Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Monday, February 20, 2012

UBABE WA DERECK CHISORA WAMPONZA,APIGWA KWA HASIRA BAADA YA KUMTEMEA MATE MWENZIE


Wakati wanapimwa uzito asubuhi ya pambano Dereck Chisora kulia alimzaba kibao Vitali Klitschko kwa ubabe wa kipuuzi.Ila jamaa hakumrudishia na kuahidi kumshikisha adabu usiku wa pambano.
Kabla pambano alijaanza wakati wanaingia ulingoni Dereck Chisora kulia alimtemea Vitali Klischko maji usoni kama unavyoona pichani.
Mpambano ulipoanza Vitali Klischko alimaliza hasira zake namna hii.
Hakuishia hapo tu,aliendeleza kurusha mikono kama mvua ya mawe na kumsababishia Dereck wakati mgumu sana ulingoni,jionee mwenyeweeee.
Kama si uhodari wa kukwepa basi kijana Dereck Chisora alikuwa apigwe Knockout.
Mpaka mwisho wa pambano ni Vitali Klischko ndiye alikuwa bingwa japo kama unavyojionea pichani bondia Dereck Chisora  bado alikuwa anataka kuleta purukushani.
Dereck kulia baada ya pambano kuisha bado aliendeleza ubabe wake wa kijinga japo alipewa kipigo.

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.