Hoja yake ni kubwa juu ya haja ya kukamia kurejesha dhahabu hii ya tanzania iliyotoweka.
Mwaka 1964 Mkonge ulichangia 65% ya mauzo yaTanzania nje, mwaka 2010 Mkonge umechagnia 0.1% ya mauzo nje ambapo ni takribani dola za kimarekani 11 milioni pekee zilizoingizwa na zao hili.
Mbunge huyo alisema Hali inapaswa kubadilishwa kwani Mkonge una faida nyingi sana na bei yake katika soko la Dunia inazidi kupanda siku hadi siku.
Aliitazama dhahabu hii ya shambani kwa midadi mikubwa
Akiwa shambani alielezea hisia zake kama mwalimu anavyofanya kwa wale wanaomsikiliza.
Alipotoka shamba alienda kuzungumza na wananchi na alihutubia kwa namna ile ile anayoifanya yaani kwa msisitizo.
Alipomaliza mkutano watu walishangilia kwa staili hii ya kumbeba juu kwa juu.
Chanzo: Lukwangule entertainment
No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.