Makamu Wa Rais wa Jamhuti ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakiwa na mavazi ya asili ya kabila la Kikonongo baada ya kuvishwa na kutunukiwa uchifu wa Kabila la Kikonongo na machifu wa Kijiji cha Inyonga Wilaya ya Mpanda wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Rukwa na Katavi jana Februari 19, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea shamba la mahindi la Waziri Mkuu Mizengo Pinda, lililopo Kijiji cha Vilolo wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Katavi na Rukwa jana Februari 20, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea shamba ufugaji wa Nyuki wa kisasa la Waziri Mkuu Mizengo Pinda, lililopo Kijiji cha Vilolo wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Katavi na Rukwa jana Februari 20, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mama Asha Bilal,akisalimiana na Mama mzazi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Albetina Kasanga, wakati wakiwa katika ziara ya Mkoa wa Katavi jana Februari 20, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Chanzo: Mjengwablog
No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.