitaachia
Lengo nitalifikia.
9. Ujumbe nauanzia
Wa hizi beti mia
Kwa kina nitagusia
Ni wapi tulianzia
HISTORIA YA AZANIA
10. Kwanza ni jiografia
Iko wapi Tanzania
Ni bara la Afrikiya
Upande wa Masharikia!
11. Ethiopia na Somalia
Juu zimetangulia
Kenya nayo yafuatia
Halafu ni Tanzania
12. Na katika historia
Hakuna jina Tanzania
Jina tumejipatia
Muungano tulipoingia
13. Wagiriki waliitia
Eneo letu Azania
Ni kabla ya kuingia
Kwa ukoloni Afrikiya
14. Kama vile wa Misria
Au watu wa Nubia
Na wale Wahabeshia
Sisi ni wa Azania!
15. Hivyo nawasimulia
Ni wapi tulianzia
Katika Historia
Hadi kuwa Tanzania
WATU WA AZANIA
16. Makabila yaliingia
Toka pande za dunia
Ni mengi kuwatajia
Alama zimebakia
17. Watu toka Arabia
Na pia Nigeria
Wakushi waliingia
Waliipenda Azania
18. Wangoni waliingia
Wana wa Zulu kwa mamia
Kutoka Kongo na Nubia
Wakatua Azania
19. Kwa miaka kwa mamia
Historia yatuambia
Mahusiano yalitulia
Wageni na Waafrikia
20. Ishirini zimefikia
Kati ya zile beti mia
Sasa nitasimulia
Ni nini kilitukia!
21. Biashara ya Azania
Uchina hadi India
Kilwa ilifanyikia
Shahidi ni historia
22. Waarabu walipofikia
Karne ya saba ilipotimia
Waliikuta Azania
Jamii iliyotulia
23. Walikuja na kuhamia
Nchi ilivyowavutia
Wakaishi na kuzalia
Na watu wa Azania
24. Jina wakatupatia
Kwa lugha ya Arabia
Ni ‘Zenji’ waliitia
Palipoitwa Azania
25. Sultani Selemania
Kutoka Ushirazia
Na meli kede kafikia
Pale Kilwa kahamia
26. Mrimba kampatia
Kisiwani ardhia
Utawala ukaingia
Na utamaduni wa Arabia
27. Lugha wakachangia
Misamiati ikaingia
Lugha ya Waswahilia
Utamaduni na dini pia
28. Jina waliitia
Ni ‘Zenji’ Naawambia
Mbali wakalifutia
Lile jina Azania!
29. Ni la kale Arabia
Al-Jahiz katuambia
Yule wa Mesopotamia
Siku hizi Iraqiya
30. Al-Muqadasi pia
Naye kayasimulia
Chuki hakuifichia
Ya Wazenj Arabia
31. Thelatha zimetimia
Ya tenzi zangu mia
Aroba nakimbilia
Hapa nawakumbushia
32. Ibn Batuta kajia
Kilwa akaifikia
Kafika kashuhudia
Kwa maneno kasifia!
33. Mji ulivyotulia
Umepangwa kuvutia
Na utumwa upo pia
Batuta kasimulia
KUKUA KWA UTUMWA
34. Zama za Waazania
Utumwa uliingia
Enzi za Waarabia
Kilele ulifikia
35. Wazee wetu mamia
Maelfu ya mia na mia
Nchi waliiachia
Kuchukuliwa Asia
36. Utumwa ukaivunjia
Familia ya Afrikiya
Mwangwi tukausikia
Ukipasua historia
37. Dini hawakuishikia
Utumwa kushikilia
Utu walituvunjia
Laana wakajipatia
38. Leo wanailipia
Na sisi tumetulia
Wao sasa wanalia
Maskini Arabia
KUINGIA KWA WARENO
39. Wareno walipoingia
Da Gama katungulia
Safari akipania
Ili afike India
40. Mombasa kaipitia
Malindi Sofala pia
Na pia akafikia
Kilwa iliyotulia
41.. Mara ya pili kajia
Na bunduki kashikia
Kilwa ikaangukia
Wazungu wakaingia
42. Miaka ikapitia
Na karne zikaishia
Mwarabu kajishindia
Mreno akakimbia
UTAWALA WA OMANI NA TAWALA ZA JADI
43. Omani ikashikia
Pwani ikashikilia
Malindi Zanzibar pia
Mombasa na Kilwa pia
44. Pwani ikiangukia
Kwa wale wa Arabia
Bara nawasimulia
Ni nini kilitukia
45. Jamii zilitulia
Za Wabantu asilia
Tawala kujiundia
Makabila kwa mamia
46. Imani walishikia
Za jadi kuabudia
Kazi wakajifanyia
Familia kujitunzia
47. Wachagga Wapare pia
Wanyakyusa wa Nubia
Wangoni waliingia
Kina Bambu kwa mamia
48. Wasukuma wakatulia
Maelfu ya Mamia
Biashara wakafanyia
Shahidi ni historia
49. Bara na Pwani pia
Falme na tawala mia
Ndivyo ilivyotukia
Hadi Mdachi kuingia!
50. Hamsa zimetimia
Kwenye zile beti mia
Pumzi naishushia
Nusu imenibakia
UJIO WA MJERUMANI
51. Mjerumani kuingia
Ni upya wa historia
Nchi akajigawia
Mikataba akaingia
52. Karli Petero kapitia
Uzigua kafikia
Usagara nako pia
Wazee kahadaia
53. Mikataba wakaingia
Nchi wakampatia
Na walipozindukia
Nchi wameiachia!
MASHUJAA MABABU
54. Wazee wakanuia
Mdachi kumpingia
Harakati kuanzia
Dhulma kuikatalia
55. Bushiri alianzia
Wadachi kushambulia
Ndipo walimvamia
Kwa kamba kaning’inia
56. Bwana Heri kaingia
Uzigua akipigania
Mdachi akamjia
Heri akasalimia
57. Kilwa ikaibukia
Hapa nawakumbushia
Makunganya na mamia
Mdachi kumpigia
58. Mdachi karudishia
Chifu akakimanyia
Kilwa ikaangukia
Kivinje akaning’inia
59. Wayao wakapigia
Machemba katangulia
Miaka kenda ikapitia
Na mwisho kasalimia
60. Isike kapigania
Tabora kuizuia
Mdachi kamzidia
Isike akakimbia
61. Kuliko kusalimia
Amori kajifungia
Shujaa kawaapia
Baruti kajipigia!
62. Sasa nawasimulia
Mwana wa Mtwa sikia
Uhehe kairithia
Mkwawa nawaambia
63. Lugalo akavamia
Wadachi kawazidia
Silaha kazipakia
Kalenga katimkia
64. Vita kavipigania
Na mwaka ukapitia
Wadachi wakamhofia
Sifa kumtangulia
65. Wa tatu ulipoingia
Wadachi wameumia
Ndipo wakajipangia
Mtwa kummalizia
66. Kalenga wakavamia
Mkwawa kawakimbia
Msituni kaingia
Bado kawang’ang’ania
67. Wadachi wanasimulia
Jinsi walimhofia
Tuzo waliahidia
Hakuna msalitia
68. Miaka ikapitia
Minne nawaambia
Ndipo wakampatia
Jeshi kumzungukia
69. Mkwawa kadhamiria
Uhai kuuachia
Kuliko kuabia
Risasi kajipigia!
70. Kwenye zile beti mia
Sabini zimetimia
Zinahusu Tanzania
Ni wapi ilianzia
VITA VYA MAJIMAJI
71. Wadachi hawakutulia
Amani hawakujulia
Kusini uliibukia
Uasi wa kihistoria
72. Mdachi katangazia
Kila kijiji kusikia
Pamba kujilimia
Na kodi kulipia
73. Mababu wakachukia
Jerumani kumtumikia
Kinjekitile kusikia
Mizimu kumshukia
74. Uasi ukalipukia
Mahenge na Kilwa pia
Rufiji ulifikia
Umatumbi kuingia
75. Chabruma kaingia
Lumecha kapigania
Na mashujaa mamia
Nchi walipigania!
76. Mdachi kawazidia
Silaha alitumia
Bunduki mabomu pia
Mbali kawamalizia
77. Mwisho ulipofikia
Songea kasalimia
Kama waliotangulia
Shujaa kaning’inia!
VITA YA KWANZA YA DUNIA
78. Kwa muda tulitulia
Miaka ikapitia
Ndipo nchi kuingia
Vita ya kwanza ya dunia
79. Mdachi kaachilia
Vita hakujishindia
Mwingereza kuingia
Nchi kuidhaminia
HARAKATI ZA UHURU
80. Miaka ikipitia
Watu wakiamkia
Fikra kuzikumbatia
Utu kuupigania
81. Jumuiya wakajiundia
Na vyama vya kushirikia
Mwanza na Moshi Pia
Tanga na vilifikia
82. TAA ilipoanzia
Mashujaa kuingia
Uhuru kupigania
Wakati ulipotimia
83. Vita ya pili ya dunia
Mwamko uliwazidia
Kutaka kujitawalia
Hilo walitamania
84. Mwingereza kumkatalia
Meru hadi Mwanza pia
Makuli kuwakatalia
Utu wao kudaia
85. Nyerere anaingia
Wakati ulitimia
Abdulwahid katulia
Yupo Mzee Rupia
86. Mengine nawatajia
Wale waliotangulia
Mashujaa wa Tanzania
Wachache nakumbushia
87. Dossa Azizi naanzia
Stephen Mhando pia
Kyaruzi kaingia
Na Shehe Amir Pia
88. TANU ilipoanzia
Yumo Mohammed Ramia
Jumbe Tambaza pia
Bibi Titi nawaambia
89. Nchi wakazungukia
Taifa kuamshia
Umoja kuupigania
Uhuru wakililia!
90. Muda ulipofikia
Mwingereza kaachia
Disemba tisa kuingia
Uhuru kutangazia
MUNGU IBARIKI TANZANIA
91. Tisini zimeishia
Kwenye zile beti mia
Mengi nimekumbushia
Ni wapi tuliianzia.
92. Mengi tumeyapitia
Ya machungu na kulia
Muungano tukaingia
Umoja kuurudishia
93. Tukaunda Tanzania
Mkoloni hakutupatia
Hila wamezitumia
Wengine wamedandia
94. Leo wanapigania
Kuivunja Tanzania
Ati wanakililia
Mkoloni alituachia
95. Damu ilimwagikia
Kuilinda Tanzania
Vipi tunawaachia
Wasotaka Tanzania?
96. Yote tuliyopitia
Sehemu ya historia
Makosa yalotukia
Hatuwezi kukimbia
97. Sasa tunashangilia
Tulipofika tumefikia
Na mengi yamebakia
Vizazi twaviachia
98. Wito ni kuwaachia
Ilo bora Tanzania
Waje kuifurahia
Mema tukiwaachia
99. Mwisho ninaufikia
Wa zile beti mia
Ee Mola ibarikia
Nchi yetu Tanzania
100. Iishi na kubakia
Nchi moja Tanzania
Kalamu naiachia
Zimetimu betie mia!
Ω

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.