Na Lulu Mussa
Mkutano wa Tano wa Mawaziri wa Mamlaka ya ziwa Tanganyika ulifanyika jana mkoani
Kigoma, ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya mkataba uliounda mamlaka hiyo.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dk.
Terezya Huvisa amesema kuwa ili kulinusuru Ziwa Tanganyika jitahada za Nchi zote nne ni
muhimu katika kukabiliana na changamoto zinazolikabili ziwa hilo kwa sasa kwa kutumia
fursa zilizopo.
Amezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na uchafuzi mkubwa wa mazingira ikiwa ni
pamoja na kujaa kwa taka za majumbani na zile za viwandani, uvuvi haramu kutokana
na ongezeko la watu, kilimo na ufugaji usio endelevu. Hata hivyo Waziri Huvisa
amewakumbusha wajumbe wa Mkutano huo kuwa Ziwa Tanganyika linaunganisha Nchi zote
nne badala ya kuzitenganisha, hivyo ni muhimu kuwa na mikakati endelevu ya kuhifadhi ziwa
Miongoni mwa maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano huo ni pamoja na Utekelezaji wa
Mpango Mkakati wa Kitaifa ambao kwa sasa unafanya kazi katika nchi zote pamoja na
Mkakati wa kukusanya fedha kwa ajili ya kuwa na usimamizi endelevu wa Ziwa Tanganyika
baadaya ya mwaka 2013 ambapo fedha za wafadhili zitafikia kikomo.
Katika Mkakati huo wa kukusanya fedha Nchi zote nne zimetia saini makubaliano ya
kuchangia fedha ili hifadhi ya Ziwa hilo iwe endelevu, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa
miradi mbalimbali.
Mkutano huo umefanyika Tanzania kwa mara ya pili, mkutano mwingine kama huo ulifanyika
jijini Dar es Salaam mwaka 2007. Mamlaka hiyo ya Ziwa Tanganyika inaundwa na nchi za
Zambia, Burundi, Congo (DRC) na mwenyeji Tanzania.
Mjengwablog
No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.