Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Wednesday, November 30, 2011

Mlevi akata rufaa kwa papa




Barua kwa mheshimiwa sana papa Benedicto wa 16,
Kwanza nakusalimia kwa jina la Yesu. Naamini hujambo pamoja na watu wako hapo Vatikano. Wenzako huku Uwanja wa Fisi na Bongo kwa ujumla hatuna hali hata hivyo gongo tunapata ingawa polisi wanatusumbua kwa kututoa upepo. Mambo yamezidi kutubana kama mikanda huku wanaotwambia tufunge mikanda wakifungua hata zipu. Wanaitana magamba, mafisi, mafisiahadi na majina mengine ya ajabu ajabu.

Kabla ya kukueleza kilichonisibu na kunisukuma kukuandikia waraka huu, ngoja kwanza nikueleze kuwa mie ni msomi lakini asiye na kazi wala hali bali kujinywea gongo lau nipunguze mateso na mawazo.

Mheshimiwa papa nisamehe. Ngoja kwanza nielezee uzoefu wangu na hali ilivyo kwangu kama kielelezo cha walio wengi katika kiza na mateso yasiyomithalika.

Baada ya kuzisahau na kuzishit shahada zangu nilizopata baada ya kuzisotea siyo kupewa wala kughushi toka chuo kikuu cha Harvard, makufuru yaliyofanywa na kanisa kuu la Kirumi la Mwanza yalinifanya nizikumbuke. Kumbe kila shari ina heri na kila heri yaweza kuwa na shari. Wajua nini? Si nilikuta panya wameishaanza kuzinyea. Kumbe ningechelewa wangeweza hata kutafuna shahada zangu na kuzitumia kutengenezea viota vya kuzaliwa panya wengine. Huu nao ni ufisadi wa mapanya so to speak.

Nasisitiza kuwa sikughushi shahada zangu. Nilizihenyekea kula Harvard na aliyenilipia karo na pesa ya kutanua bia wakati ule na kuotesha kirimba tumbo tena majuu si mwingine ni mzee Mchonga mwenyewe na awamu yake ya kwanza ya kila kitu kwa watanzania. Wakati huo Bongo ilikuwa bongo kweli na siyo Danga ya Nyika kama ilivyo sasa.

Je mheshimiwa sorry ndugu papa unajua kuwa huku Danganyana ya Danganyika kanisa lako limeingia kwenye kashfa ya ajabu? Kashfa yenyewe ni kuanza kuwasafisha mafisadi pale wanapotoa pesa. Kinachoendelea hakina tofauti na kile alichokuwa akikifanya muuza mibaraka wa zama za kiza wa kanisa lako kule Ujerumani aitwaye Johann Tetzel ambaye alisema kuwa kadri sarafu idondokavyo kwenye kishubaka cha kukusanyia pesa mwenye roho ya mwenye dhambi hutoka motoni na kuingia peponi. Nadhani unamkumbuka tapeli huyu ambaye makufuru yake yalichochea watu kama Martin Luther, Menno Simmons, Conrad Grebel, Wycliffe John, Melchior Hoffman, John Hut, Balthazar Hubmeier na wengine kuasi kanisa lako na kuunda madhehebu yaliyogeuka tishio baadaye. Anyways, huko kwenye mambo ya radicals and reformation leo siendi nisije nikakuudhi kama hawa walitenda makufuru huku Mwanza.

Ndugu katika Kristo mheshimiwa Papa,
Kwa niaba ya wanywa kahawa wa Danganyika nakuandika mtukutu sorry mtukufu kuwa hekalu la kanisa lako la Kirumi katika jimbo kuu la Mwanza liligeuzwa kuwa pango la wezi pale lilipomkaribisha Eddie Ewassa ambaye huku huitwa gamba kuu namba mbili eti kulichangishia pesa ya kujenga kanisa jingine. Wajua kanisa lako limeuzwa kwa bei gani? Huwezi kuamini lakini ndiyo ukweli-madafu milioni 200. Najua hujui madafu ambayo si kama Lira. Dola moja ni madafu 1900 kwa bei za kilanguzi ambazo zimeanza kuhalalishwa kutokana na wakubwa kuchota pesa za kigeni zilipo na kuzipitisha mlango wa nyuma kuchuma faida.

Ndugu Papa,
Machukizo haya makuu yaliasisiwa na kufanywa na askofu Rulanchi akisaidiana na wadogo zake katika jimbo lake. Baada ya kufanya makufuru hayo, huwezi kuamini eti alifunga safari kwenda kwenye nchi ya voodoo ulipokuwa kukutana nawe wakati huko nyuma aliacha amechafua hekalu! Najua alipofika huko hakukueleza ukweli. Maana hakujua jinsi umma wa walevi ambavyo ungechukulia haya makufuru ya hekalu la bwana kuchangiwa na wezi huku kanisa lako likiwekwa mifukoni mwa watu wezi waroho na wachafu ambao Rulanchi aliwamwagia sifa ambazo hata hajawahi kukumwagia wewe. Hakuna aliyetegemea kuwa vipande thelathini kama vile alivyopewa Yuda kumsaliti Bwana Yesu vingeweza kutumika tena kipindi hiki cha maendeleo makubwa na utajiri wa kutisha wa kanisa lako tukufu. Inashangaza na kukatisha tamaa hadi wanywa kahawa wameamua kukuandikia waraka. Hii ni baada ya kugundua kuwa mamlaka husika huku zimo kitanda kimoja na mafisi wawalao watu ambao sasa wamejipenyeza kwenye hekalu la Bwana.

Huku Uwanja wa Fisi kwenye kijiwe chetu cha kula gongo nasikia maneno machafu yakipita kila mtaa. Wapo wanaosema eti roho mtakatifu siku hizi amepinduliwa na roho mtakakitu. Wengine wanasema kuwa hekalu la Bwana kwa sasa ni halali kuwa pango la wezi ili mradi watoe mshiko. Wapo wanaosema etiuna mpango wa kuanzisha utaratibu wa ubinafsishaji wa Kanisa ili kuongeza mtaji wa kwendea mbinguni. Hali inatisha. Kama wewe au mdogo wake Porikapu Peng’o hamtamchukulia hatua huyu Rulanchi, msichanganye kujikuta mkivuna magugu badala ya mpunga kwenye shamba la Bwana.

Kwa ufupi habari nilizo nazo ni kwamba kuna waamini wa kanisa lako wengi wanaopanga kujiengua na kujiunga na madhehebu mengine na wengine kujinyonga kama hutamwajibisha Rulanchi na genge lake la mafisadi wa kiroho wanaotumia uroho kama roho mtakatifu wakati ni roho mtakachafu.

Nimalizie kwa kukushauri kuwu umwajibisha yeyote mwenye kuvaa ngozi ya kondoo ili kuwahadaa kondoo wa Bwana. Wengi wanashangaa ni dini gani inayoweza kulala kitanda kimoja na mafisadi? Ningeshauri Vatikano isikubali kurejeshwa kwenye enzi za akina Paul Mackincus yule habithi wa kimarekani aliyechafua benki ya Mungu (Banco Ambrosiano) kwa kushikiana na mafia, “Uomini di fiducia”kama akina Licio Gelli, Michele Sindona, Umberto Ortolani, Roberto Calvi na majambazi wengine waliomuua papa John Paul I (Albino Luciano). Kaka papa, nakuomba usiruhusu akina Edwardo Roberto Calvi Ewassa na Andrea Michele Sindano Chenga wa Danganyika waliteke kanisa.

Kwa vile tulivyoheshimiana na Albino Luciani, nguvu zimeniishia na siwezi kuendelea.

Wabanikiwe walioliuza kanisa kwa mafisadi huku waliolinunua wakilaaniwa milele na milele aaamini.

Chanzo: Dira Novemba, 2011.

Tuesday, November 29, 2011

Lowassa; “Mungu Yupo Na Mimi Nitayashinda Majaribu

Askofu Mkuu wa Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Kati Mch, Eliufoo Sima akitoa mahubiri katika kanisa hilo usharika wa Amani Sabasaba mjini Singida wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo ulioendeshwa na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa.
Askofu wa KKKT Mchungaji Eliufoo Sima akipokea kiasi cha shilingi milioni 10 taslimu kutoka kwa Mhe.Lowasa kama mchango wake katika kufanikisha harambee ya ujenzi wa kanisa hilo.
WAZIRI Mkuu Mstaafu Mhe.Edward Lowasa amesema kuwa pamoja na kusemwa maneno mengi sana kwenye vyombo vya habari juu yake lakini anamwamini Mungu kuwa anampigania kila kukicha.
Mwandishi wa mtandao huu kutoka mkoani Singida Hillary Shoo anaripoti kuwa Lowasa ameyasema hayo leo mjini Singida wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa la KKKT usharika wa Amani sabasaba mjini Singida. “Wale wanaofuatilia siasa za nchi yetu kuna maneno mengi saana lakini bwana ni mwema na mwaminifu hatimae tumeshinda”.Alisema. Alisema mara baada ya taarifa hizo siku moja akiwa nyumbani kwake na mkewe huku wakiangalia TV na kutaka kujua magazeti yanasemaje asubuhi kulikuwa na maneno mengi yaliyosemwa ya hovyo hovyo juu yake mengine walishindwa kuyasoma.
“Lakini mke wangu alienda chumba cha pili na kuchukua biblia na kunifungulia maneno ya bibilia kitabu cha Isaya 41:10, usiogope kwa maana mimi niko pamoja nawe tusifadhaike kwa maana mimi ni mungu wako nitakutia nguvu naam nitakusaidia, naam nitakushika mkono wa kuume wa haki yangu.” Alisema na kuongeza kwa maneno hayo niliendelea sana lakini baba askofu nisamehe nichukue hadhara hii kuwashukuru watu wengi sana walioniombea na hatimae kufika hapa nilipo. “Wapo waislamu na mashekhe walifanya dua kwa niaba yangu, nawashukuru sana, pia wapo wakristo walioniombea nao nawashukuru sana, mapadri, mashemasi na watawa, wachungaji na wainjilisti wa madhehebu yote, kwaya mbalimbali na waimbaji wa nyimbo za injili, wanamaombi wote, wanamtandao wao wa ajabu una nguvu kweli kweli na maaskofu wa makanisa yote ya k ikristo pia nawashukuru sana.” Alisema Lowasa.
Aidha Mhe Lowasa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli alisema kuwa maneno mengi ya kisiasa yalisemwa juu yake lakini kimsingi hayakuwa ya kweli ya ukweli na siasa zinazoendelea kwa sasa ni za kuchafuana. Pia Lowasa alinukuu maandiko mengine ambayo aliyasoma kutoka kitabu kitakatifu cha Warumi ambayo aliyasoma mwenyewe. “ Lakini ikiwa roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu hataihuisha miili yenu iliyo katika hali ya kufa kwa Roho wake anakaa ndani yenu” alinukuu Lowasa.Aidha alisema kutokana na misukosuko ya kisiasa ambayo amekumbana nayo amekuwa akimwona Mungu akimtetea na utetezi huo ameupata kutoka kwa Mungu, kutokana na maombi ya watakatifu kutoka dini mbalimbali ambao wako pamoja.
Wale wote ambao wanaamini kuwa nafanya kazi kwa kusimamia haki ya Mungu na kazi zote kwa ujumla waliniombea usiku na mchana na kwa hilo Mungu kawasikia na kanifanya kuendelea tofauti na uchafu ambao mimekuwa nikibambikizwa na siasa za kuchafuana. Hata hivyo Lowasa alidai kuwa kama kiongozi hana Mungu ndani yake hawezi kuhimili mikiki ya kisiasa kwani kinachotakiwa ni kumwomba Mungu ili aweze kutetea kazi zinazofanywa na mtu mwenye haki. “Nimekuja kwenye harambee sio kupiga maneno ya kisiasa, nilimwambia baba askofu tuna utamaduni wa kualikwa haramabee nyingi sana, lakini kabla ya kukubali unauliza kwamba hao unaoshiriki nao wamefanya nini, nyie mmefanya kazi kubwa sana nawashukuru na nafurahi kwenye harambee hii.” Alisistiza na kuongeza.
“Kwa sababu ni njia mojawapo ya kuthibitisha kwamba wananchi wanaweza kufanya mambo yao kwani kanisa kama hili miaka ya nyuma lingeweza kujengwa na wafadhili wa nje lakini leo limejengwa na wananchi wenyewe. Mapema askofu mkuu wa KKKT Dayosisi ya kati Mchungaji,Eliufoo Sima anaamini utulivu wa viongozi wa nchi hii ni dhahiri kwamba Taifa hili kwa jinsi ya utamaduni na mapokeo yake , na mambo magumu yanayotokea siku hadi siku, litafanikiwa kutengeneza njia thabiti ya mafanikio ya watu wake. Askofu Sima alisema kumekuwepo na madai mengi kuwa nchi yetu ni maskini lakini angependa viongozi kuyashughulikia kwa umakini mkubwa ili kuondoa manung’uniko miongoni mwao ili yasiharibu tabia njema ya baadhi yao. Hataa hivyo Askofu Sima alimwagia sifa Mhe.Lowasa na kusema kuwa ni tofauti na viongozi wengine ambao u naweza kuwatafuta kwenye simu kwa muda mwingi na wakawa hawapatikani.
“Kwa kweli wewe ni kiongozi wa pekee,tofauti na wengine,unaweza ukamtafuta kwenye simu hata mara tano na hapatikani, lakini wewe kila ninapokupigia unapokea simu yangu,na hata katika harembee hii nilipokupigia nikakuomba uje Singida ukasema upo njiani unaenda Dodoma,”. “Lakini na mimi nikakwambia nipo njiani naenda Morogoro,ukasema basi tukutane njiani,mtu mkubwa kama wewe kukutana njiani hiyo ni ajabu.”alisema Askofu. Katika harambee hiyo Mhe.Lowasa amechangia kiasi cha shilingi milioni kumi ambapo makusanyo yote yaliyopatikana katika ujenzi wa kanisa la Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Amani zilipatikana zaidi ya shilingi milioni 138. Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini liliko Kanisa hilo Mohammed Dewji (MO) alichangia shilingi milioni 10, Mfanya biashara maarufu hapa nch ini aliyemtaja kwa jina moja tu la Patel amechangia mabati ya kuezekea kanisa hilo yenye thamani ya shilingi milioni 50. Kanisa hilo la usharika wa amani linatarajiwa kukamilika mapema hapo mwakani kwa gharama ya kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 480.
--MJENGWA BLOG---

RAIS ASAINI MUSWAADA WA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Novemba 29, 2011, ametia saini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.

Hatua hiyo ya Mheshimiwa Rais kutia saini Muswada huo inakamilisha safari ya kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 baada ya Bunge kuwa limepitisha Muswada huo uliowasilishwa na Serikali katika kikao kilichopita cha Bunge.

Aidha, kutiwa saini kwa Muswada huo ili uwe Sheria ni hatua kubwa na muhimu katika safari ya kutungwa kwa Katiba mpya ya Tanzania kama ilivyoahidiwa na Mheshimiwa Rais Kikwete katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi Desemba 31, mwaka jana, 2010.

Pamoja na kutiwa saini hiyo bado Serikali itaendelea kusikiliza maoni na mawazo ya wadau na wananchi mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha sheria hiyo.

Hivyo, Mheshimiwa Rais Kikwete anatoa wito kwa mwananchi yoyote mwenye maoni ama mawazo ya namna ya kuboresha Sheria hiyo, ajisikie yuko huru kutoa maoni yake na Serikali itasilikiza na kuchukua hatua zipasazo.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

29 Novemba, 2011

Monday, November 28, 2011

Msimamo wangu: Kupandisha posho za wabunge ni ukichaa na kutojali Hali ya Nchi by zittokabwe

New post on Zitto na Demokrasia

Msimamo wangu: Kupandisha posho za wabunge ni ukichaa na kutojali Hali ya Nchi

by zittokabwe
Nimeshtushwa sana na taarifa za kupandishwa kwa posho za vikao kwa Wabunge. Nimeshtushwa zaidi kwamba Posho hizi zimeanza kulipwa katika mkutano wa Bunge uliopita kabla hata Rais hajaamua maana maslahi yote ya Wabunge huamuliwa na Rais Baada ya kupokea mapendekezo ya Bunge kupitia Tume ya Bunge.
Wabunge wote watambue kwamba kuamua kujipandishia posho zao bila kuzingatia Hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida ni usaliti usio na mfano. Mbunge yeyote ambaye anabariki Jambo hili au anaishi hewani haoni tabunza wananchi au ni mwizi tu na anaona Ubunge ni Kama nafasi ya kujitajirisha binafsi.
Kwa Wabunge wa Chadema, wajue uamuzi kuhusu posho ni uamuzi wa chama na ni uamuzi wa kisera. Mbunge yeyote wa Chadema anayepokea posho za vikao anakwenda kinyume na maamuzi ya sera za chama tulizoahidi wananchi wakati wa uchaguzi. Nimemwomba Katibu Mkuu wa chama kuitisha kikao maalumu cha Kamati Kuu ya chama kujadili suala hili.
Toka tarehe 8 juni mwaka 2011 nilikataa kupokea posho za vikao. Popote ninapohudhuria vikao huomba Risiti ya fedha ninazokataa. Baadhi ya Wabunge Kama Januari Makamba wamekataa posho na hata kwenye semina ya kamati ya nishati alikataa na tumeona kwenye vyombo vya habari jina lake likiwa limekatwa ilhali viongozi wakubwa kabisa wamechukua posho. Nampongeza kijana mwenzangu kwa uzalendo huu. Nawataka wabunge wengine wenye Moyo wa dhati kukataa sio tu ongezeko hili la posho Bali posho yote ya vikao. Kwa nini mbunge akubali kulipwa kwa kukaa?
Tazama nchi hii, juzi serikali ilipokea Msaada wa tshs 20bn kwa ajili ya Sensa ya mwakani wakati wabunge wanalipwa 28bn Kama posho za kukaa tu.
Tanzania inaagiza gesi ya matumizi ya nyumbani kutoka nje kwa kutumia mamilioni ya dola za kimarekani. Kuwanda cha kutengeneza LPG kinagharimu tshs 35bn tu, Wabunge peek Yao kwa mwaka wanatumia 28bn kwa posho za kukaa tu achilia mbali mishahara na marupurupu mengine.
Ipo siku Watanzania watatupiga mawe kwa usaliti huu dhidi yao.
zittokabwe | November 28, 2011 at 10:29 AM | Tags: Say No to posho, say NO to sitting allowance | Categories: Posho za Vikao, Tanzania, Zitto Kabwe | URL: http://wp.me/pRboX-rR
Comment    See all comments
Unsubscribe or change your email settings at Manage Subscriptions.

Thanks for flying with WordPress.com

SALAAM KWA MH. EDWARD LOWASA NA WENZAKE KUHUSU KUSEMA UKWELI (TRUTH) NA SUALA ZIMA LA UADILIFU NA UWAJIBIKAJI WA VIONGOZI TANZANIA.

NAAM, tazama ahadi ya 8 ya mwanachama wa CCM, inasema, “NITASEMA KWELI DAIMA, FITINA KWANGU MWIKO” mwisho wa kunukuu.
Ndugu zangu waheshimiwa wote waliotajwa katika sakata la Richmond napenda wasome kwa kurudia mara kadhaa nukuu hiyo niliyoanza nayo hapo juu katika mstakabali mzima wa kutukuza kwa unyenyekevu kitu kinaitwa kusema UKWELI (TRUTH).

Wahenga walisema UKWELI UNAUMA. Ni vizuri tu wote tukakubaliana hivyo. Huo ndio ustaarabu. Ndio utu kusema ukweli. Tuhuma hizo nzito zinazowakabili wakizijibu pasipo kukiri kitu kinaitwa UKWELI na badala yake wakaendekeza majigambo , uwongo na tukafanya hivyo mahali pasipo husika hawalitakii Taifa letu la Tanzania mema. Katika hili hawatakiwi kutumia jaziba au hasira.

Tena wakumbuke kuwa Mh. Edward Lowasa, na Karamagi na Msabaha walipewa nafasi halali Bungeni. Pale walichokifanya kwa bahati mbaya walitawaliwa na jazba na hasira “ ANGER ”. Ndugu zangu, kuhusu hasira naomba niwaase kama mtaalam mmoja kwa jina SENECA alivyosema kuwa ukikumbwa na hasira (samahani kwa kunukuu kwa kiingereza)“there is no other way but to meditate and ruminate well upon the effects of anger, how it troubles man’s life.

The best time to do this is to look back upon anger when the fit is thoroughly over. Anger is like ruin, which breaks itself upon that, it falls. The scripture teaches us to possess our souls in patience. Whosoever is out of patience is out of possession of his soul. Men must not turn bees” Mwisho wa kunukuu.

Katika makala yangu iliyopita Salaam kwa Mawaziri wa Mhe. J.Kikwete kuhusu uadilifu na uwajibikaji kwa sehemu kubwa nilizungumzia juu ya mawaziri bila kumtaja Mheshimiwa Edward Lowasa.

Mb wa Monduli. Kwa haya aliyoyafanya baada ya kuomba kwa Spika Bungeni na kupewa nafasi ya kwanza ajieleze kuhusu ufisadi wa Richmond, namtafadhalisha asome na kurudia mara kadhaa nukuu niliyoanza nayo hapo juu sambamba na hiyo ya mtaalamu SENECA. Napenda niseme kuwa kwa yale aliyosema Bungeni na Monduli na katika mahijioano ya TVT, bwana Lowasa nasema “si mkweli hata chembe moja”.

Waandishi wa habari wengi tu wamekwisha mchambua kwa usahihi jinsi asivyokuwa mkweli, asivyo muadilifu anavyopenda kusifiwa kwa gharama yoyotena asivyolitakia mema Taifa letu. Narudia, asome kwa utulivu nukuu zote mbili nilizoanza nazo hapo juu. Kama Mwanasheria Mkuu, Mwanyika na wenzake Lowassa hakuridhika na ushauri wao juu ya Richmond na kuona kuwa ulikuwa na madhara kitaifa, kwanini hakutafuta ushauri wa ziada?

Je? Hizo ndizo rasilimali watu pekee nchini katika ushauri wa kiserikali? Je, Vyuo Vikuu na Mahakama Kuu hakuna wataalam wa kisheria wa kuisaidia serikali? Did he leave any stone un-turned?

Kwa mapenzi mema na nchi yetu na mwana (CCM) napenda niwape mfano hai wa Bwana Lowasa asivyo muadilifu na asivyopenda kuwajibika kichama CCM na kiserikali. Tanzania nzima mtakumbuka kuwa huyu mheshimiwa Edward Lowasa alikuwa ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Urais mwaka 1995 na akaenguliwa kwa hoja nzito ya kutokuwa muadilifu na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere, kwa ukweli (wala sio tuhuma) kuwa alikuwa amejilimbikizia mali nyingi kwa kipindi kifupi ndani ya CCM na
Serikali. Muda mfupi alikuwa ni mtumishi wa CCM, muda mfupi kama Mkurugenzi wa kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha.

Mfano hai wenyewe uko hivi; tufuatane kwa kuusoma tafadhali:-
Mara baada ya kurudi Butiama, 1995, baada ya kuenguliwa kugombea nafasi ya urais, siku moja mapema asubuhi Bwana Lowasa alinipigia simu na kusema yafuatayo:
“Bwana Kasori, naomba uende kumwambia Baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, aende Monduli kusaidia kusafisha jina langu ili nisikose ubunge kutokana na yale aliyonisema Dodoma'. Nilishikilia mkono wa simu (TTCL) kwa zaidi ya nusu saa tukiwa tunazungumza na hatimaye mimi nilipata ujasiri wa kumwambia Bwana Lowasa kuwa siwezi kwenda kusema maneno hayo kwa Baba wa taifa na kwamba akitaka aje Butiama na nitamruhusu waongee ana kwa ana. Nikanyamaza na hatimaye yeye akawa wa kwanza kukata simu. Hiyo ikawa itifaki njema kwangu!

Kesho yake tena asubuhi nilipokea simu, safari hii akawa ni mheshimiwa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Kwa maneno yake alisema “Bwana Kasori,jana ulizungumza na Edward Lowasa; naomba ufikishe ombi lake kwa Baba wa taifa tafadhali”.

Kutokana na heshima ya Mheshimiwa Mzee Kawawa, nilikubali na nikaenda na kabla ya hapo nilimuomba Mzee Kawawa akae karibu na simu ili nimpe jibu muda si mrefu.
Nilimueleza Baba wa Taifa kuwa “Mheshimiwa Edward Lowasa kupitia kwa Mhe. Mzee Rashidi Mfaume Kawawa anaomba usaidie kusafisha jina lake kule jimboni kwake Monduli ili asikose ubunge kutokana na yale uliyomsema katika Kamati Kuu ya CCM Dodoma”. Jibu la Baba wa Taifa alilonipa ni kuwa “Nenda umwambie Mzee Rashidi Mfaume Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa”!

Watanzania wote, leo March19, 2008, nawaomba radhi kuwa jibu hilo kwa uzito wa maneno hayo kuwa “Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa” kweli kwa kuzingatia heshima kati ya wazee hao wawili; “Kawawa sikumwambia hivyo”! Badala yake nilimdanganya (nawaomba radhi tena watanzania) jibu nililompa Mzee Kawawa ni kuwa juma lililokuwa linafuata tungekuwa Dar es Salaam na kwamba aje Msasani aongee na Baba wa Taifa. Mhe. Kawawa alikubali.

Nikarudi kwa Baba wa taifa kusema uongo (naomba radhi tena) kuwa “Mzee Kawawa ameomba mzungumze tatizo la Lowasa tutakapofika Dar es Salaam”. Baba wa taifa alikubali na akaagiza nimuombe Mhe. mzee Kawawa kuwa Lowasa na Guninita na wapambe wengine wa Lowasa wote wafike Msasani.

Siku ya siku ikafika. Tukawepo Msasani na Mhe.mzee Kawawa akaja. Lowasa hakuwepo! Sababu anazijua mwenyewe.(muulizeni maana nasema ukweli). Mkutano ulipoanza mzungumzaji wa kwanza nikawa mimi, kueleza lengo la mkutano. Mzungumzaji wa pili alikuwa Baba wa Taifa na swali la kwanza ni kuuliza Lowasa yuko wapi?.

Bila kupoteza wakati Mwalimu alisema “Rashidi , huyu Kasori ananiambai eti niende Monduli nikasafishe jina la Mhe. Lowasa eti asikose ubunge kwamba nilimchafulia Dodoma katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM. Kutokana na ombi lako nilimtuma akuambie usiwe mjinga kama Lowasa. Kasori alikuambia eh?”

Oneni , huko nyuma tayari nilishasema uongo kwa kutosema maneno hayo kwa Mhe. mzee Kawawa. Kweli hilo kurudiwa na Baba wa Taifa kwa Mzee Kawawa mbele yangu lilisababisha kalamu yangu kuanguka, nikatetemeka na nikatokwa na jasho jingi mbele ya hao wazee!!! Bila kutegemea na kwa mshangao mkubwa Mhe. mzee Kawawa alikubali kwa kuitikia “NDIO ALINIAMBIA”. Mwalimu akacheka sana!!!! Sababu sijui hadi leo kwa nini alicheka sana.

Kwa kuendelea, Mwalimu alimwambia Mzee Kawawa kuwa “Kasori ana umri mkubwa kuliko Lowasa. Kasori alipata taabu sana kufikisha kwangu ombi la Lowasa na aliniambia kuwa jana yake alikuwa amekataa ombi la Lowasa. Sasa nasema kuwa kwa umri wangu mimi mzee, Lowasa ni mtoto wangu tena mdogo sana. Kwa heshima mliyonayo kwangu na kwa chama cha Mapinduzi mtanishangaa sana mkisikia niko Monduli eti nipo kwenye majukwaa nasafisha jina Bwana Lowasa asikose ubunge.

Kweli Lowasa ni jasiri sana kusema maneno hayo. Hayo ningeambiwa na Kasori tu ningesita kumuamini. Lakini kwamba hata wewe Rashidi ulitumiwa kusema maneno hayo! Huyu Lowasa ni jasiri sana!!. Lakini kwa nini hajatuambia ukweli kuhusu mali hizo ambazo ni nyingi kuliko mimi ambaye nimekuwa Rais wenu kwa kipindi kirefu? Sasa Bwana Rashidi, nakuomba hivi, kamwambie mwenyekiti wa CCM Mhe. Mwinyi aitishe wajumbe wote wa Kamati Kuu, chagueni tarehe na mahali popote Tanzania, mimi nitakuja kumsafisha Bwana Lowasa na nitagharamia mkutano huo kwa hela zangu. Kamwe msitumie hela za chama wala serikali. Monduli sitokwenda,umesikia eh?”

Mkutano ukaisha hapo Msasani. Hadi uchaguzi 1995, unafanyika na kumalizika Baba wa Taifa hakwenda Monduli. Alichukia sana tabia za Lowasa na alimfahamu kama mtu muongo na mwenye kiburi. Hadi Baba wa Taifa anafariki,sikuwahi na hata niandikapo makala hii sijasikia wala kusoma popote ambapo Lowasa anakanusha alivyolombikiza mali akiwa mtumishi wa CCM na serikali kwa muda mfupi kiasi cha kumzidi Rais wa Kwanza !!!

Sasa anatuhumiwa na vyombo vya habari kununua sehemu ya Ranchi za Taifa kwa kuandika majina ya wanafamilia! Kama hilo nalo ni kweli, ningekuwa mimi nisingeota tena kugombea URAIS n.k Tanzania. Bora kuendelea na biashara kwa uwazi kuliko kupitia mgongo au wa serikali au wa chama ( CCM). Huo ndio ushauri wangu kama mwana CCM kwa Lowassa.

Angalia tunavyofanya “total transgression of CCM regulations and ethics.” Kamati kuu 1995 ilimwona Mhe. Lowassa hana uadilifu. Mhe. Mkapa baada ya kuingia madarakani baada ya muda si mrefu sijui ni kwa kikao gain cha CCM na taasisi ipi ya serikali akamwona Lowassa ni safi na akamweka katika safu yake ya baraza la mawaziri.

Huyu bwana akaendelea na huo usafi hadi akaukwaa uwaziri mkuu 2005. Yote haya yanatia shaka kama kweli ndani ya CCM na Serikali tuna benki sahihi za takwimu za mienendo kitabia ya wanachama na watumishi wetu kama si kubebana kwa majina tu! Nilinunua gazeti la mzalendo nikampa Baba wa Taifa na aliposoma kuwa Lowassa ni Waziri alimaka AHH!!

Katika hili nabaki nimeduwaa hasa tunapopeana madaraka makubwa ya kuendesha nchi kimzaha tu. Tukumbuke kuwa kwa kila kitu na kwa dini yoyote Mungu huweka wazi mambo mahali na kwa muda atakao yeye.( Time and space) ya Mwalimu J.K Nyerere juu ya Lowassa tuliyapuuza. Sasa Mungu kayaanika! Basi tuone hizi tuhuma za RICHMOND n.k, Mikataba ya Madini, EPA zitakavyoshughulikiwa.

Ni huyu Lowasa leo anasema kanyimwa “Natural Justice” hakuulizwa na kamati , kaonewa, kamati ya Mwakyembe inauonea wivu uwaziri mkuu wake na ni mahiri wa kuchukizwa mikataba mibovu na kudhalilika! Oh kweli?

Hivi Lowassa amewahi kusoma wasifu wa kila mmoja wa hao? Bila kupima uzito, busara na hekima ya maneno yake anasema ameachia ngazi kama alivyofanya Mhe.Alli Hassan Mwinyi, Peter Kisumo, Peter Siyovelwa n.k. Hivi CCM yetu hawa ndiyo viongozi tulio nao ngazi za juu? Wasio sema ukweli? Tukumbuke na kukiri kwa dhati wajibu wa wanachama wa CCM , katika katiba (ccm) inasema 15 (7) “ kuwa tayari kujikosoa na kukosolewa…

Watanzania wenzangu haya anayosema Lowasa yanafanana na nukuu niliyoanza nayo? Fikiria nairudia tena “For those winding and crooked courses, are the goings of the serpent, which goes basely upon the belly and not upon the feet!

There is no vile that does cover a man with shame as to be found false and pertifidious” Niharakishe kusema hapa kuwa viumbe vyote ambavyo havikupenda kusema ukweli Mungu aliviadhibu kwa kuvifanya vitembelee matumbo yao milele nyoka wakiwemo! Lowasa, Mwanyika, Hosea na wenzake naomba kama nilivyoanza, tafadhali wasome hiyo nukuu mara kadhaa na waielewe na kuizingatia.

Watanzania wanawashangaa, wanadharau na kuchukizwa na viongozi wasiopenda kusema ukweli kwa maisha magumu waliyo nayo ambayo wao wanawazomea kwa dharau kuwa ni wavivu na wachovu wa kufikiri. Wanasahau kuwa hawa watu wa kawaida ndio wanaozalisha kile kinacholipa mishahara na marupurupu yao.

Kama viongozi wakuu wa CCM, katika hili daima kumbukeni wajibu wenu kwa mujibu wa katiba ya CCM, ibara ya 15 (4) kuwa wakati wote mkweli, mwaminifu na raia mwema wa Tanzania. Onekaneni hivyo kwa vitendo tafadhali. Utaratibu huu wa kusema uongo unadhoofisha amani na utulivu Tanzania.

Hayo niliyasema niko tayari kuyasema bungeni akiwepo Lowasa ikibidi. Hatuwezi kukubali nchi hii kuendelea kuwa na viongozi wa aina hii. WAWE WAKWELI, WASEME UKWELI TU. WANAPOKOSEA HARAKA NA KWA UKWELI NA UNYENYEKEVU WAOMBE RADHI KWENYE VYAMA VYAO, SERIKALINI NA KWA WANANCHI. NI UPUUZI WA HALI YA JUU KUJITETEA OVYO NA KUINGIZA UKABILA ( LOWASSA NA OLE NAIKO) HATA KWA MAKOSA YALIYO DHAHIRI.

Katika mahojiano na TVT Lowassa alikiri kuwa alishindwa kuvunja mkataba wa RICHMOND. Sababu alizitaja. Sawa. Waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa Serikali, kwa mujibu wa kanuni za kudumu za utumishi wa umma ( Toleo 1994), kifungu F33, makosa yake kiserikali ni haya yafuatayo; 33( xi) omission which is against public interest. 33(xiii) negligence occasioning loss to the employer ( yaani serikali na taifa kwa ujumla). 33( xiv) gross negligence in the performance of duty.

Kama mtendaji mkuu wa shughuli zote nzito za serikali bwana Lowassa hana namna ya kujitetea kwa makosa hayo yaliyodhahiri ambayo TANESCO imeendelea kudhoofishwa na RICHMOND kwa yeye kuogopa kutumia utaalam nje ya wale aliowaamini. Mbona tuna vyuo vikuu, je, aalivitumia kikamilifu? Mbona kwa maswala yasiyo na maslahi ya maana tumezoea sasa kukodi wataalam wa nje?

Kwanini hakujiridhisha katika maeneo yote hayo? Tatizo hili ni kubwa sana maana watanzania sasa wanatozwa viwango vikubwa sana kulipia umeme ikiwa ni pamoja na sehemu za uzalishaji zenye kutumia umeme achilia mbali malipo ya capacity charges? Nani anabisha kuwa kwa huu mkataba wa RICHMOND n.k Bwana Lowassa na Wenzake waliweka sahihi za kifo siyo kwa TANESCO tu bali pia cha kuvuruga maendeleo ya nchi yetu na kuendeleza umasikini?

Katika yote haya ambayo yamesemwa, Bwana Lowassa na wenzake wajue kuwa kama watanzania, we have a compelling moral case for complaining against him.
There is also a compelling case that is in Tanzania’s self interest. Recently many trade agreements already have made the poorest countries worse off. Such agreement already have condemned to death thousands of our people . Corporations of whatever name do strip Tanzania of its natural resources leaving behind a trail of environmental devastation etc. This is done through very poor legal frameworks. Nimuhimu tukawa na viongozi waaminifu, waadilifu na wasema ukweli. Kwa haya yanayotendeka, something is fundamentally wrong with our government.

Kwa kila maamuzi tunayoyafanya mara zote tuzingatie ni kwa maslahi ya nani; yale ya Taifa ni kipaumbele cha kwanza. Tuzingatie matumizi mazuri ya rasilimali zetu daima. Duniani ziko serikali nyingi tu ambazo zimevunja mikataba mibovu. Kwa ziara nyingi ambazo viongozi wetu wanafanya na baada ya wanahabari kupigia kelele RICHMOND, kwanini Lowassa huko nje hakutaka kujifunza namna ya kuvunja mikataba mibovu?

Yaani umahiri wake uliishia mkataba wa maji Dar es salaam na kiwanja cha Mnazi Mmoja? Mikakati yetu ya maendeleo imekuwa haileti tija iliyokusudiwa moja ya sababu ikiwa a flawed vision of development. Successful countries have a broader vision of what development entails and a more comprehensive strategy for bringing it about.
It is very unfortunate that in the majority of developing countries Tanzania included the nation – state has been weakened thoroughly! Haya maamuzi yanayofanywa na viongozi kama Lowassa ndiyo matokeo ya kutojua namna ya kuthibiti na kutumia kwa uangalifu fursa za kitu kinaitwa UTANDAWAZI.

Government that attempt to control capital flows find themselves unable to do so, as individuals find ways of circumventing the regulations. A county may want to raise the minimum wage, but discovers it can’t, because foreign companies operating there will decide to move to a county with lower wages.

Situmeona jinsi waziri Chiligati ( waziri wa kazi wa wakati huo) alivyohenyeshwa na wakubwa – wawekezaji kukataa kulipa kima cha chini hapa Tanzania? Wengine wamepunguza kazi ndugu zetu na sasa ni katika kundi la Machinga! Waziri mkuu wa wakati huo Lowassa alisaidiaje? KIMYA! Dhahiri kinachoonekana hapo ni sense of powerlessness. Kwa kukumbatia matajiri na wakubwa wa nje, kupitia utanzawazi, baadhi ya viongozi wetu kama inavyojidhihirisha kupitia RICHMOND n.k. find their ability to act eroded.

These days it is the order of the day for the electorate to see its government bending before foreigners wenye (mitaji). Day in day out democracy is being systematically undermined. When the electorate shouts through the media etc, no body listens! Wanataka sifa tu.
The electorate feels being thoroughly betrayed. Whether we like it or not, it is perceived, quite rightly, I think the way globalization is currently managed is not consistent with democratic principles. Little weight is given to the concerns and voices of ordinary people and the poor! Kwa kiburi cha wakubwa kutosikia, kutopenda kukosolewa Tanzania inaendelea kubaki masikini. Lowassa na wenzake wangekuwa makini na mahiri katika kusikiliza waandishi wa habari mapema RICHMOND n.k isingetufikisha tulipo sasa ambapo kila siku tunapoteza fedha nyingi.

Tusingekuwa na tume juu ya tume ambazo baadhi tunazibeza kwa kejeli hata kwa kutumia chama (CCM). CCM kweli tunasoma na kuzingatia kwa vitendo wajibu wa mwanachama wa CCM kifungu 15(3) na 15 (4) na 15(7) pamoja na ahadi za mwanachama wa CCM (3) na (4), na (8). Hivi CCM sasa ni mali na jina la mtu; kwamba hivyo mtu akikosolewa hamtaki kuona kakosa na mko tayari chama kife kwa ajili ya mtu mmoja au kundi dogo tu la watu? Nendeni Butiama mtupe majibu tafadhali. Uwezo, busara na nia vyote mnavyo. Ningekuwa Lowassa Butiama nisingeenda. Yeye kwenda huko ni kejeli kwa Baba wa Taifa.

BADO TUTAENDELEA KUWASEMA WENZAO KUHUSU MIKATABA YA HOVYO NA UKWAPUAJI WA RASILIMALI ZA NCHI HII. HOJA YA MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR BWANA IDD PANDU HASSAN- “ Lowasa kutostahili kuitwa Waziri mkuu Mstaafu” ni muhimu ikazingatiwa sambamba na utata wa stahili za mafao. Haitoshi kuimba utawala wa sheria na kumbe inapofika kwa wakubwa tunakunja na kunyonga sheria zetu. Sheria ni Msumeno. Someni Pensions Ordinance cap 371 sambamba na kanuni za kudumu za utumishi wa umma toleo la (1994) kifungu F53 (d) na (e). Tusiwe na kigugumizi katika hili.Tujifunze yaliyojiri hapo jirani Kenya hivi majuzi.

Namalizia kwa kusema “Tuheshimu na kudumisha kitu UKWELI”. Kwa viongozi, zingatieni na kwa unyenyekevu heshimuni viapo vyenumnapokabidhiwa madaraka. Baba wa Taifa daima katika mkoba wake alibeba Bibilia na Azimio La Arusha.

Nyinyi kwa kipindi hiki kigumu cha ufisadi na kukithiri kwa rushwa na mikataba mibovu; bebeni daima photo-copy za viapo vyenu pamoja na Bibilia au Koran pamoja na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mnazo dini zenu. Sikusikia yeyote akiapa kwa dini za asili kwa Rais au kwa Spika wa Bunge. Nawashukuru watanzania, Mhe. Spika na Waandishi wa habari ambao wamekemea maneno ya Lowasa na wenzake baada ya kikao cha Bunge.

Namshukuru sana Mhe. William H. Shelukindo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji na Biashara kwa kuwasilisha hoja ya kuundwa kwa kamati ya kuchunguza Richmond na shukran maalum nazitoa kwa Dr. Mwakyembe na wajumbe wote walioshughulikia suala la Richmond na kuwasilisha taarifa Bungeni kwa uadilifu mkubwa sana.

Mwisho nawashukuru Watanzania wote na nchi za nje walionipongeza na kunipa moyo kuhusu makala zangu za kukemea ukwepuaji rasilimali za nchi BoT yenye kichwa cha habari “Salaam kwa Mawaziri” Namshukuru Rais Kikwete. Namshukuru pia Mhariri gazeti la Rai namba 748 na 749. Halmashauri kuu ya CCM inayokutana Butiama naitakia mafanikio makubwa katika maazimio watakayofikia . Baada ya hapo muonekane mmedhamiria kutenda kwa kuleta maendeleo yenye kuzingatia uadilifu na uwajibikaji
Viongozi wabovu wawajibishwe tu.

Watanzania wengi leo bado wanamlilia Mwalimu J.K. Nyerere hasa kwa matatizo kama haya ya mikataba mibovu ya Madini, RICHMOND n.k. Wanasema sorry Mwalimu lived ahead of his time. Alituangazia kwa mengi, hakuna wa kututetea leo kwa matatizo yote haya.

Mungu Ibariki Tanzania. Mungu Ibariki Afrika.

Samwel. H. Kasori
Katibu mstaafu wa J.K.Nyerere

Sunday, November 27, 2011

Nova Kambota: Viva Kamanda Lowassa



Kalamu yangu nashika, shairi nakutungia
Kamanda umeongea, kiwingu umeondoa
Hukutaka kusinzia,makosa kuyarudia
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa

Mwananchi nimesoma, la jana nilinunua
Machoya yakatuama, dukuduku umetoa
Uliyosema Dodoma, Kwakweli yanavutia
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa

Richmond kupasua, mapema uligundua
Kikwete ukamwambia, mkataba kuondoa
Rais akakataa, nini alitegemea?
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa

Nape akashikilia, lile asilolijua
Mikoani kaambaa, uzushi kang’ang’ania
Jinalo kulichafua, wewe ukavumilia
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa

Mapema nilitabiri, falsafa nikapinga
Magamba sikukariri, kuvuana sikuunga
Ukweli niliukiri, mantiki iso kunga
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa

Beti sita nakomea, kalamu naweka chini
Mengi nimeongelea, soma tena kwa makini
Yatazidi kutokea,kusini kaskazini
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa.

Shairi limetungwa na Nova Kambota Mwanaharakati,
Tanzania, East Africa
Jumamosi, November 26, 2011

Lowassa Ni Msafi, Hahitaji Kusafishwa ( Jibu)

Mjengwa naomba tena, jukwaani nirejee
Niliyoandika jana, napenda niyatetee
Mkuranga kimanzichana, Lowassa aendelee
Nkwazi hujaelewa, umefakamia mada

Mhango kajichanganya, kujibu asichojua
Kauropoka unyanya, pasipo kulitambua
Si hasi wala si chanya, Nkwazi kasimamia
Mhango wajipotosha, kujibu usichojua

Lowassa ni mtu safi, tegua kitendawili
Angelikuwa ni ni fisi, mahakama mhimili
Hojazo ni mufilisi, wewe ndumilakuwili
Nkwazi rudi shuleni, kaisome CCM

Mhango wanishangaza, ukweli kutofahamu
Waonekana kilaza, rejea Dar es salaamu
Kwa hoja ntakuchakaza, wewe mwana wa Adamu
CCM huijui, fitina wamezoea

Lowassa ni kiongozi, hili unalitambua
Achana na upuuzi, ule walomzushia
Usijifanye dandizi, kudandia usojua
Nkwazi mwana Mhango, uliza nakusikia


Beti sita natuama, nimefikia tamati
Lowassa mtu wa maana, hodari wa mikakati
Nkwazi soma kwa sana, tambua hizi nyakati
Lowassa ni mtu safi, hahitaji kusafishwa.

Nova Kambota
Tanzania, East Africa

JK Alipokutana Na Viongozi Wa CHADEMA Ikulu





Picha: Ikulu
Chanzo: mjengwa blog

Saturday, November 26, 2011

Kikwete Katika Mahafali Ya Uongozi Wa Mahakama Lushoto

 
 JK na wahitimu wa Stashahada (majoho mekundu) na Certificate (Bluu) katika picha za pamoja
JK na Jaji Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Mh Mohamed Chande Othman

Rais Jakaya Kikwete akihutubia katika mahafali hayo ya 11 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama mjini Luahoto.
Kwa hisani ya Mjengwa Blog

Barrick Gold Corporation - The world's largest gold producer

Careers at Barrick Gold Corporation

Whether a geologist, engineer, haul truck driver or another one of the professionals it takes to make this business run, our employees are the backbone of Barrick's enduring success. They have made us the gold industry leader and we make it a priority to support the aspirations of each individual.
Barrick is a growing and responsible global mining organization that employees are proud to be part of. If you thrive on challenge and delivering results, consider the advantages of a career with Barrick and search our current job openings.

Watanzania Wawili Kucheza Ligi Daraja La Pili Sweden

Joseph Kaniki (Golota).
William John

Wachezaji wawili wa kitanzania, Joseph Kaniki (Golota) na William John wamefanikiwa kujiunga na timu ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF) nchini Sweden, baada ya kufanikiwa kupita katika majaribio( Trials). Majaribio hayo yalijumuisha wachezaji zaidi ya thelathini ambapo wachezaji watano walichaguliwa kujiunga na klabu hiyo ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF)Habari hii imeletwa kwenu na:http://www.africa4life.com/
Na Nancy Mtunga

Mahafali UDOM ni moto wa kuotea mbali

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgvzv1BDaObeXbvatYf00ZQ8FzJ6bdfw1DWEDpvv2eBVKCx-pF8JZfDMUfE0MPYycV3cYFLL7Y2sHfblix5phayXL19ouA-kKRrTAllEXP48oV_pa10BFfEQgPbcqL8GixwrWX26xCDppba/s1600/PB261259.JPG
Chuo kikuu cha Dodoma jana kilifanya mahafali ya pili tangu kuanzishwa ambayo ilikuwa yakufana sana

Papa ashtua Ulimwengu

http://api.ning.com/files/xYb8uwkbeCW-ZoXBkPcnZ9zAsXLf8ZEcqTnjWupYMY3Cqa9atkD8Nx3R9vi65JJLNmT9PLm6R0hPLnahKCUKHQwoxTC-Td2k/PAPA.jpg
Hamida Hassan na MitandaoKIONGOZI Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Joseph Aloisius Ratzinger ‘Papa Benedict XVI’, ameushtua ulimwengu, ishara ya vidole na mikono wakati wa kutoa salamu katika picha zilizotundikwa mitandaoni, vimefananishwa na alama za Jamii ya Siri (Secret Society) inayoitwa Freemasons.
Chanzo; Global Publishers

Syrian Crisis

http://moderntokyotimes.com/wp-content/uploads/2011/05/Syria-crisis.jpg
Syrian forces are pushing towards the centre of the city of Hama as they continue an offensive in which scores of people have died.
Residents told the BBC many people were fleeing to nearby villages, believing the army would gain full control.
On Monday, security forces cracked down on protests in towns around Syria, often after prayers on the first day of the Muslim holy month of Ramadan.
The UN Security Council has resumed discussions on the crisis.
Bridget Kendall reports.

Friday, November 11, 2011

Breaking News; Mlimani Kumechafuka, ni mabomu na risasi zinarindima

Mwandishi wetu kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam anaripoti kuzuka kwa vurugu hivi punde katika viunga vya chuo kikuu Dar es salaam. Kiini cha vurugu hizo kinaelezwa kuwa ni ubabe wa serikali kwa kujibu hoja kwa kutumia risasi na mabomu, taarifa zaidi kutoka kwa baadhi ya wanafunzi zinaeleza kuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wengine wanaitaka serikali kuwapatia haki yao "mikopo" pamoja na fedha za kujikimu lakini cha ajabu si waziri wa elimu Dk Shukuru Kawambwa wala rais Jakaya Kikwete aliyefungua mdomo wake kujibu hoja badala yake wasomi hao wanatishiwa kufungwa midomo kwa nguvu ya risasi na mabomu ambayo yanaendelea kurindima chuoni hapo.
BLOG HII INALAANI VIKALI UBABE HUU NA KUWAPA POLE WANAFUNZI WOTE WANAAONEWA BILA SABABU ZA MSINGI.

Kafulila na Zitto wanaivuruga NCCR - Moses Machali

http://www.corruptiontracker.or.tz/dev/images/stories/zitto%20z.%20kabwe.jpg
SIRI kubwa kuhusu mwenendo wa Zitto Kabwe (Mb) ndani ya chama chake zimeanikwa mitaani na zinaweza kumzamisha kisiasa, MwanaHALISI sasa linaweza kuripoti.

Siku nne baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Willibrod Slaa kusema wamenasa taarifa za mawasiliano ya Zitto, baadhi ya taarifa zimepatikana jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Zitto ananukuliwa akiapa kusaidia wagombea uongozi katika vyama vingine; na katika moja ya taarifa ananukuliwa akisema atasaidia David Kafulila kupata ubunge “hata kabla ya akina John Mnyika…”

Mnyika ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CHADEMA na Kafulila alikuwa Afisa Habari ambaye baada ya kuondolewa wadhifa huo amekimbilia NCCR-Mageuzi. Mnyika anatarajia kugombea ubunge jimbo la Ubungo.

Naye Zitto amenukuliwa na gazeti la Mwananchi la Jumatatu akilalamika kuwa ameingiliwa katika mawasiliano yake ya baruapepe (e-mail); jambo ambalo Mkurugenzi wa Upelelezi, Robert Manumba, amedakia haraka na kusema Zitto akiwapelekea malalamiko watashughulikia.

Kwa mujibu wa mpangilio wa taarifa husika, lazima aliyezitoa amepata ufunguo wa baruapepe (password) wa ama Zitto au mwandishi wa habari wa Mwananchi, Denis Msacky.

Karibu mawasiliano yote ni kati ya Zitto na Msacky juu ya “ushujaa” wa Zitto na jinsi anavyopendwa nje ya chama huku “akichukiwa” na viongozi wake wakuu.

Katika moja ya mawasiliano, inaonyeshwa kuwa Msacky alimwandikia Zitto akieleza, “Leo hii Mrema (Augustine Lyatonga) anasema anakuheshimu wewe, lakini si Mbowe; hivyo hivyo, Lipumba (Profesa Ibrahim) na James Mbatia wanasema wewe una visheni.”

Katika mawasiliano hayo ya Jumanne, 1 Desemba 2009, saa 6.45 adhuhuri, Msacky anaonyeshwa kumwambia Zitto pia kuwa, “CCM nao…wanakusifu kwamba pamoja na kwamba unawaliza sana, lakini ni kiongozi shupavu.”

“Leo hii siasa za CHADEMA zingekuwa zinatisha kama ungekuwa mwenyekiti wa CHADEMA, vijana nchi nzima wangejiunga na chama, uko nao karibu, unaongea nao, una elimu nzuri, unajua mambo, unasoma sana,” imeeleza sehemu ya mawasiliano kutoka kwa Msacky kwenda kwa Zitto.

Kinacholeta wasiwasi ndani ya CHADEMA kinaweza kuwa lugha inayotumiwa katika mawasiliano hayo. Kwa mfano, katika waraka huohuo, Msacky ananukuliwa akiandika:

“Wanataka kukumaliza, nami sitakubali mtu ammalize rafiki yangu nikiangalia…wanasema Mbowe hata Mbatia akikaa vema anaweza kumpita kama siasa za kufukuza zitaendelea. Muhimu, usisikilize watu, tulia, urudi tupange tufanye nini? Lakini ukweli ni kwamba sasa wanakuogopa…Mwenyekiti Mtarajiwa…”

Mawasiliano yanaonyesha kuwa Zitto hakufurahishwa sana na taarifa za Mwananchi kuwa amemsaidia Kafulila magari matatu kwenda Kigoma kufanya kampeni chini ya NCCR-Mageuzi, lakini Msacky anaonyesha kumfariji.

“Kaka, mimi nimeiona story, haina matatizo zaidi ya kuwafanya akina Mbowe kusitisha mpango mbaya dhidi yako maana wanaanza kuogopa. Hata Mrema Lyatonga amesema kwamba Zitto huwa unamsaidia akiwa na shida. This shows that ur a leader katika opposition, wewe ni mtu wa maridhiano, unakuza upinzani Kigoma,” anaeleza.

Anasema, “Leo nasikia akina Mnyika wanahaha sana, waambie familia yako wasiingie katika mtego wa kuanza kuhojiwa na akina Kubenea (Saed wa MwanaHALISI), watawachanganya. Wewe usiongee kitu chochote, wabaki wanahaha, lakini for sure you are safe, na hizo kampeni za Mnyika kukuchafua huku akitaja majina ya Kafulila, ataziacha.”

Akionyesha juhudi za kushawishi, kuliwaza au kufarakanisha, Msacky anaandika, “Katika hili Zitto, mimi niko na wewe, huna kosa ambalo umefanya, na wala usihofu maana wewe utakuwa nguzo ya upinzani Tanzania…Wanakupa majina ya ajabu, wanakuita Mr Dowans, wanatumia akina Halima Mdee kukuchafua katika magazeti…”

Awali Zitto alikuwa amemwandikia Msacky akisema, “Stori niliyoiona kwenye mwananchi itaniletea matatizo sana.” Hiyo ilikuwa Jumatatu 30 Novemba 2009, saa 5.21 asubuhi. Baruapepe hiyo ilikuwa na kichwa kisemacho: “Muhimu na haraka.”

Aidha, katika mawasiliano mengine, Zitto anaendelea kuonyesha kutofurahishwa na taarifa juu ya magari matatu kwa safari ya Kafulila.

Naye anaandika kwa Msacky, “tatizo la stori ni wingi wa magari, itaonekana mimi nina magari mengi na ni fisadi unajua? Hilo ndio tatizo.”

Saini ya Zitto inatofautiana katika baadhi ya baruapepe. Pengine anaandika “zitto” na kwingine anaandika “Zi.”

Moja ya mawasiliano ambayo yanazua mashaka yanaonyesha Zitto akikiri kuwa na mawasiliano na waasi nchini Kongo akiandika, “take it from me (niamini), nina contacts nyingi sana Congo na hao rebels (waasi) huwa wananiomba sana ushauri na kutaka kuwaunganisha.”

Katika moja ya mawasiliano, Msacky anamwonya Zitto kutotumia baruapepe ya “CHADEMA kwa mawasiliano ya siri” na kutaka amwambie mama yake Shida Salum akatae kuongea na waandishi wa habari. “…nasikia Mbowe anataka mama awe akiongea na waandishi, usikubali,” alieleza.

Zitto alipoulizwa kuhusu taarifa ya Mwananchi kuwa anatembea na barua mfukoni ya kujiuzulu uanachama CHADEMA, alisema “Sina la kusema.”

Alipong’ang’anizwa kwamba imekuwaje hawezi kuzungumzia suala hilo ambalo ni muhimu kwa mustakabali wake wa kisiasa kwa chama chake, Zitto alisema, “Ni kwa sababu sitaki kuingia katika malumbano na katibu mkuu wangu (Dk. Willibrod Slaa) kwani malumbano hayo hayataijenga CHADEMA.”

Alipotakiwa kueleza juu ya baruapepe ambazo zinadaiwa kuwa mawasiliano kati yake na Msacky, haraka alijibu, “Sina la kusema.”

Alipoelezwa umuhimu wa yeye kueleza msimamo wake juu ya baruapepe hizo, Zitto alijibu, “Chochote nitakachosema sasa hivi, kitawachanganya Watanzania.

“Sitaki malumbano. Hakuna sababu ya kuwachanganya Watanzania. Hiyo haina maana yoyote,” alisema Zitto kwa sauti ya ukali. Zitto alikuwa akiongea kutoka Ujerumani kwa simu Na. +4915222493231.

MwanaHALISI ilimtafuta Msacky. Baada ya kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa, hatimaye aliandika ujumbe “Kaka, niko katika kikao. Tuma ujumbe.”

Msacky aliulizwa, “Kaka, tumesikia kwamba umetajwa katika sakata la Zitto na chama chake na kwamba wewe ndiye mtibuaji. Je, ni kweli?” Hakujibu ujumbe na alipopigiwa simu ilikuwa inaita hadi kukatika.

Gazeti lilipowasiliana na Mnyika na kumueleza kwamba amekuwa akitajwa katika ujumbe wa Zitto na Msacky, alikiri kupokea ujumbe huo wa baruapepe uliotoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni “Mtanzania mwema.”

Alisema alipoona ujumbe mmoja unahusu Zitto kushauri Msacky kutochapisha habari za mkutano wake na waandishi wa habari, ndipo aliamua kupeleka ujumbe huo kwa Zitto.

“Nilimuuliza kuna hiki kitu nimetumiwa. Je, haya ni maandishi yako au kuna mtu ameingilia emaili yako na kujiandikia haya? Hadi leo hii, bado sijapata jibu,” alisema Mnyika kwa sauti ya masikitiko. Alisema yeye hana cha kusema na kuongeza, “labda umuulize Zitto.”

Alipoulizwa anachukuliaje suala hilo, Mnyika alisema, “Ukiniuliza mimi kwa upande wangu, nilitegemea mambo hayo yangemalizwa katika vikao vya chama na si kwa vyombo vya habari. Lakini kwa hatua ya hivi sasa, nadhani Zitto bado anayo fursa ya kulieleza hili.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe alipoulizwa juu ya madai ya kuwapo njama za kuhujumu chama chake zinazofanywa na Msacky kwa kumtumia Zitto, haraka alijibu, “tuna utaratibu wetu wa kushungulikia mambo ndani ya CHADEMA.”

Alisema, “Sina la kusema. CHADEMA ina utaratibu wake wa kushughulikia mambo yake.”

Kwa kadri mawasiliano ya Zitto na Msacky yanavyoonyesha na iwapo yatathibitishwa kuwa kweli, jambo ambalo linaanza kuthibitishwa na Zitto kwa kulalamika kuingiliwa kwenye faragha, basi uhusiano wake katika chama utakuwa umepata nyufa.

Wachunguzi wa siasa za upinzani nchini wanasema kwa hali hii, uwezekano wa Zitto kubaki ndani ya chama chake ni mdogo. “Ama atajiondoa mwenyewe au hatimaye atafukuzwa,” ameeleza mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Hata hivyo, Zitto amenukuliwa na Mwananchi akisema, “Sitaki kugombana na mtu mimi. Wala msiniweke kwenye kifungo cha siasa. Ni bora niishi huru kuliko katika mateso ya siasa za kipumbavu kabisa. Nitafanya maamuzi ambayo hayajawahi kufikiriwa.”

Wiki iliyopita Kafulila aliwaambia waandishi wa habari kwamba Zitto atafanya maamuzi makubwa ambayo hawakutegemea.

Sunday, November 6, 2011

Uraia wa nchi mbili shinikizo la mafisadi?

http://in2eastafrica.net/wp-content/uploads/2011/07/Bernard-Membe.jpg

Makala yangu juu ya uraia wan chi mbili utaua uzalendo, katika gazeti hili toleo namba 209 la Oktoba 26 hadi Novemba mosi, 2011, imezua mjadala mkubwa.  Nimepokea hoja mbalimbali kwa njia ya simu, nyingi za kuunga mkono na chache za vitisho kutoka kwa wapigaji wasiojitambulisha, nami nimeona vyema kuziweka wazi hisia hizo ili viongozi wetu wapate kuelewa mtizamo wa baadhi ya wananchi wanaowaongoza.
Kwa kuwa ajenda hii inaonekana kugusa na kuzua hisia kali za sehemu kubwa ya jamii ya Kitanzania, hasa kutokana na kauli nyingi za Waziri wetu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na kauli ya Rais, Jakaya Kikwete; aliyoitoa kwa Watanzania raia wa Marekani wakati wa ziara yake nchini humo hivi karibuni na kuwapa matumaini kwamba suala hilo linashughulikiwa kikamilifu. 
Kwa jinsi ninavyoiona ajenda hii, inaweza kutugawa Watanzania. Ni ajenda nzito na nyeti iliyowahi kutolewa kwa miaka 50 ya Uhuru wetu, ukiondoa ile ya mwaka 1962 juu ya “uraia”, iliyomgharimu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, nafasi yake ya Uwaziri Mkuu, kwa kujiuzulu na kurejea kijijini.
Hapa, nitatoa baadhi tu ya hoja nilizopokea kutoka kwa wasomaji kuhusu makala hiyo, kuonyesha jinsi jamii inavyoliona suala hili la uraia pacha kwa mtizamo na hisia hasi.
Awali ya yote, naomba ifahamike kuwa, si kwa Tanzania pekee kwamba hoja ya uraia pacha inatia hofu na kero.  Utafiti uliofanywa unaonesha kuwa, kati ya nchi 53 huru za Afrika, ni nchi 11 tu zimeonyesha kutaka uraia huo; 42 zilizosalia zimesema HAPANA!
Kati ya nchi 173 zinazounda dunia hii, ni nchi 17 (asilimia 9.8) tu zilizoridhia uraia pacha kwa sababu zinazofahamika.  Nchi hizo ni pamoja na Australia, iliyoanzishwa na wafungwa huru (ex-convicts) wa Kingereza miaka mingi iliyopita; Canada na New Zealand, ambazo hadi sasa zimo kwenye himaya ya Malkia wa Uingereza; Costa Rica na Columbia. Soma zaidi nenda http://raiamwema.co.tz/uraia-wa-nchi-mbili-shinikizo-la-mafisadi

Kikwete ngoma nzito! Sitta, Nape wasubiri huruma yake

http://www.fikrapevu.com/wp-content/uploads/2011/04/Kikwete2008.jpg
Na Waandishi wetu

BUNDI mharibifu anazidi kuinyemelea CCM hali inayotishia mgawanyiko mkubwa miongoni mwa makada na wanachama wa chama hicho kikongwe nchini na barani Afrika.

Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu mwaka jana, CCM imejikuta kwenye malumbano mazito miongoni mwa makada wake, yanayochangiwa kwa kiasi kikubwa na mitazamo tofauti katika uendeshaji wa chama na utekelezaji wa misimamo inayotolewa na chama likiwemo suala la kujivua gamba.

Katika hali inayozidisha tishio la mpasuko huo, wenyeviti wa mikoa wa chama hicho sasa wamemtega Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete, wakimtaka amfukuze uanachama Waziri wa Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Samuel Sitta.

Kwenye kikao cha kutathimini uhai wa chama katika mikoa yao kilichofanyika wiki hii jijini Dar es Salaam, wenyeviti hao walishauri, Sitta avuliwe uanachama wa CCM kwa madai kuwa amemtukana, Mwenyekiti wa Taifa, Rais Kikwete.

Mbali na Sitta, baadhi ya wenyeviti hao walitaka Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Nape Nnauye, adhibitiwe kwa madai kuwa amekuwa akitoa matamshi ya upotoshaji yanayokwenda kinyume na maazimio ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC).

Walidai kuwa Sitta alimtukana Rais Kikwete na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM kupitia Kipindi cha dakika 45, kinachorushwa na Kituo cha ITV, kutokana na hatua yake ya kulalamikia utaratibu uliopendekezwa na chama hicho kusimamisha mwanamke kugombea kiti cha Uspika wa Bunge, kwa madai kuwa uamuzi huo ulitokana na shinikizo la mafisadi lililolenga kumwengua kwenye nafasi hiyo.

Ingawa baadhi ya wenyeviti walipinga ushauri huo, kauli hii ni mtihani mpya na mzito kwa Rais Kikwete ambaye anatarajiwa kuongoza Kikao cha Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) Novemba 23, mwaka huu mjini Dodoma.

Sitta aliwahi kunusurika kuvuliwa uanachama baada ya baadhi ya wajumbe wa NEC kumtuhumu kuwa anaendesha bunge kwa ajili ya kuwasaidia wapinzani na kukivuruga chama hicho.

Hata hivyo, Mwenyekiti Rais Kikwete na baadhi ya wajumbe wengine walimnusuru na kuendelea na wadhifa wake wa Spika hadi alipomaliza kipindi chake cha miaka mitano ya kuliongoza Bunge la Tisa mwaka jana.

Kama wenyeviti hawa ambao pia ni wajumbe wa NEC watashikilia msimamo wao wa kutaka Sitta ang'olewe, huenda kikao kijacho kitakuwa moto, hivyo busara za Mwenyekiti (Rais Kikwete) zitahitajika kupoza hali hiyo inayotishia mpasuko mkubwa.

Hata hivyo, wadadisi wa mambo ya kisiasa ndani ya CCM wanaamini kuwa kikao hicho cha wenyeviti ni sehemu ya maandalizi ya msingi kupima joto halisi la kisiasa ndani ya chama kuanzia ngazi ya mikoa kabla ya Kikao cha Kamati Kuu (CC) kitakachofuatiwa na NEC.

Kuna taarifa kwamba, wengi wa wenyeviti wanaoshinikiza kung'olewa Sitta, wanaungwa mkono na kundi la watuhumiwa ufisadi ambao wamekuwa kama paka na panya na kundi linalojipambanua kuwa wapambanaji dhidi ya ufisadi ndani ya chama hicho, linaloungwa mkono na mwanasiasa huyo.

Hivi sasa kuna kila dalili kuwa CCM inapita katika wakati mgumu, kutokana na makundi hayo mawili yanayovutana chini huku kila moja likijaribu kuonyesha kuwa lina nguvu dhidi ya lingine.

Kundi la watuhumiwa wa ufisadi sasa linadaiwa kutumia nguvu ya fedha na vikao vya chama kuhakikisha linawageuzia kibao cha kujivua gamba wanaowapinga ili watoshwe na chama hicho.


Kauli ya Msekwa
Makamu Mwenyekiti wa CCM- Tanzania Bara, Pius Msekwa, akizungumza baada ya mapumziko ya mchana ya kikao hicho, alikiri malumbano hayo kutawala kikao hicho na kusema; "Tunachofanya hapa ni kupokea taarifa ya hali halisi ya kisiasa ndani ya chama kwa mikoa yote ya bara na visiwani. Hiki siyo kikao cha maamuzi".

"Ni vikao vinavyofanyika mara kwa mara, lakini safari hii mimi ndiyo naongoza nikichukua nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa ambaye ni Rais. Yeye yuko nje, sasa tumeona ni vema niwepo hapa kusimamia na kusikiliza taarifa za wenyeviti wa mikoa yote," aliongeza Msekwa.

Kujivua Gamba
Akizungumzia kujivua gamba, Msekwa alisema baadhi wanahoji kwa nini jambo hilo haliendi kwa kasi ili kulikamilisha na hatua hiyo iweze kufika pia ngazi ya chini.

Makamu huyo alisema, ni kweli uamuzi huo wa kukisafisha chama ni wa NEC, lakini akatoa angalizo kwamba, "Tunachofanya sasa katika kutekeleza hili ni kitu kinachoitwa ‘Political Management.’ Hatuwezi kufanya jambo hili kwa shinikizo".

Alisema CCM ni chama cha siasa ambacho kinaendeshwa kwa mujibu wa taratibu zote za kiuongozi hivyo, hata utekelezaji wa maamuzi yake unapaswa kusukumwa kwa kanuni na misingi ya uongozi wa chama cha kisiasa na si vinginevyo.

Mkutano wa NEC
Mbali na suala la kujivua gamba inayotarajiwa kutawala mkutano NEC, mpasuko ndani ya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) nao unatajwa kuteka kikao hicho.

Kwa mujibu wa ratiba ya kikao hicho ambayo gazeti hili limefanikiwa kuiona jijini Dar es Salaam wiki hii na kuthibitishwa na baadhi ya wajumbe wa NEC, kikao hicho kitakaa baada ya kukamilika maandalizi yake ya msingi.

Msimamo wa Ndejembi
Katika hali inayoonesha kuzidi kufukuta moto ndani ya CCM, kada mkongwe wa CCM , Pancres Ndejembi, ameibuka na kusema kuwa rais ajaye anaweza kutokana na chama chochote ili mradi asiwe fisadi.

Ndejembi alisema kwa sasa Watanzania wana macho na masikio, hivyo hawawezi kuchagua mtu ambaye ni fisadi katika nafasi ya urais na kukemea watu wanaoendeleza malumbano wakati muda muafaka haujafika.

Ndejembi alitoa kauli hiyo jana katika mahojiano maalumu na Mwananchi Jumapili nyumbani kwake Mtaa wa Kilimani, Dodoma ambapo alisema mtu atakayechaguliwa kuwa rais ni lazima awe mtu safi asiye na doa ndani ya chama na Serikali kwa ujumla.

“Mabishano ndani ya chama hayafai, kwa kuwa ipo Katiba ya CCM ambayo inaelekeza jinsi watu wanavyoweza kutoa hoja. Kubishana katika vikao kuhusu urais ni ujinga unaotakiwa kukomeshwa mara moja,’’ alisema na kuongeza;

“Kama mabishano yao yanalenga urais basi watakuwa wamekosea kwa kuwa huu si wakati wa kujadili mambo hayo kwani Tanzania ina rais na anaitwa Jakaya Mrisho Kikwete sasa kwa nini waendeleze malumbano hayo katika kipindi hiki?’’

Alisema kuwa wanaobishana wamesahau kuwa Tanzania inaongozwa na mfumo wa siasa wa vyama vingi ambapo kila chama kitasimamisha mgombea wake na kuwa chama kitakachosimamisha mgombea safi ndicho kitakachoibuka na ushindi.

Kada huyo aliwataka Watanzania kutulia kwa kuwa wakati utafika ambapo watatakiwa kuangalia nani anafaa kuwa rais wao lakini kipindi hiki ifahamike kuwa hakuna mwenye mamlaka ya kutangaza habari za urais kwa kuwa bado kuna kipindi kirefu mbele yao.

Kuhusu mvutano ndani ya CCM, alikemea na kusema kuwa tabia iliyojengeka kwa sasa ni mbaya kwa sababu watu wanalumbana bila ya kufuata utaratibu wa chama.

Alisema watu wanaolumbana kwa sasa ndani ya chama wana ugomvi wao binafsi na wanaivuruga CCM.

“Hebu watafute kitabu cha Mwalimu kiitwacho ‘Tujisahihishe’ ambacho kiliandikwa kwa lengo maalumu la migogoro midogomidogo kama hiyo.’’

Ndejembi aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma 1982-2007 na katika kipindi hicho alikuwa Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Mikoa wa chama hicho.

Ole Millya na vijana
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, James Millya amekionya chama hicho na kueleza kuwa kama kinataka kuendelea kushika dola, kihakikishe kinakuwa karibu zaidi na kundi kubwa la vijana na kuwapa matumaini.

Akizungumza katika mahojiano na Mwananchi Jumapili jana, Millya alisema chama chochote cha siasa hakiwezi kukamata dola kama hakiungwi mkono na vijana ambao ndio wengi.

“UVCCM Arusha tunampongeza sana mlezi wetu Stephen Wassira akishirikiana na katibu wetu UVCCM, Martin Shigella kwa kufanikisha muafaka Arusha, tunaamini sasa tutasonga mbele kusaidia chama,” alisema Millya.

Hata hivyo, alisema angalizo ambalo analitoa sasa kwa CCM ni kuwasikiliza vijana na kuwa nao karibu ili iendelee kukamata dola.

Akizungumzia siasa za makundi ndani ya CCM, Millya alisema ni tatizo kubwa ndani ya chama hicho na kwamba linatokana na siasa za majitaka na ubinafsi.

Sir Kahama
Mwanasiasa mkongwe nchini, Sir George Kahama (82) naye ameishauri CCM na kuitaka kutambua kuwa ili nchi itawalike lazima pawepo demokrasia ya kweli kinyume na hapo, umma utachoka na kuingia mitaani kuleta vurugu.

Sir Kahama alitoa kauli hiyo hivi karibuni kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi Jumapili nyumbani kwake Dar es Salaam, kuhusu mustakabali wa kisiasa maendeleo ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini.


chanzo: Gazeti la Mwananchi