Naibu waziri waTamisemi Agrrey Mwanri
Mhandisi wa ujenzi wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Atu Mwaipyana kushoto akifikiri kwa makini
Mhandisi wa ujenzi wilaya ya Kilolo Atu Mwaipyana akisikitikia maamuzi makali ya Mwanri dhidi yake
Kazi mbaya ya Mhandisi wa ujenzi Kilolo ambayo imemweka pabaya zaidi
Karavati lilianza kubomoka baada ya barabara kutumia kwa muda mfupi Kilolo
Mwanri akiingia chini ya karavati kupima vipimo kama vinaendana na BOQ
Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Agrrey Mwanri ameuagiza uongozi wa mkoa wa Iringa kumwagiza mhandisi wa ujenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Atu Mwaipyana kuwasilisha Vyeti vyake vya elimu kuanzia elimu ya sekondari pamoja na chuo alichosomea taaluma hiyo kabla ya kuwajibishwa kuisababishia Halmashauri ya Kilolo hasara kubwa katika miradi ya ujenzi.
Pamoja na kukosoa utendaji mbovu wa wahandisi wa ujenzi katika Halmashauri zote ikiwemo ya Manispaa ya Iringa ,Iringa vijijini, Ludewa,Njombe ,Kilolo na Makete ,Mwanri alisema kuwa Halmashauri ambayo mkurugenzi wake na wahandisi wa ujenzi wanapaswa kupongezwa kwa kazi nzuri ni Halmashauri ya Mufindi pekee ndio imemfurahisha katika ziara yake mkoani Iringa.
Alisema kuwa pamoja na kukutana na wahandisi wenye mapungufu wengi katika Halmashauri za wilaya ila kwa mhandisi huyo wa wilaya ya Kilolo hajapata kukutana na mhandisi kama huyo ambae ameonyesha kutofahamu vema wajibu wa kazi yake..
Mwanri alitoa maagizo hayo jana katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo wakati wa majumuisho ya ziara yake katika Halmashauri za mkoa wa Iringa alisema majibu aliyoyapata kutoka kwa mhandisi huyo wakati akihoji usimamiaji mbaya wa miradi ya ujenzi ndio yaliyomfanya kuingia wasiwasi na elimu ya yake .
"Toka tumeanza kukagua barabara za wilaya ya Kilolo na miradi ya ujenzi katika wilaya hiyo majibu ambayo alikuwa akijibu kwa maswali aliyoulizwa ndio yalithibitisha kuwa mhandisi huyo hajasomea baada ya kushindwa kutetea ama kutolea ufafanuzi mapungufu mbali mbali katika miradi hiyo ".
"Mheshimiwa mkuu wa naomba kukueleza hapa kuwa mhandisi wa ujenzi wa wilaya ya Kilolo nimeagiza aniletee vyeti vyake vya elimu ....Kwani naona huyo hana sifa za kuwa mhandisi wa wilaya na inaonekana vyeti vyake vimefojiwa"
Mwanri alisema katika ujenzi wa kituo cha stendi ya Ikokoto jengo la choo limekamilika na kuanza kutumika kwa miezi 6 sasa ila hakuna hata mlango mmoja ambao kitasa chake kinafungika .
Katika hatua nyingine Mwanri ameagiza Halmashauri ya wilaya ya Kilolo kuingia mikataba na wafanyabiashara ambao wamejitokeza kujenga vibanda vya biashara katika stendi hiyo ya Ikokoto ikiwa ni pamoja na kujenga kituo cha polisi katika eneo hilo ili kuongeza hali ya usalama katika stendi hiyo.
Katika Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mwanri ataka mhandisi ya ujenzi katika wilaya hiyo kuwajibika pia kwa uzembe na kuwa nyumba tatu Kati ya kumi zilizojengwa Ludewa mjini kwa ajili ya watumishi zimejengwa chini ya kiwango wakati ,bati zilizotumika kuezeka bwalo la chakula Manda Sekondari kuwa chini ya kiwango na kuagiza jengo la nyumba ya mganga kata ya Lupanga lililokarabatiwa chini ya kiwango kuvunjwa ili kuepusha madhara kwa watumiaji .
Kuhusu wanafunzi kufanyishwa kazi majira ya masomo katika wilaya ya Ludewa alitaka mwalimu mkuu wa shule ya Luilo kuwajibishwa .
Pia kubomoka kwa daraja lililojengwa kwa ufadhili wa Japan kwa Kiasi cha shilingi milioni 96 baada ya kusimamiwa na NGOs kuwa suala la daraja hilo lazima Halmashauri itolee majibu .
Chanzo: http://francisgodwin.blogspot.com/
Halmashauri nyingine ambazo wahandisi wake wanapaswa kuwajibishwa kwa uzembe ni Makete na Njombe mji huku wakurugenzi wa Halmashauri zote za wilaya isipo kuwa Mufindi wameagizwa kutolea majibu kwa mapungufu yaliyokutwa katika miradi ya ujenzi katika maeneo yao.
Jisikie huru kabisa kuchangia lolote linalohusiana na jamii, uchumi, siasa, imani na elimu katika Blog yetu. Tunakaribisha habari, taarifa, picha za matukio, maoni na ushauri ili kuwekana sawa katika dunia yetu hii ndogo. Wote mnakaribishwa katika kuimarisha mshikamano wa kuleta mabadiliko ya kweli nchini mwetu!!
Pages
Forums
- Critical Analysis (11)
- Education Issues (15)
- Geology and Mining (21)
- International News (37)
- National News (147)
- Political Issues (67)
- Religious Issues (28)
- Social Issues (79)
- Sports (19)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.