Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Sunday, November 6, 2011

Uraia wa nchi mbili shinikizo la mafisadi?

http://in2eastafrica.net/wp-content/uploads/2011/07/Bernard-Membe.jpg

Makala yangu juu ya uraia wan chi mbili utaua uzalendo, katika gazeti hili toleo namba 209 la Oktoba 26 hadi Novemba mosi, 2011, imezua mjadala mkubwa.  Nimepokea hoja mbalimbali kwa njia ya simu, nyingi za kuunga mkono na chache za vitisho kutoka kwa wapigaji wasiojitambulisha, nami nimeona vyema kuziweka wazi hisia hizo ili viongozi wetu wapate kuelewa mtizamo wa baadhi ya wananchi wanaowaongoza.
Kwa kuwa ajenda hii inaonekana kugusa na kuzua hisia kali za sehemu kubwa ya jamii ya Kitanzania, hasa kutokana na kauli nyingi za Waziri wetu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na kauli ya Rais, Jakaya Kikwete; aliyoitoa kwa Watanzania raia wa Marekani wakati wa ziara yake nchini humo hivi karibuni na kuwapa matumaini kwamba suala hilo linashughulikiwa kikamilifu. 
Kwa jinsi ninavyoiona ajenda hii, inaweza kutugawa Watanzania. Ni ajenda nzito na nyeti iliyowahi kutolewa kwa miaka 50 ya Uhuru wetu, ukiondoa ile ya mwaka 1962 juu ya “uraia”, iliyomgharimu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, nafasi yake ya Uwaziri Mkuu, kwa kujiuzulu na kurejea kijijini.
Hapa, nitatoa baadhi tu ya hoja nilizopokea kutoka kwa wasomaji kuhusu makala hiyo, kuonyesha jinsi jamii inavyoliona suala hili la uraia pacha kwa mtizamo na hisia hasi.
Awali ya yote, naomba ifahamike kuwa, si kwa Tanzania pekee kwamba hoja ya uraia pacha inatia hofu na kero.  Utafiti uliofanywa unaonesha kuwa, kati ya nchi 53 huru za Afrika, ni nchi 11 tu zimeonyesha kutaka uraia huo; 42 zilizosalia zimesema HAPANA!
Kati ya nchi 173 zinazounda dunia hii, ni nchi 17 (asilimia 9.8) tu zilizoridhia uraia pacha kwa sababu zinazofahamika.  Nchi hizo ni pamoja na Australia, iliyoanzishwa na wafungwa huru (ex-convicts) wa Kingereza miaka mingi iliyopita; Canada na New Zealand, ambazo hadi sasa zimo kwenye himaya ya Malkia wa Uingereza; Costa Rica na Columbia. Soma zaidi nenda http://raiamwema.co.tz/uraia-wa-nchi-mbili-shinikizo-la-mafisadi

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.