Kwa uteuzi huo Silinde anaziba nafasi iliyoachwa wazi na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika ambaye amepangiwa majukumu mengine.
Wakati huo huo, Kurugenzi ya Bunge na Halmashauri ya CHADEMA, inatambua mchango mkubwa wa wabunge wa CHADEMA katika kuwasilishwa, kujadiliwa na kupitishwa kwa muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba wa mwaka 2011 katika mkutano wa sita wa bunge.
Kurugenzi ya Bunge na Halmashauri ya CHADEMA inatarajia wabunge kama walivyofanya katika hatua hii ya kwanza ya marekebisho yanayohusu tume na mchakato wa ukusanyaji maoni watafanya hivyo katika marekebisho yatayofuata ya sheria tajwa kuhusu utungaji wa katiba mpya kupitia bunge maalum la katiba na uhalalishaji wa katiba husika kupitia mchakato wa kura za maoni.
Ikumbukwe kwamba tarehe 20 Novemba 2011 Kamati Kuu ya CHADEMA ilipitisha azimio la “Kuwapongeza wabunge wote wa CHADEMA kwa hatua thabiti na sahihi walizochukua, kwa niaba ya wananchi wa Tanzania, kupinga Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 kusomwa kwa mara ya pili na kujadiliwa Bungeni bila ya wananchi kushirikishwa kwa ukamilifu kutoa maoni yao na muswada kuboreshwa kwa kuzingatia muafaka wa kitaifa.
“Kamati Kuu imewapongeza wabunge wa CHADEMA na wale NCCR Mageuzi kwa kususia vikao vya Bunge vilivyojadili na kupitisha Sheria hiyo kwani kushiriki kwao kungeipa uhalali wa kisiasa na kijamii Sheria ambayo haikuzingatia nia na haja ya dhati ya kuweka utaratibu wa kisheria utakaoiwezesha nchi yetu kupata Katiba Mpya yenye kuzingatia na kukidhi matakwa ya umma wa Watanzania”.
Imetolewa tarehe 12 Februari 2012 na:
Tumaini Makene
Afisa Habari wa CHADEMA
No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.