Ngoja leo
niyadadavue makosa yanayofanywa na wanawake wengi pale wanapoamua ni nani wa
kuoana naye:
1.
Kosa la kwanza, unaolewa na mtu ambaye unajua kabisa ni dhaifu
na mkorofi, ukitarajia kwamba ataondoa kasoro zake akiwa ndani ya ndoa. Hili ni
kosa kubwa. Kama huna furaha sasa na mtu kabla hujaoana naye, usikubali kuingia
huo mkenge. Huwezi kutegemea mtu kuadilika aiwa ndani ya ndoa.
2.
Kosa la pili, unaolewa na mtu asiye sahihi kwa sababu ya msisimko wa
mwili kimapenzi lakini si kwa sababu ya tabia zake. Kuwa mwangalifu na neno
“Nakupenda” neno hili mara nyingi maana yake ni “Nina uchu nawe.” Ndiyo
amevutiwa nawekimaumbile, lakini undani wa tabia yake unaujua? Hapa kuna mambo
manne… Kwanza, Je anapenda kutomfanyia binadamu mwenzie mabaya kama mabavyo yeye
hataki kufanyiwa? Pili, anaishi vipi na watu wengine? Anaishi vipi na watu ambao
ana uadui nao, Anawasamehe au analipiza visasi? Je anatoa misaada kwa masikini?
Tatu, je ni mkweli, anachokisema ndicho anachokifanya? Je anaaminika? Majukumu
anayoahidi kuyafanya anayatimiza? Nne, je anajipenda? Je ni mtu ambaye yuko
imara kimapenzi au ni mtu wa kuyumbayumba na asiye na msimamo? Sio mtu
akishauriwa na marafiki zake au ndugu zake huko, anakuja na maamuzi yasiyo na
kichwa wala miguu
3.
Kosa la tatu, unaolewa na mtu ambaye hamna malengo na
vipaumbele vya aina moja vya maisha. Je mna utashi wa aina moja? Kwa mfano ni
vyema mwanamuziki akaolewa na mwanamuziki mwenzie kwa kuwa anajua mzingira ya
kazi ya mwenzie ili kupunguza wivu wa kupindukia usio wa
lazima
4.
Kosa la nne, unaolewa na mtu asiye sahihi kwa sababu mnakutana
kimwili mapema mno. Kukutana kimwili kabla ya ndoa kunaweza kuleta matatizo
makubwa mno. Tendo la ndoa kabla ya ndoa hufunika uwezo wa mtu kufikiri. Mtu
anabaki kufaidi na kubaki kujali mapenzi ya kimwili na kusahau kukuna ubongo juu
ya mambo mengine. Ni lazima mwanamke akune ubongo ili kujua kama huyo mpenzi
anakidhi vigezo vyote vya mume mtarajiwa.
5.
Kosa la tano, unaolewa na mtu ambaye huna msisimko wa kimwili
umwonapo. Kuna uwezekano mkubwa mwanamke akavutiwa na mwanaume kwa sababu ya
aina ya gari analomiliki. Hapa hakuna msisimko wa kimwili bali mwanamke kavutwa
na gari au rasilimali alizo nazo mwanaume huyo.
6.
Kosa la sita, unaolewa na mwanaume anayependa kudhibiti. kuwa
na tabia ya kudhibiti wenzako ni ya dalili za mtu jeuri na mwenye kujisikia na
mfujaji. Naomba kutofautisha kati ya “kudhibiti” na “kutoa mawazo.” Mtu
anayekupa mawazo ni kwa faida yako, lakini anayekudhibiti ni kwa faida
yake.
7.
Kosa la saba, unaolewa na mtu asiye sahihi kwa sababu unakimbia
matatizo uliyo nayo. Unaweza kuwa hujaolewa na huna raha wala amani na ukataka
kuolewa. Ndo haiwezi kukutatulia matatizo yako binafsi ya kisaikolojia nay a
kimapenzi. Badala a kuyapunguza matatizo hayo, ndoa itayaoneza. Kama huna amani
na huyafuahii maisha, chukua jukumu la kurekebisha matatizo hayo sasa kabla
hujaolewa. Itakuwa ni faida kwako na kwa mmeo mtarajiwa.
8.
Kosa la nane, unaolewa na mtu asiya sahihi kwa kuwa yuko ndani
ya pembe tatu. Mtu ambaye anaishi na wazazi wake ni moja ya mfano wa mtu
anayeishi katika pembe tatu. Watu wengine wanaoweza wakawa wanaishi ndani ya
pembe tatu ni kama wanaofanya kazi saa 24! Huyu mtu halali? Watu wengine walio
katika pembe tatu ni watu wanaotumia madawa ya kulevya, mtu anayetawaliwa na
“hobbie” zake, anapenda sana michezo (Mpira), kuperuzi mitandao ya kijamii na
anapenda sana fedha. Hakikisha kwamba wewe na mpenzi wako , nyote hamtawaliwi na
pembe tatu. Mtu ambaye anatawaliwa na pembe tatu hawezi kumtimizia mpenzi wake
haja ya upendo atakapokuwa anahitaji. Kama mpenzi wako anatawaliwa na pembe tatu
kwa kiasi kikubwa, wewe huwezi kuwa kipaumbele chake.
Chanzo: http://kaluse.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.