KURUGENZI ya Oganaizesheni na Mafunzo ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), inatoa taarifa kwa umma kuwa, tarehe 19, Februari, 2012, kutafanyika mkutano mkuu wa Wilaya ya Kichama ya Segerea, ambapo wajumbe wa mkutano huo watafanya uchaguzi mkuu kuchagua Kamati ya Utendaji ya Wilaya.
Nafasi za uongozi huo wa wilaya ya kichama ya Segerea, ziko wazi kufuatia viongozi wote waliokuwepo kujiuzulu mbele ya kikao maalum kilichofanyika Ofisi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA Februari 16, 2012, baada ya muda wao wa kukaimu kufikia mwisho.
Fomu za nafasi hizo zitaanza kutolewa leo Ijumaa, Februari 17, 2012 hadi Jumamosi, Februari 18, Makao Makuu ya CHADEMA na katika tovuti ya chama, www.chadema.or.tz.
Wajumbe wote wa mkutano huo wanatakiwa kuhudhuria kufanya kazi hiyo muhimu ya ujenzi wa chama na taifa kwa ujumla.
Imetolewa leo Dar es Salaam, Februari 17, 2012 na
Benson Kigaila
Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo CHADEMA
No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.