Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Friday, December 9, 2011

Lulu amgeukia Mungu wake !

Friday, December 9, 2011MatejaBAADA ya kufanya jitihada za hapa na pale za kujisafisha kufuatia kuandamwa na msururu wa skendo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, (pichani) ameamua kumgeukia Mungu, The Udaku Master, Ijumaa lina fulu data.
 

ANAKIRI KUTENDA DHAMBI NYINGI
Staa huyo mkali wa muvi za Kibongo na video za wanamuziki wa Kizazi Kipya, anakiri kutenda dhambi nyingi pamoja na umri wake mdogo wa miaka 18 hivyo kuhitaji utakaso kutoka kwa Mungu.

SASA ATEMBEA NA BIBLIA
Akizungumza na gazeti hili katika ‘intaviyu’ maalum ndani ya bustani mwanana za hoteli ya kifahari ya The Atriums iliyopo Sinza-Afrikasana, Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki hii, Lulu alisema kwa sasa anatembea na Biblia ikiwa ni sehemu ya kutambua uwepo wa Mungu kila sehemu anapokwenda.

KISA CHA YOTE
Lulu alisema kuna siku alikaa na rafiki yake, akamwambia kuwa hivi sasa dunia imeharibika na kila wanachokifanya (maovu) ni marudio tu kwani kuna watu walishafanya uozo, lakini hawapo duniani.

AJIWEKA KARIBU NA MUNGU
Lulu aliweka kweupe kuwa tangu siku hiyo, aliamua kujiweka karibu na Mungu hivyo akatafuta kitabu hicho kitakatifu ili ajifunze Neno la Mungu kiundani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kwenda mbinguni.
 

Lulu anayesali Kanisa Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Tabata, Dar es Salaam alifunguka:
“Sasa hivi popote ninapokwenda lazima niwe na Biblia. Hata katika kitanda ninacholala, ukibinua mto utakutana nayo.
“Ukweli ni kwamba katika kila ninachofanya ni lazima nisali kwanza.

AKIRI HIZI NI SIKU ZA UOVU
“Katika maisha tunayoishi na siku tulizonazo ni za uovu uliopindukia, nimegundua ni vyema kila ulipo uwe na utukufu wa Mungu kwa sababu hakuna anayejua siku wala saa ya kuondoka hapa duniani hivyo nawasihi watu wote kumjua Mungu,” Lulu.

KUTOKA IJUMAA
Kama Lulu amejitambua na kuamua kumrudia Mungu ni jambo zuri na anastahili pongezi, lakini tahadhari ni kwamba anapaswa kushikilia aina hiyo ya maisha na siyo baada ya siku mbili tusikie karudi tena kulekule.Chanzo ni http://www.globalpublishers.

1 comment:

  1. nimeipenda hii, yani na mpenda sana huyu mtoto Mungu amsaidie eendelee mbele maana shetani ni mbaya atamuua tusipo muombea na kumshauri vema.

    ReplyDelete

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.