Kupanga ni kuchagua ukizingatia idadi ya unaowapangia kutegemeana na malighafi uliyonayo
Jisikie huru kabisa kuchangia lolote linalohusiana na jamii, uchumi, siasa, imani na elimu katika Blog yetu. Tunakaribisha habari, taarifa, picha za matukio, maoni na ushauri ili kuwekana sawa katika dunia yetu hii ndogo. Wote mnakaribishwa katika kuimarisha mshikamano wa kuleta mabadiliko ya kweli nchini mwetu!!
Pages
Forums
- Critical Analysis (11)
- Education Issues (15)
- Geology and Mining (21)
- International News (37)
- National News (147)
- Political Issues (67)
- Religious Issues (28)
- Social Issues (79)
- Sports (19)
Friday, August 19, 2022
Maisha ya uyaya na changamoto zake
Hapo awali kulikuwa na msemo kuwa mayaya huamka Kombora na kulala Lala salama wakilinganisha na vipindi vya redio hii wakati ule wa redio Tanzania Dar es Salaam. Basi msomaji leo hii katika makala haya maalumu ya siku ya wafanyakazi Duniani inayofanyika Mei Mosi ya kila mwaka tunayajibu maswali haya:Yaya anapatwa na matatizo gani akiwa kazini? Wana haki zipi na Je hali mayaya huko ughaibuni ikoje?
Miaka ya hivi karibuni tumeshudia huitaji mkubwa wa mayaya majumbani, mikahawani na ata katika maofisi ya kibalozi. Hilo linatokana na nchi kusonga mbele, kwani katika nchi zinazoendelea hivi sasa kati ya asilimi 4 mpaka 10 ya watu wa mataifa haya likiwamo taifa letu wanajishughulisha na kazi za majumbani.
Mwaka 2008 yaani miaka sita iliyopita shirika la kazi Duniani ILO lilibainisha kuwa watu Milioni 100 duniani kote , mkono huenda kinywani kwa kazi hizo. ILO inapambanua kuwa kuongezeka kwa majukumu ya majumbani, kukosekana kwa sera sahihi na zenye mizani kwa wafanyakazi wenye majukumu mengi ofisini mathalani ujauzito na likizo na kukuwa kwa maendeleo ni ithibati tosha ya kuongezeka kwa mahitaji ya mayaya majumbani.
Maoni ya viongozi wa CHODAWU
CHODAWU ni chama chenye dhamana ya wafanyakazi hawa nchini Tanzania na Bi Deoglasia Vuluwa ni miongoni mwa maafisa waandamizi wa chama hiki.“Mfanyakazi wa kazi za ndani anapaswa kuheshimika kama mfanyakazi mwingine kwakulipwa mshahara stahiki mathalani mfanyakzi wa kawaida anatakiwa kulipwa elfu arobaini kwa mwezi kama anaishi nyumbani kwako na anaishi nyumbnai kwake mshahara wake unatakiwa kuwa zaidi.”Anasema Bi Vuluwa
Jamii za kiafrika wakati na ata baada ya ujima zimekuwa na mgawanyiko wa kazi, kuna majukumu ya wanawake na ya wanaume . Wanaume wakijishugulisha na kuzalisha mali huku akinamama wakitekeleza na mambo ya uzazi na nyumbani.
Mintarafu ya majukumu hayo ya kimaumbile, mahitaji kwa sasa yameongezeka sana hasa ya kuwatunza watoto na kazi nyingine majumbani. Wanawake wa leo wanafanya kazi ambazo zinaiongezea kipato kaya husika. Nako majumbani majukumu yakiongezeka mzigo huo wanatishwa wafanyakazi wa majumbani kwa hivyo soko la huhitaji wa mabinti lipo juu.
“Wafanyakazi wa majumbani wanapaswa kuheshimiwa mno na siyo kuwalisha makombo na kuwapa ujira mdogo, nimeshudunia kuna familia wanalipwa elfu ishirini yaani elfu kumi kumi mbili tu tunapaswa kuheshimu kazi hizi.”Anabainisha mdau mmoja Mkoani Dar es Salaam.
Kutokana na mtazamo kuwa majukumu ya nyumbani ni ya wanawake kumefanya jamii nyingi kuona kuwa ata haki ya umiliki wa mali zote za majumbani ni za wanaume hili linaoneka ata hii leo katika hatua mbalimbali za maamuzi ya mahakama mathalaini pale migogoro ya ndoa inapotokea. Mchango wa mwanmke kulea na kutunza nyumba hauna thamani. Mathalani katika kesi ya ndoa ya Omari Chikamba dhidi ya Fatuma Malunga shauri nambari 39 la mwaka 1989 la mahakama kuu palionekana mtazamo huu. Ninaweza kusema kuwa hilo ndilo linalosababisha ata uthamani wa kazi za majumbani kutopewa hadhi ya juu.
Bibi Chungu Wagala na Kiongozi wa CHODAWU Mkoa wa Dar es salaam anazitaja haki zaidi za mayaya kuwa ni kwenda likizo, kupewa kazi nyepesi akiwa mjamzito na kuheshimu sheria zote za kazi kama mfanyakazi mwingine.
Kazi hizi mara zote zinafanywa na vijana ambao ndiyo kwanza wnayaanza maisha na mara nyingi wanakuwa wamemaliza elimu yao ya msingi na wachache sana huwa wamepata elimu ya sekondari.
Mwaka 2006 , Benki ya Dunia ilisema kuwa katika nchi nyingi zinazoendelea kusini mwa jangwa la Sahara idadi ya watu inaongezeka kwa kasi. Inabainishwa zaidi kuwa idadi ya vijana ifikapo mwaka 2050 vijana kati ya umri wa miaka 15-24 itakuwa kubwa mno barani Afrika na Asia. Ingawa idadi hiyo ikiongezeka hakuna hima inayofanyika kuongeza ajira ya vijana hawa ambapo kwa nchi ya Kenya vijana kati ya miaka 15-30 ambao ni asilimia 32 ya wakenya wote inakadiliwa asilimia 25 tu ndio wanaopata ajira ambazo nyingi ni za kawaida kama za wakaka na wadada wa kazi.
Hapa nyumbani Tanzania vijana wa kati ya miaka 15—34 ni asimiia 56 ya Watanzania wote ambapo theluthi ya hao wapo vijiweni wakizamia katika kazi za majumbani kama vijana wenzao wa Kenya.
Kisa cha dada Mfilipino
Hali imekuwa na ahuweni kwa wasichana kuliko wavulana kutokana na mtu anayeweza kufanya kazi za nyumbani ni mwanamke tu kuliko mwanaume kwani wasichana wengu hupata kazi hizi. Hali hii inasababisha baadhi ya vijana hao kukimbilia ng’ambo ili wakiamini kuwa huko kazi zina nafuu. Lakini hali ya huko si salama kweli Kama anavyothibitisha dada huyo mfilipino aliyekimbilia Katari.“Kufanya kazi majumbani nchini Katari ni pagumu sana, nimekuja mwaka 2008 miaka kadhaa iliyopita wakati nafanya kazi na mwajiri wangu wa awali, hakunipa chakula, mishahara ilicheleweshwa na hakukuwa na muda wa kupumzika. Kwa siku nilifanya kazi saa 14 kazi nikianza saa 12 asubuhi.
Ukilala, kama wao wameamka wakitaka uwatayarishie chochote huna budi kuamka na kutekeleza hilo, huku majukumu mengine ya kupika na kupokea simu zao kila mara wanapohitaji kuuliza jambo hapo nyumbani, sasa kwanini yaya afanye kazi bila ya kula na hakuna muda wa kupumzika na kulala. Ata mikataba haitiliwi maanani. Katika mkataba wangu natakiwa kulipwa dola 400 lakini nalipwa dola 200 tu . Mbaya zaidi ata kibali changu cha kusafiria kilichukuliwa na mwajiri wangu.
Niliruka jivu na kukanyaka moto, mwajili wangu wa pili alikuwa hatari zaidi, yeye alitaka kunibaka ndani ya chumba changu. Alinipa pesa ambayo niliikataa na kukataa kufanya nae ngono. Kwani kufanya hivyo halikuwa jukumu lililonipeleka . Nilifika hapa kufanya kazi kwa manufaa ya familia yangu na siyo michezo hiyo Kukataa kwangu kulisababisha kuondoka kwake niliacha kila kitu changu isipokuwa nguo zangu na pesa ya nauli ya Taxi tu iliyoweza kunipeleka kwa mwajiri mwingine.
Sasa kila nimuonapo mwanaume wa hapa katari naogofya mno, nadhani watanikamata, kunifunga na kunirejesha kwetu Ufilipino
Sasa nikirudi huko, Je familia yangu watakula nini? Kwa hiyo haina budi nijifiche tu na kufanya vibarua vya muda ili nipate pesa ya kupeleka kwetu. Kwa kweli hapa Katari ukiondoka kwa bosi wako ni tatizo kubwa kwani utakosa uhalali wa kufanya kazi na vibali vyako vyote vitapotea. Unaweza kupata kazi ya muda lakini wakigundulika wamekupa kazi wanalipishwa faini na mie nitarudishwa kwetu.
Hivi sasa nimepanga nina chumba kidogo na najinunulia chakula .Pia nina Kigali kidogo ila kikikaguliwa na polisi ni tatizo kubwa. Bado nahitaji kuishi huku . Nahitaji kufanya kazi ili nipate kibali cha kuishin huku kutoka uhamiaji.
Ninadhani kibali changu kipo Basmutaba eneo ambalo nilikaguliwa vidole vyangu hapo awali. Ninajaribu kutafuta msaada kutoka idara ya CID lakini hawajanipatia kibali changu hadi leo
Kibali hili kilitoka 2011 ili nikipate natakiwa kulipa rila 6500 na rila 6000 kupata mwajiri mwengine halali. Natakiwa kulipia tiketi ya kwenda na kurudi nyumbani na kulipa faini ya rila 10 kila siku tangu mwaka 2008 mpaka leo hii. Kwa hiyo natakiwa kulipa rila 19500 wakati nafanya kazi ya muda mfupi tu huo mshahara wenyewe, vipi familia yangu Ufilipino sijui watafanya nini
Kulingana na ripoti Human Right watch ya Aprili 23 mwaka inabainisha kuwa hali ni mbaya katika taifa hili linalojiandaa na kufanyika kwa Kombe la dunia la mwaka 2022. Nchini nyengine zenye hali hii ni Saudi Arabia na Imarachi ambapo mfanyakzi wa ndani kwa juma zima anafanya kazi zaidi ya saa 100 ambapo ni sawa kwa siku anafanya kazi saa 17 ambapo kihalali mfanyakazi anatakiwa kufanya kazi saa 8 kwa siku ama kama kutakuwa na ziada ya kazi basi kutakuwepo na malipo ya ziada kwa muda unaongezeka.
Tume ya usuluhishi na mahakama ya kazi
Panapokuwepo na unyanyasaji wowote nchini petu sheria ya kazi ya mwaka 2004 na kanuni zake za mwaka 2007 zinatoa nafasi ya muhusika kupeleke suala hilo Kwenye Tume ya Usuluhishi na uamuzi yaani CMA ata mayaya wana nafasi hiyo kisheria lakini ni ukweli ulio wazi kuwa mayaya wengi wamekuwa hawana mikataba ya kazi ambayo inaweza kuwasaidia pale hali inapokuwa tofauti. Kwani mkataba ndiyo uthibitisho pekee wa mtu kufanya kazi sehemu fulani na ndipo sehemu pekee panapoweza kubainisha haki na wajibu wa kila mmoja . Chakusikitisha kwa muda mrefu uajiri wa wafanyakazi za ndani inatumia mitindo ya kijamaa na kidugu huku wengine wakiwaita binti na kaka wa wa kakazi kaka,/dada , wakimaanisha kuwa ni sehemu ya familia zao lakini vitendo vimekuwa kinyume. Ukweli uliowazi kuwa yaya au kaka wa kazi si ndugu ni mwajiriwa sehemu husika hivyo ni wajibu wa kila mmoja kutenda haki stahiki.Mashauri ya mayaya mahakamani
Kwa hakika hali ya unyanyasaji wa mayaya imekuwa ni tatizo kubwa dunia ebu soma kisa hiki cha binti Mtanzania. “Mahakama ya kazi nchini Uingereza ilitoa hukumu ya ushindi kwa binti yaya Mtanzania Bi Elizabeth Kawongo kwa kulipwa Paundi 58,583 sawa na milio 130 kwa wakati huu kutokana na kutolipwa mishaharayake , kutopewa nafasi ya kupumzika na kufanywa mtumwa.Watuhumiwa walikabiliwa na tuhuma nyingine za kibaguzi kwa mfanyakzi huyo. Mahakama hiyo ya Watford ilitoa uamuzi wake dhidi ya Ramadhani Dhanji na mkewe Kudra Dhanji waliokuwa ni wazazi wa Zainab Alibhai Muingereza aishie nchini Tanzania. Bi Zainabu Alibhai alimchukuwa binti Elizabeth Kiwango na kumpeleka Uingereza kufanya kazi ya uyaya.
Mahakama ilijulishwa kuwa baadaye Elizabeth aliambiwa kuwa hatorudi naye Tanzania atabaki uingereza akiwa yaya kwa Mama wa Alibhai. Elizabeth alitumikishwa sana na alipomwomba mama Alibhai waweze kurudi wote Tanzania, Ombi hilo lilipokelewa na sikio lisilo sikivu. Badala yake ya kufanya kazi kwa wazazi wa Bi Alibhai, Binti Elizabeth alipelekwa nyumbani kwa ndugu mwingine wa familia hiyo akifanya kazi za ndani kama vile kufua kupika na kufanya usafi.
Mtu kwake na mkataa kwao mtumwa, alipofika huko kila alipouliz na kuomba kurudi nyumbani Tanzania aliambiwa kuwa kuwepo Ulaya kwake ni ngekewa, ingawaje binti huyo alilazwa jikoni tena sakafuni na wakati wa baridi kali. Akila makombo na vyakula vilivyopita muda wake.
Mungu bahati, siku moja aliomba ruhusa ya kwenda kusali , alilopata ruhusa hiyo alipofika kanisani aliwaeleza jamaa wengine kwa yaliyomsibu ndipo walipoweza kufanikisha kuonana na ubalozi wa Tanzania na chama cha utetezi wa wanawake na kufanikisha kupata kibali chake cha kusafiri na kurudi nyumbani Tanzania lakini ndugu Dhanji aliomba suala hilo limalizika kimya kimya kwa kumpa Elizabeth paundi 380 ambapo Eliza alizikatata hadi suala lake lilipomalizwa na mahakama.”
Wakati wafanyakazi wote wakisherekea siku hii ni wajibu wa kila mmoja wetu kuthamini mchango wa mabinti na kaka wa kazi majumbani kwetu . Basi kwa Kisa hicho ndiyo naufunga ukurasa wa makala haya ya siku ya wafanyakazi duniani. Kumbuka Leo hii tulitupia jicho suala la wafanyakazi wa majumbani
~Ngugi wa Thiong'o wrote:
Raila had refused to eat.He was on hunger strike. .He grew thin and pale.His right palm had gone dark,the arm had pimples and boils as well. He was receiving extraordinary punishment. He stood for his words. Dictators had to go. Moi had to go.
I had been initially jailed for a year by the Kenyatta's regime. For criticising the government acts on my book,, "l will marry when I want". I had set up a revolutionary theatre ,this provoked the dictatorial regime. I was jailed for a year.
Odingas's was involving. Seven years already in jail. He kept his words. Kenya needed a fresh air. He was willing to pay the price. I felt touched by his story. When I came to see him, he was denied a chance to talk to me. However he wisely did it in a writing. "Tell lda to ask the doctor to prescribe me these drugs, am slowly dying ".
Soon his mother died.His other relatives including his aunt followed. He would never be allowed to attend any of the burrials. It was painful. It was Real torture.
He remained in detention without trial. The government would not allow it. Soon he was transfred to Kamiti maximum prison. He was taken the torture corner. The isolation block. The detention camp. A prison within a prison. Here he was daily served with half cooked ugali with vegetable water with a few limp leaves floating around. And for the first time in two weeks, he was served with food.
The blows to his head dazed him.He fell on the floor and lay there. Rono,a GSU officer, and others jumped from his head to his genitals.His left leg twisted and was confirmed broken. He was either going to speak the truth or become a dead meat. He waited for the end, but it did not come. But still Odinga refused to give in. ...
Raila Odinga genuinely fought for our second liberation,
(Copy and paste)
Saturday, June 7, 2014
MASHABIKI MILIONI 3.5 KUTAZAMA MECHI 64 ZA KOMBE LA DUNIA BRAZIL
MWENZI WA MAISHA YAKO! TAFUTA KITABU HIKI KIKUONGOZE KUMPATA ANAYEKUFAA, KINAZINDULIWA KESHO MWANZA
Wednesday, June 4, 2014
MASKINI TEMBO WETU, WAMEKOSA NINI JAMANI?
Tembo kama huyu pichani anauawa kinyama na wendawazimu wachache ambao wanaangalia maslahi yao ya kuuza meno yake bila kujali hatma ya baadaye ya rasilimali zetu.
Zimekuwepo operesheni nyingi nchini, miongoni mwazo ni ile ya Tokomeza Ujangili iliyoendeshwa mwaka 2013, ambayo ilisitishwa baada ya kudaiwa kwamba wasimamizi wake waliendesha vitendo vya utesaji kwa wale walioshukiwa kujihusisha na ujangili.
Lakini pamoja na kusitishwa huko, bado kikwazo kikubwa kinaonekana kipo serikalini, kwani tunaelezwa kwamba wapo maofisa wakubwa wanaojihusisha na biashara hiyo haramu, na wanatengeneza mamilioni ya fedha.
Ndugu zangu, lazima tuwe wazalendo, tuungane kwa pamoja kupinga unyama na ujambazi huu ambao kama hatukisimama imara unaweza kuwapukutisha hayawani wote nchini na tukabaki na picha za wanyama kwenye vitabu vyetu vya historia. Tembo ndiye mnyama mkubwa kabisa aliyesalia duniani katika jamii zile za dinosaur, hivyo ni urithi mwingine kwa vizazi vyetu.
Ndugu yenu,
Daniel Mbega,
Iringa - Tanzania
Ndugu zangu,
Ujangili umeendelea kushika kasi nchini Tanzania, hasa wa tembo, licha ya jitihada kadhaa zinazofanywa na mamlaka husika.
Tembo kama huyu pichani anauawa kinyama na wendawazimu wachache ambao wanaangalia maslahi yao ya kuuza meno yake bila kujali hatma ya baadaye ya rasilimali zetu.
Zimekuwepo operesheni nyingi nchini, miongoni mwazo ni ile ya Tokomeza Ujangili iliyoendeshwa mwaka 2013, ambayo ilisitishwa baada ya kudaiwa kwamba wasimamizi wake waliendesha vitendo vya utesaji kwa wale walioshukiwa kujihusisha na ujangili.
Lakini pamoja na kusitishwa huko, bado kikwazo kikubwa kinaonekana kipo serikalini, kwani tunaelezwa kwamba wapo maofisa wakubwa wanaojihusisha na biashara hiyo haramu, na wanatengeneza mamilioni ya fedha.
Ndugu zangu, lazima tuwe wazalendo, tuungane kwa pamoja kupinga unyama na ujambazi huu ambao kama hatukisimama imara unaweza kuwapukutisha hayawani wote nchini na tukabaki na picha za wanyama kwenye vitabu vyetu vya historia. Tembo ndiye mnyama mkubwa kabisa aliyesalia duniani katika jamii zile za dinosaur, hivyo ni urithi mwingine kwa vizazi vyetu.
Ndugu yenu,
Daniel Mbega,
Iringa - Tanzania
source: MASKINI TEMBO WETU & www.mjengwablog.com