mpenzi mdau wa mtandao huu kwanza naomba radhi kwa picha hizi za kusikitisha ila ndio hali halisi ya mambo inatisha sana Kijana kizito Kimeya (28) mkazi wa kijiji cha Mkoga kata ya Isakalilo Manispaa ya Iringa akiwa Hospitali ya mkoa wa Iringa kupatiwa matibabu baada ya kuchomwa kisu na utumbo wake kutoka nje
Miguu ikiwa imekatwa katwa mapanga na wauwaji hao ambao hawakufanikiwa kutimiza azmayao
hapa utombo ukiwa nje baada ya kuokolewa na afisa mtendaji wa kata hiyo ya Isakalilo Iringa mjini
Ni vigumu kuamini kama kweli kuna binadamu na wanywa damu ila kutokana na matukio kama hayo ndipo unaweza kuamini kuwa wapo binadamu na wanywa damu baada ya watu wanne ambao majina yao yametajwa na kijana huyo kudaiwa kumchoma visu kijana huyo pichani baada ya kumfuma akiiba mahindi ya mabichi maarufu kama Gobo katika shamba lao Kijana huyo alichomwa kisu na kucharangwa mapanga na baada ya wahusika kutenda unyama huo walimchukua na kumweka katika mfuko wa sarufeti na kujaza mchanga na kisha kumtupa mtoni kabla ya na kusindwa katika maji kwa masaa zaidi ya matano na baadae maji kusaidia kuupasua mfuko huo na mchanga wote kumwagika na kijana huyo kujisaidia kujikokota hadi nje kavu na kukutwa porini siku ya pili yake majira ya saa 1 usiku na wasamaria wema.
Habari zaidi itakujia katika gazeti la Uwazi ama katika mtandao huu kesho
Chanzo: http://francisgodwin.blogspot.com/
Jisikie huru kabisa kuchangia lolote linalohusiana na jamii, uchumi, siasa, imani na elimu katika Blog yetu. Tunakaribisha habari, taarifa, picha za matukio, maoni na ushauri ili kuwekana sawa katika dunia yetu hii ndogo. Wote mnakaribishwa katika kuimarisha mshikamano wa kuleta mabadiliko ya kweli nchini mwetu!!
Pages
Forums
- Critical Analysis (11)
- Education Issues (15)
- Geology and Mining (21)
- International News (37)
- National News (147)
- Political Issues (67)
- Religious Issues (28)
- Social Issues (79)
- Sports (19)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.