KIKAO cha cha Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Vijana ya CCM (UVCCM) mkoa wa Arusha kimevunjika Jumamosi Februari 18 baada ya wajumbe wawili Mrisho Gambo na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya Karatu aliyetajwa kwa jina la Bayo kutunishiana misuli na baadaye polisi kuingilia kati.
Wajumbe hao walizipiga kavukavu baada ya Bayo kujaribu kumzuia Gambo kwa madai kuwa si mjumbe halali wa kikao hicho kilichokuwa kinaoongozwa na Kaimu Mwenyekiti , Esther Maleko ambaye alikaimishwa na Mwenyekiti James Ole Millya.
Esther ambaye ni Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arumeru alitumia busara kuvunja kikao hicho baada ya sintofahamu hiyo kusababisha Bayo kuchukuliwa na polisi, alikokua saa kadhaa pamoja na Gambo aliyekwenda huko kuandika maelezo.
Awali kabla kuibuka kwa vurugu wajumbe walilazimika kupiga simu kwa Katibu Mkuu wa UVCCM Martine Shigela kuuliza uhalali wa Gambo kushiriki kikao hicho na Shigela aliwajibu kuwa hakuna kikao chochote kilichiowahi kumsimamisha Gambo hivyo ni mjumbe halali na kutokana na majibu hayo ndipo Mwenyekiti wa Karatu alipoamua kujichukulia sheria mkononi kujaribu kumtoa Gambo kwa nguvu ndani ya kikao.
Chanzo cha kumtoa Gambo inaelezwa kuwa ni hatua ya mjumbe huyo kukataa kuungana na kundi la vijana wa arusha wakioongozwa na Millya ambao wanatajwa kuwa katika kambi ya mmoja wa wanasiasa wanaowania kuteuliwa na CCM kuwania Urais 2015.
zaidi:
http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/225126-viongozi-wa-uvccm-arusha-watwangwana

http://www.jamiiforums.com/
No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.