Ngoja
niyadadavue malalamiko ya wanawake kwanza hapa chini:
1.
Wanawake wanalalamika kwamba wanaume sio waelewa wazuri, yaani huwa wanatafsiri
mambo tofauti na isivyo.
2.
Wanalalamika kwamba wanaume huwa hawajali hisia za wapenzi wao wala hawajali pia
kuhusu mahitaji yao.
3.
Wanalalamika kwamba wanaume huwa hawajui kuonesha upendo , yaani hata
wanapopenda inakuwa kama vile wanajisumbua tu, kiasi kwamba mwanamke anaweza
kuhisi kwamba hapendwi.
4.
Wanalalamika kwamba wanaume huwa hawana muda wa kucheza na wapenzi wao kabla
hawajafanya nao mapenzi yaani hawawaandai kabla ya tendo, wao huwarukia tu na
kumaliza haja zao haraka na kugeuka ukutani kabla ya wao (wanawake)
hawajaridhika.
5.
Wanalalamika kwamba wanaume hawana mawasiliano, huwa hawajui kueleza hisia zao
na mawazo yao, bali ni watu wa kunyamaza na kujifungia kwenye dunia yao wenyewe.
Wanahisi kama kuelezea hisia zao na mawazo yao ni kuwa dhaifu.
6.
Wanawake hulalamika kwamba, wanaume hawana muda wa kukaa nyumbani na familia
zao, kwa sehemu kubwa ni watu wa nje tu.
7.
Wanawake pia wanawalaumu wanaume kwamba, hawajali mustakabali wa usafi au
kupendeza kwa nyumba.
8.
Wanawake wanawalalamika kwamba, wanaume huwa wanafanya maamuzi yao bila kujali
kuwa wanawake wapo na wanaweza kuwa na michango mizuri sana kwa hicho
wanachotaka kukifanya. Huamua kama kwamba wanawake siyo sehemu ya
familia.
9.
Wanalaumu kwamba, wanaume ndiyo wanaoanzisha au kuendekeza kutoka nje ya ndoa
ukilinganisha na wao wanawake.
Malalamiko
ya wanaume nayo nayadadavua kama ifuatavyo…..
1.
Wanaume wanalalamika kwamba wanawake ni watu wa kulalamika, kukosoa na wenye
vijineno vya hapa na pale visivyo na maana na vyenye kukera.
2.
Wanaume wanalalamika kwamba wanawake wanajaribu sana kuwadhibiti na
kuwakandamiza pale wanapoachiwa nafasi kidogo.
3.
Wanaume wanadai kwamba wanawake huwa hawana furaha, mara nyingi wanaonekana kama
vile wako kwenye simanzi fulani na wanapenda sana kununanuna hasa pale wanaume
wanaposhindwa kuwatekelezea kile walichotaka hata kama hakina umuhimu kwa wakati
ule.
4.
Wanaume wanalalamika sana kwamba wanawake wanawanyima unyumba kama adhabu ya
kuwakomoa. Siyo kuwakomoa tu, bali huwa wanafanya hivyo kwa lengo la
kuwashurutisha wakubaliane na utashi wao fulani.
5.
Lalamiko lingine la wanaume kuhusu wanawake ni lile la kwamba, huwa hawafikirii
kwa mantiki, bali mara nyingi kufikiri kwao huwa kunakumbwa na mhemko. Kwa hiyo,
uamuzi wao mwingi hauangalii mantiki bali hujali zaidi hisia
zao.
6.
Wanawake wanalalamikiwa na wanaume kwamba, hali zao za kihisia huwa
hazitabiriki. Yaani huwa zinabadilika kufuatana na mabadiliko ya miili yao ya
kihomoni miilini mwao nyakati kama zile za siku zao(hedhi), nyakati za ujauzito
na hata wanapokoma kuziona siku zao(menopause) .
7.
Wanaume wanawalalamikia wanawake kwa tabia yao ya umbea, kwamba midomo yao
huwasha sana hadi waseme kile walichokiona au kukisikia hata kama si lazima na
pengine ni hatari.
8.
Wanawake wanalalamikiwa pia na wanaume kwamba, huwa wanatoka nje ya ndoa, hasa
wanapohisi kukosewa upendo ndani, jambo ambalo haliwezi kuleta suluhu kwa tatizo
hilo.
Kama wewe
ni mwanaume na umegundua kwamba moja au baadhi ya malalamiko ya wanawake
yanakugusa inabidi ubadilike na kufanya kinyume chake. Kama wewe ni mwanamke pia
hali ni kama hiyo. Kama kweli una mdomo mwingi kwa mfano, ujue wanaume hawapendi
tabia hiyo, hivyo huna budi kubadilika.
Chanzo: http://kaluse.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.