Rhobi Chacha na Imelda Mtema
MWENYEKITI wa Tawi la CCM ambaye pia ni Mjumbe wa Nyumba Kumi (Balozi), Keko Machungwa jijini Dar es Salaam, Richard Rutta anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Kilwa Road kwa madai ya kumbaka binti yake mwenye umri wa miaka 16 (jina tunalo).
Kwa mujibu wa binti huyo ambaye anasoma kidato cha tatu katika shule moja ya sekondari jijini Dar, baba yake huyo alianza kumbaka tangu mwaka 2009 hadi ilivyobumbuluka hivi karibuni.
MWANZO WA MAJARIBU
Binti huyo alisema siku ya kwanza kuingiliwa kimwili na baba yake huyo…
Rhobi Chacha na Imelda Mtema
MWENYEKITI wa Tawi la CCM ambaye pia ni Mjumbe wa Nyumba Kumi (Balozi), Keko Machungwa jijini Dar es Salaam, Richard Rutta anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Kilwa Road kwa madai ya kumbaka binti yake mwenye umri wa miaka 16 (jina tunalo).
Kwa mujibu wa binti huyo ambaye anasoma kidato cha tatu katika shule moja ya sekondari jijini Dar, baba yake huyo alianza kumbaka tangu mwaka 2009 hadi ilivyobumbuluka hivi karibuni.
MWANZO WA MAJARIBU
Binti huyo alisema siku ya kwanza kuingiliwa kimwili na baba yake huyo ilikuwa usiku akiwa amelala chumbani ambapo mzee huyo mwenye miaka 72, aliingia na kumtaka walale wote huku akimpa vitisho kama angekataa.
Binti: “Mimi nilikataa, akanilazimisha akisema mama hatajua kwani amemuacha usingizini. Niliendelea kumkatalia na yeye akazidi kunilazimisha mpaka akafanikiwa kuniingilia kwa nguvu.
“Alivyomaliza, akaniambia iwe siri yangu kwani atanisomesha shule na kuninunulia begi na mahitaji mengine nikitaka, lakini akanionya kuwa siku nikimwambia mama atanifukuza nyumbani.”
Akizungumza mbele ya mama yake mdogo, binti huyo alisema kuwa, yeye na baba yake huyo waliendelea na mchezo huo mpaka mama yake alipofariki dunia, Novemba 17, 2011.
Akasema baada ya kifo hicho, akajua baba yake angeacha, lakini aliendelea kumtokea usiku na kumtaka ampe penzi huku akimuahidi mahitaji mbalimbali ya shule jambo ambalo lilimshawishi kukubali.
POLISI MARA YA KWANZA
Akasema: “Niliendelea na mchezo huo na baba kwani niliamini nikiwaambia ndugu, nitakosa vitu vya masomo nilivyoahidiwa.
“Lakini siku moja niliamua kusema kwa mama zangu wadogo, wakachukua jukumu la kwenda Polisi Kilwa Road, baba akaitwa. Alipofika akasema hatarudia tena mchezo huo.”
Hata hivyo, binti huyo alisema alipotoka polisi ndugu hao waliamua kumchukua kwenda kuishi naye Keko ambapo ni jirani na nyumbani kwa mzee huyo.
Akasema baadaye, alisafirishwa kwenda kuishi Dodoma kwa ndugu wengine.
LAKINI CHA AJABU SASA...
Ajabu ni kwamba, akiwa Dodoma, mzee huyo alitafuta mawasiliano akamtumia nauli ili arudi Dar ili kuendelea kujivinjari na penzi lao.
“Nikiwa Dodoma, muda mchache baba alinitumia nauli nirudi Dar kwani alikuwa amenimisi. Kweli nilirudi bila ya ndugu zangu kujua, nikafikia kwake.
“Kumbe kuna majirani waliniona wakaenda kuwaambia mama zangu wadogo ndiyo hivi juzi (Februari 11, 2012) baba na mimi tukakamatwa na Polisi wa Kilwa Road.
“Kule polisi tulikaa ndani wote, ila mimi nilitoka siku ya pili, baba alipelekwa mahakamani na hadi leo hii (Februari 14, 2012) yupo mahabusu Keko,”alisema binti huyo.
MAELEZO YA NDUGU
Aidha, wanawake watatu waliojitokeza wakati waandishi wetu wakihojiana na binti huyo walidai wao ni mama zake wadogo, walisema walishtuka kuwa mtoto wao anafanya mapenzi na baba yake toka kwenye msiba wa dada yao ambaye ni mama mzazi wa mwanafunzi huyo.
Ndugu hao walipomuuliza mtoto huyo kuhusu wasiwasi wao, aliwaambia ukweli hivyo wakaenda kuripoti polisi na mambo kumalizwa ‘kistaarabu’ kwa ahadi ya kutorudia tena mchezo wake huo mchafu.
Ndugu hao walisema, hivi karibuni waliambiwa na majirani kuwa, binti huyo amerejea toka Dodoma alipokwenda na sasa yupo kwa mzee huyo wakiendelea ‘kula raha’.
Ndipo walipoamua kwenda tena Kituo cha Polisi Kilwa Road, Dar es Salaam na kupewa RB yenye namba KIR/RB/765/2012-KUBAKA.
Wakasema mzee huyo alikamatwa na kushikiliwa kituoni hapo, baadaye mahakamani kujibu shitaka lake.
BINTI ANAPELEKWA KUPIMA UKIMWI, MIMBA
Baada ya ishu hiyo, binti huyo aliandikiwa Fomu ya Polisi Namba 3 (PF3) kwa ajili ya kwenda kupima Ukimwi, mimba na magonjwa mengine ya zinaa.
Akasema: “Namshukuru Mungu nimepima, nimekutwa sina maambukizi yoyote na pia sina mimba.”
MAANDAMANO MTAANI
Huku Richard akiwa mahabusu Keko, majirani zake waliandamana mtaani wakiwa wameshika mabango yenye ujumbe wa kumtaka mjumbe huyo ahame mtaani hapo kwani si mara yake ya kwanza kumwingilia mtoto wake huyo.
HISTORIA KWA UFUPI
Mzee Richard ni baba wa kufikia. Wakati mzee huyo anamuoa mama wa binti huyo ambaye ni marehemu, mwaka 1999 alimkuta ameshamzaa na kuishi naye kwa muda wote licha ya kwamba mlalamikiwa huyo ana watoto kwa mwanamke mwingine.
No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.