MAJADILIANO YA MADAKTARI YASHINDWA KUANZA LEO
Majadiliano
baina ya Serikali na Madaktari kuhusu madai yao yaliyowasababisha wagome mwezi
uliopita, yameshindikana kuanza leo (Alhamisi, Machi 1, 2012) baada ya
madaktari kutoka nje ya mkutano wakikataa kujumuishwa na makundi mengine ya
watumishi wa kada nyingine za afya wanaofanya kazi nao pamoja.
Baada
ya madaktari hao kukataa kuanza majadiliano na kutoka nje ya ukumbi wa mkutano,
makundi mengine yaliyobaki nayo yalikataa kuanza majadiliano bila ya kuwepo
madaktari.
Madaktari
hao wametoa sababu kwamba wasingependa kufanya majadiliano hayo na Serikali katika
kikao kinachojumuisha kada nyingine za afya kama wauguzi, wafamasia,
wanasayansi wa maabara za afya, wafiziotherapia na wataalamu wa mionzi kwa sabau
wakiwa pamoja madai yao hayatopewa uzito stahiki.
Majadiliano
hayo yaliitishwa na Serikali kufuatia maombi ya madaktari kwa Serikali ya
kujadiliana nao kwa pamoja kuhusu utekelezaji wa madai yao baada ya Mkutano wao
na Waziri Mkuu Februari 9, 2012 na kukamilika kwa kazi
ya kamati iliyoundwa na Waziri Mkuu.
Wakati
akihutubia Taifa jana (29 Februari 2012), Rais Jakaya Kikwete alieleza kwamba
amepokea taarifa kuwa Kamati aliyounda Waziri
Mkuu kushughulikia madai ya madaktari imekamilisha kazi yake na kuwasilisha
taarifa kwake. Kuanzia leo (01 Machi
2012) Serikali itaifanyia kazi taarifa hiyo na kuamua ipasavyo kulingana na
uwezo uliopo.
Serikali
bado inafanya jitihada za kuzungumza na madaktari na kada nyingine za Afya ili
waweze kurejea kwanye meza ya mazungumzo na kuanza majadiliano mapema
iwezekanavyo.
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
01 Machi 2012
Irene K. Bwire,
Email: irenekaki@yahoo.com
No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.