Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Friday, March 2, 2012

Mastaa wakiri kushea mabwana



Wema.
Shilole.

Uwoya.
Na Waandishi Wetu
MINONG’ONO ya muda mrefu kuhusu mastaa wa kike Bongo kuchangia wanaume, sasa imepata majibu baada ya kuthibitika kwamba vitendo hivyo vimeshamiri sana miongoni mwao, Ijumaa linaifumua.
Habari zisizo na shaka zilizolifikia gazeti hili, zinasema kwamba mastaa hao wamekuwa wakipangwa bila kujijua na wakati mwingine wakiwa na taarifa ya mchezo mzima huku wakijua kufanya hivyo ni kuhatarisha afya zao.
MAMBO HADHARANI
Chanzo chetu, ambacho ni miongoni mwa mastaa wanaowika kwenye tasnia ya filamu, kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, alisema mtindo huo upo sana na umekuwa ukiibua mabifu baina yao.
“Haya mambo yapo, yaani hakuna amani kabisa, unakuta staa ana mpenzi wake, lakini bila kujua mwenzake anaanza kujitongozesha kisha naye anatoka naye,” alisema mtoa habari wetu na kuongeza:
“Hata huu mgogoro wa Wema (Sepetu), Wolper (Jacqueline) na Uwoya (Irene) chanzo chake kilikuwa mambo hayo hayo, sema walikuwa wanashindwa tu kuweka wazi.
“Ukweli Wema alikuwa analalamika kwamba Wolper anajipitisha tena kwa Diamond, wakati mwanzoni alimuacha akiwa hajawa maarufu. Uwoya naye hakuwa na imani na Wolper kwa madai kwamba alikuwa anajigonga kwa Ndikumana.”
Maelezo ya mnyetishaji wetu huyo yalienda mbali zaidi, yakisema kwamba, imefikia hatua staa akiwa na uhusiano na mwanaume wake anamficha kwa rafiki zake ili asitegwe.
“Hasa huku kwetu kwenye filamu ndiyo kuna haya mambo zaidi. Sijui hawaoni kinyaa?” alisema.

MASTAA WAFUNGUKA
Timu ya gazeti hili kwa nyakati tofauti lilifanya mahojiano na baadhi ya mastaa wa tasnia mbalimbali Bongo kuhusu madai haya, ambapo wengi walikiri.
Mmoja wa mastaa hao ambaye hakupenda kuandikwa jina lake gazetini kwa kuhofia kunyimwa dili, alisema wasichana ndiyo wamekubuhu zaidi kwenye mchezo huo ambao si wa kistaarabu.
“Nakwambia ukionekana unapendeza, unatunzwa vizuri na mwanaume wako, nao wanamuwinda ili wamtie mkononi. Ni tabia ya hovyo sana,” alisema msanii huyo, mweupe mwenye figa namba nane.
Mastaa waliopata kuzungumza na Ijumaa na kutoa ushirikiano ni Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, Aunt Ezekiel, Jacqueline Dustan, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Baby Joseph Madaha, Lucy Komba na Belina Mgeni, soma walichokisema hapa chini.

KABULA
“Tabia hiii ipo sana, kikubwa ni tamaa...mtu akiona upo na fulani anajua unafaidi, hivyo na yeye anajiingiza akijua atapata kama unavyopata kumbe hajui ni nyota ya mtu tu.”

AUNT
“Hiyo tabia ipo na si nzuri, kila mtu anatakiwa kumheshimu mtu ambaye alikuwa na uhusiano na rafiki yake ili kujenga heshima.”

JACQUELINE
“Tabia hiyo ni mbaya sana na ipo kwa mastaa wa hapa kwetu Bongo. Kiukweli haileti picha nzuri kabisa kwa jamii, unashindwa kueleweka.”

SHILOLE
“Najua kwamba wapo mastaa wenzetu wenye tabia hiyo, ila nawatahadharisha, kwangu mimi mtu asijaribu kabisa, nitamwangamiza! Siyo tabia nzuri, kwa kweli inakera.”

MADAHA
“Hiyo ipo kweli na ni kujivunjia heshima, unajua mwanaume wa shoga yako ni sawa na shemeji yako kwa dada’ko, sasa inakuaje unatembea naye? Inaudhi sana. Kiukweli hata jamii haituelewi.”
BELINA
“Mastaa wengi wamefanya kama ndiyo mchezo siku hizi, naamini ni tamaa tu ndiyo inawaponza na si kingine. Mtu aliyetembea na rafiki yako ni shemeji yako na hao wanaume wanatudharau sana kwa mtindo huo.”

LUCY
“Tabia  hiyo ni mbaya na ipo kwa mastaa wengi, kama tukiendelea hivi, hii heshima ambayo tunaililia, hatuwezi kuipata kamwe. Ni lazima mastaa tubadilike, tuheshimiane.”

WAKIRI KUAMBUKIZANA UKIMWI
Baadhi ya mastaa waliopata kuzungumza na Ijumaa walikiri kwamba mchezo huo ni hatari na ni rahisi kuambukizana ukimwi.
Jacqueline Pentenzel ‘Jack wa Chuz’, aliye staa katika kiwanda cha filamu Bongo, alisema: “Wapo wasanii wanadaiwa kuwa na ngoma, lakini piga picha kwa mapenzi yetu haya, unatoka kwa msanii huyu unakwenda kwa yule bila kinga, nini kitatokea? Lazima kuna kuambukizana hapo.”
Mwingine aliyezungumzia hilo ni Aunt ambaye alikuwa na haya ya kusema: “Mtu yeyote asipotumia kinga wakati wa kufanya mapenzi hiyo inakuwa ni ngono zembe na lazima atapata ukimwi ikiwa anayefanya naye atakuwa na maambukizi.”

KUTOKA KWA MHARIRI
Chondechonde mastaa wetu, ninyi ndiyo kioo cha jamii, ni vyema mkijiheshimu na kuthamini afya zenu. Kama unajijua una tabia hii acha kwa ajili ya kulinda staha yako.

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.