Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Wednesday, February 29, 2012

Uranium mining dangers downplayed, belittled by government officials with vested interests

DANGERS OF URANIUM MINING DELIBERATELY PLAYED DOWN

Tanzanian officials continue to play down the dangers of the proposed
Uranium mining project inside the UNESCOs World Heritage Site Selous
Game Reserve, according to some experts consulted almost deliberately
endangering the health of local populations for the sole motive of
profits. They have been bought, that much is clear, and when they say,
like the Commissioner for Energy, that playing with Uranium is safe
they are misleading the public for the simple motive of profits. There
is a very serious risk of pollution, and the former Soviet Union is a
very good example for that, there they are struggling until today with
the mess and fall out of those Uranium mines, poisoned water sources
and poisoned soil said a regular conservation source from Dar es
Salaam while passing on the information overnight. The Tanzanian
government has applied to UNESCO to get permission to commence mining
in the reserve or else excavate the area earmarked for mining, but as
rivers flow through the proposed mining areas into the reserve and
then on to the Indian Ocean, fears are growing of contamination of the
water with devastating effects for people, wildlife and eventually
marine life, with the long term effects not possible to mitigate away.
There are however also other areas of the country where Uranium
deposits have been found and where the focus of environmental groups
has been less until now.

Development partners too are concerned that the portion of revenue
coming to the Tanzanian government seems outrageously low, confirming
doubts on the value of the deal or else suggesting that the true value
will go elsewhere, and your guess here is as good as mine.

Interesting enough were comments attributed to a senior staff of an
Uranium exploration company, who was subsequently quoted in the local
media warning of lasting liver damage to those drinking water which
has been in contact with Uranium with other health problems due to the
toxicity not fully explored at this stage.

While government in full mouthed statements heap praise on their
policies and regulations, it is often a sad fact that those are
trampled upon and discarded when money starts to flow as has often
been seen in other sectors across the economy, giving little
confidence that it would be any different here. NEMA officials
reportedly also decried the low capacity of monitoring and
enforcement, suggesting further that government would largely have to
rely on data by the mining companies, which could easily be doctored
or present it such a way as to suggest minimum risks, many of which
would only become apparent in the longer term.

Stakeholders operating into the Selous have also expressed concern
over the ongoing negative publicity surrounding Africa largest game
reserve, with one, on condition of anonymity saying: We are worried
about this controversy. Tourists are easily put off and they can now
find on their computers anything you people write and expose. Like
your story about Stieglers Gorge has raised a lot of questions
overseas and government should come out and make a statement that they
will leave the gorge intact and not built a power plant there. The
same for mining of Uranium. There are a lot of issues with poaching
and government should concentrate on that, to open up the Selous into
the distant unexplored places so that more tented camps can be put up,
more visitors can come in and sustainable revenue can create jobs and
earn us Forex. That is the way forward for us. Spoken with the heart
of a true conservationist. Watch this space.

http://wolfganghthome.wordpress.com/2011/11/18/tanzania-conservation-news-uranium-mining-dangers-downplayed-belittled-by-government-officials-with-vested-interests/

Mitt Romney ashinda uteuzi wa Republican

Mitt Romney ashinda uteuzi wa chama cha Republican jimbo la Michigan


Mgombea anayepigiwa upatu kushinda uteuzi wa urais wa chama cha Republican katika uchaguzi mkuu wa mwezi novemba nchini Marekani, ameshinda uteuzi wa chama hicho katika jimbo la Michigan alikozaliwa.
Romney alishinda uteuzi huo baada ya kinyanganyiro kikali dhidi ya mpinzani wake wa karibu Rick Santorum.
Ushindi huo katika jimbo la Michigan umeonekana kuwa muhimu kwa bwana Romney kujikatia tikiti ya chama hicho kupambana na rais Barrack Obama.
Ameshukuru waliompigia kura na kuahidi kuendelea na juhudi zake za kutafuta uungwaji mkono.
Wachanganuzi wa masuala ya kisaisa wanasema ushindi wa Romney utampa nguvu zaidi hasa kwa kuwa kura za maoni zilikuwa zimeashiria kuwa mgombea mwenzake Bw Santorum huenda angeshinda.
Mitt Romney vile vile ameshinda uteuzi wa chama hicho katika jimbo la

BBC

Dkt. Bilal Amaliza Ziara Iringa

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Iwawa baada ya kuzungumza nao wakati akimaliza ziara yake ya Wilaya ya Makete Mkoa wa Iringa jana Februari 28, 2012.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti cha kumiliki hisa katika Benki ya Wananchi (NJOCBA), Olive Luena, bada ya kuzindua rasmi benki hiyo iliyopo Wilaya ya Njombe mkoa wa Iringa jana Februari 28, 2012.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha SAO Hill, Nick Moore, hukusu ufanyaji kazi wa mashine mpya nay a kisasa ya kuchana mbao iliyofungwa katika kiwanda hicho, wakati alipofika kiwandani hapo jana Februari 28, 2012, kilichpo Wilaya ya Mafinga mkoa wa Iringa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya silaha ya jadi ya kabila la Wahehe (Mkuki) kutoka kwa Mjukuu wa Chifu Mkwawa, Ignas Muyinga, baada ya kumaliza kuzindua kituo cha afya na kuwahutubia wananchi wa Kijiji cha Lungemba, Wilaya ya Mafinga mkoa wa Iringa, jana Februari 28, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wananchi wa Kijiji cha Lungemba baada ya kuwahutubia wananchi hao, Wilaya ya Mafinga mkoa wa Iringa, jana Februari 28, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE-IRINGA

 
http://mbungeiringamjini.blogspot.com/

mikutano ya chadema yaendelea iringa mjini moto wa msigwa haushikiki.


akina mama wamtwivila wakijipanga kununua kadi za chadema
 
Mhe. Msigwa akicheza na wanachama wa chadema wakati wakichangia chama.
katika mkutano huu wananchi walichangia Tsh.52000, pichani diwani kata ya mivinjeni chadema Mhe. Nyalusi.

akina mama wafurahia chadema
mitaa ya mtwivila watu wakishangila chadema mara baada ya mkutano.

umati wa wananchi wa mkwawa ukimsikiliza msigwa katika mkutano mkubwa ulio fanyika siku ijumaa.
ikiwa hata bibi wazee walikuepo kumsikiliza msigwa, hii nidhahili kuwa chama kinaungwa mkono na rika zote.
pamoja nakuwepo kwa mvua iliyo taka kuzuia mkutano, lakini watu walimuomba msigwa aendelee kuhutubia, wengine wakitumia viti kujikinga na mvua kama inavyo onekana katika picha juu.
vijana wakimsikiliza kwamakini Mhe. Msigwa.

peeeepoooooooozz?????? POWER
                                      
Mbunge Msigwa akiwahamasisha wananchi

akihutubia umati ulio kuwa ukimsikiliza kwa makini.
moto wa msigwa waendele kupamba katika maeneo mbalimbali ya jimbo la iringa huku leo katika maeneo ya mivinjeni zaidi ya wanchama wapya 60 kujiunga na chadema, muendelezo huu wa ufunguzi wa matawi ya chadema wananchi wameweza changia zaidi ya sh laki mbili na nusu wakati leo pekee ni shilingi 80000 ileweza changwa na watu katika harambee hizo, huku akina mama wengi kujitokeza kujiunga na chadema nakuonekana kumuelewa zaidi Mhe Msigwa kwamba si mbunge wa kuwapa samaki bali ni mbunge wa kuwafundisha kuvua samaki.

mbunge msigwa akisikiliza nakujibu maswali kutoka kwa wanchi.

 60 wajiunga chadema l ipogolo.



JK: Hatutaki Rais mzee 2015


na Nasra Abdallah
WAKATI makundi ya urais yakijipanga kuwania kiti hicho mwaka 2015, bila kuyajali, Rais Jakaya Kikwete amesema wanaota urais wakiwa na umri kama wake, wasahau, Tanzania Daima Jumatano limedokezwa.
Kikwete alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kilichokutana juzi, pamoja na mambo mengine, kupitisha jina la mgombea ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilisema kuwa Rais Kikwete alitoa kauli hiyo wakati akifungua kikao hicho.
Kwa mujibu wa habari hizo, Rais Kikwete alisema kuwa kinachotokea Arumeru Mashariki ni makundi yanayotaka urais na kusisitiza kuwa kama kuna mtu mwenye umri kama wake na anataka urais mwaka 2015, asahau kupata kiti hicho.
Alisisitiza kuwa wanaotajwa kutaka urais wakiwa na umri kama wake na hata kuzidi, huu si wakati wao bali wa vijana.
Mtoa habari wetu kutoka ndani ya kikao hicho, alisema kauli hiyo ya Rais Kikwete iliwanyong’onyeza baadhi ya makada wanaotajwa kutaka nafasi hiyo wakiwa tayari na umri mkubwa.
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Bombuli, Januari Makamba (CCM), amependekeza kuwa umri wa kugombea urais, ushushwe kutoka miaka 40 ya sasa hadi 35.
Ushauri huo uliungwa mkono pia na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ambaye alihoji kuwa kama Uganda wameweza kwa nini Tanzania mabadiliko hayo hayawezekani.
Makamba alitoa kauli hiyo jana katika kongamano la Femina HIP la vijana walio nje ya shule, lilioandaliwa na Jukwaa la Femina, huku likiwa limebeba mada kuu ya ushiriki wa vijana katika uundwaji wa Katiba mpya na kufanyika katika Ukumbi wa British Council, jijini Dar es Salaam.
Wabunge hao wawili pia walitaka umri wa mtu kuruhusiwa kupiga kura uwe miaka 16 badala ya 18 kama ilivyo sasa.
Akifafanua pendekezo hilo, Makamba alisema Tanzania inapaswa kuiga mfano wa nchi jirani kama Uganda, Burundi na Rwanda ambao tayari wanafuata mfumo huo.
Alisema asilimia kubwa ya wananchi wa taifa hili ni vijana hivyo haoni ni kwa nini hawapewi fursa kugombea nafasi hiyo kwa kisingizio cha umri.
Kuhusu kupiga kura, mbunge huyo alisema anaamini kwamba umri wa miaka 16 alionao kijana wa karne hii ana uwezo wa kuchambua mambo na kumchagua kiongozi anayeona anafaa.
Kwa upande wake Zitto alisema hata yeye anaunga mkono hoja hiyo na kudai kwamba linawezekana kabisa huku akitolea mfano kwamba kipindi cha nyuma wanawake walikuwa hawashiriki katika kupiga kura.
Kama vile haitoshi alisema miaka ya kupiga kura ilikuwa ni kuanzia 21 lakini kadri muda ulivyozidi kwenda na kuonekana kwamba kuna haja ya sheria hiyo kufanyiwa marekebisho, ndipo ikafika miaka 18 hivyo ni wakati sasa muafaka kwa vijana kudai haki hiyo ya kupiga kura wakiwa na miaka 16.
Hata hivyo Zitto aliwataka vijana katika mchakato huu wa Katiba kutokubali mjadala huo utawaliwe na wanasiasa kwa kuwa wengi wanajadili kwa maslahi yao.
Kwa mujibu wa Zitto tayari ameshaona wanasiasa hao wameanza kuutumia mjadala huo kwa manufaa yao huku wakilenga katika kugawana madaraka na kuacha kujadili mambo muhimu kama ajira kwa vijana na namna gani wataweza kulipwa kutokana na kazi wanazozifanya.
Pia mbunge huyo aliwaonya vijana wasije wakafikiri Katiba mpya ndiyo itakuwa suluhu ya matatizo yanayowakabili na badala yake kuwataka wafanye kazi kwa bidii.
“Msidhani kwamba eti Katiba mpya ikiwepo ndipo matatizo ya ajira yatakwisha au uibwaji wa rasilimali za nchi utaisha la hasha kwani matatizo haya yanaweza kuendelea kuwepo; kinachotakiwa ni kuchapa kazi na kujenga hoja pale mambo wanapoyaona yanaenda sivyo,” alisema.
Hata hivyo wabunge hao walipoulizwa swali na mmoja wa washiriki wa kongamano hilo, Humphrey Polepole, kama wangependa kuwa kwenye Bunge Maalum la Katiba, walisema ndiyo kwa madai kwamba wanaamini watakuwa na mchango mkubwa kuwepo kwao katika tume hiyo.
Kwa pamoja wabunge hao walisema kwamba wanataka kuonyesha siasa za tofauti katika kuondoa matatizo ya vijana na wananchi kwa jumla bila kujali vyama wanavyotoka.
Katika kongamano hilo la siku mbili ambapo mgeni rasmi alikuwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, linalenga kupata maoni ya vijana wa Tanzania kuhusu Katiba mpya kwani takwimu zinaonyesha kwamba Tanzania ina watu milioni 44 na kati ya hao asilimia 65 ni watu walio chini ya umri wa miaka 25.


Source: Tanzania Daima. 29/Feb/2012
JK: Hatutaki Rais mzee 2015


na Nasra Abdallah
WAKATI makundi ya urais yakijipanga kuwania kiti hicho mwaka 2015, bila kuyajali, Rais Jakaya Kikwete amesema wanaota urais wakiwa na umri kama wake, wasahau, Tanzania Daima Jumatano limedokezwa.
Kikwete alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kilichokutana juzi, pamoja na mambo mengine, kupitisha jina la mgombea ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilisema kuwa Rais Kikwete alitoa kauli hiyo wakati akifungua kikao hicho.
Kwa mujibu wa habari hizo, Rais Kikwete alisema kuwa kinachotokea Arumeru Mashariki ni makundi yanayotaka urais na kusisitiza kuwa kama kuna mtu mwenye umri kama wake na anataka urais mwaka 2015, asahau kupata kiti hicho.
Alisisitiza kuwa wanaotajwa kutaka urais wakiwa na umri kama wake na hata kuzidi, huu si wakati wao bali wa vijana.
Mtoa habari wetu kutoka ndani ya kikao hicho, alisema kauli hiyo ya Rais Kikwete iliwanyong’onyeza baadhi ya makada wanaotajwa kutaka nafasi hiyo wakiwa tayari na umri mkubwa.
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Bombuli, Januari Makamba (CCM), amependekeza kuwa umri wa kugombea urais, ushushwe kutoka miaka 40 ya sasa hadi 35.
Ushauri huo uliungwa mkono pia na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ambaye alihoji kuwa kama Uganda wameweza kwa nini Tanzania mabadiliko hayo hayawezekani.
Makamba alitoa kauli hiyo jana katika kongamano la Femina HIP la vijana walio nje ya shule, lilioandaliwa na Jukwaa la Femina, huku likiwa limebeba mada kuu ya ushiriki wa vijana katika uundwaji wa Katiba mpya na kufanyika katika Ukumbi wa British Council, jijini Dar es Salaam.
Wabunge hao wawili pia walitaka umri wa mtu kuruhusiwa kupiga kura uwe miaka 16 badala ya 18 kama ilivyo sasa.
Akifafanua pendekezo hilo, Makamba alisema Tanzania inapaswa kuiga mfano wa nchi jirani kama Uganda, Burundi na Rwanda ambao tayari wanafuata mfumo huo.
Alisema asilimia kubwa ya wananchi wa taifa hili ni vijana hivyo haoni ni kwa nini hawapewi fursa kugombea nafasi hiyo kwa kisingizio cha umri.
Kuhusu kupiga kura, mbunge huyo alisema anaamini kwamba umri wa miaka 16 alionao kijana wa karne hii ana uwezo wa kuchambua mambo na kumchagua kiongozi anayeona anafaa.
Kwa upande wake Zitto alisema hata yeye anaunga mkono hoja hiyo na kudai kwamba linawezekana kabisa huku akitolea mfano kwamba kipindi cha nyuma wanawake walikuwa hawashiriki katika kupiga kura.
Kama vile haitoshi alisema miaka ya kupiga kura ilikuwa ni kuanzia 21 lakini kadri muda ulivyozidi kwenda na kuonekana kwamba kuna haja ya sheria hiyo kufanyiwa marekebisho, ndipo ikafika miaka 18 hivyo ni wakati sasa muafaka kwa vijana kudai haki hiyo ya kupiga kura wakiwa na miaka 16.
Hata hivyo Zitto aliwataka vijana katika mchakato huu wa Katiba kutokubali mjadala huo utawaliwe na wanasiasa kwa kuwa wengi wanajadili kwa maslahi yao.
Kwa mujibu wa Zitto tayari ameshaona wanasiasa hao wameanza kuutumia mjadala huo kwa manufaa yao huku wakilenga katika kugawana madaraka na kuacha kujadili mambo muhimu kama ajira kwa vijana na namna gani wataweza kulipwa kutokana na kazi wanazozifanya.
Pia mbunge huyo aliwaonya vijana wasije wakafikiri Katiba mpya ndiyo itakuwa suluhu ya matatizo yanayowakabili na badala yake kuwataka wafanye kazi kwa bidii.
“Msidhani kwamba eti Katiba mpya ikiwepo ndipo matatizo ya ajira yatakwisha au uibwaji wa rasilimali za nchi utaisha la hasha kwani matatizo haya yanaweza kuendelea kuwepo; kinachotakiwa ni kuchapa kazi na kujenga hoja pale mambo wanapoyaona yanaenda sivyo,” alisema.
Hata hivyo wabunge hao walipoulizwa swali na mmoja wa washiriki wa kongamano hilo, Humphrey Polepole, kama wangependa kuwa kwenye Bunge Maalum la Katiba, walisema ndiyo kwa madai kwamba wanaamini watakuwa na mchango mkubwa kuwepo kwao katika tume hiyo.
Kwa pamoja wabunge hao walisema kwamba wanataka kuonyesha siasa za tofauti katika kuondoa matatizo ya vijana na wananchi kwa jumla bila kujali vyama wanavyotoka.
Katika kongamano hilo la siku mbili ambapo mgeni rasmi alikuwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, linalenga kupata maoni ya vijana wa Tanzania kuhusu Katiba mpya kwani takwimu zinaonyesha kwamba Tanzania ina watu milioni 44 na kati ya hao asilimia 65 ni watu walio chini ya umri wa miaka 25.


Source: Tanzania Daima. 29/Feb/2012

Pinda atoboa siri juu ya uwekezaji kwa maliasili

                                             Waziri Mkuu wa Tanzania, 

Mizengo Pinda
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema ili nchi iweze kunufaika na maliasili ilizonazo, kuna haja ya kutumia wawekezaji wa ndani na kama itashindikana basi utumike mfumo wa ubia katika utafutaji wa maliasili hizo.
Aliyasema hayo Februari 28, 2012 wakati akifungua majadiliano yaliyohusu Jinsi ya kutumia vema maliasili na kuhakikisha zinalitajirisha bara la Afrika yaliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Amesema mikutano ya majadiliano kama hiyo inapaswa kusaidia kutoa mafunzo kwa Watanzania ili wajue namna ya kusimamia vizuri zaidi maliasili za nchi yao. “Tunapaswa tuwafundisha watu wetu jinsi ya kuwekeza katika utaalamu, mitaji, mitambo na kwenye teknolojia ili tuache kutegemea vyanzo vya kutoka nje ya nchi,” alisema.
Amesema: “Tusipofanya hivyo tutajikuta tunaangukia katika balaa la kutonufaika na maliasili zetu ambalo limezikumba nchi nyingi za Afrika ambazo zimefanikiwa kugundua rasilmali kama vile almasi, mafuta, gesi na dhahabu katika nchi zao,” alionya.
“Balaa ama laana ya kutonufaika na rasilmali imezikumba nchi nyingi za Afrika, sina haja ya kuzitaja majina. Wengi wetu tumeshuhudia jinsi ambavyo ugunduzi wa maliasili ulivyochangia kuleta vita vya wenyewe kwa wenyewe, vita baina ya nchi; tumepoteza fedha nyingi, tumepoteza maisha ya watu wengi wasio na hatia hasa wanawake na watoto na wengine wamebakia vilema kutokana na vita hivyo,” aliongeza.
Amesema Tanzania iko tayari kushirikiana na wabia wa maendeleo, taasisi za kimataifa, sekta binafsi au watu binafsi ili kuhakikisha inajengea uwezo wananchi wake katika maeneo tofauti yakiwemo ya utafutaji, uongezaji thamani na uuzaji wa maliasili tulizonazo.
“Hii ndiyo njia pekee ambayo itahakikisha kwamba nchi na wananchi wake wanafaidika na maliasili zilizopo,” alisisitiza.
Naye Prof. Paul Collier wa Chuo Kikuu cha Oxford cha Uingereza anayeshughulikia masuala ya uchumi wa Afrika ambaye alikuwa mtoa mada katika majadiliano hayo, alisema Tanzania na nchi za Afrika hazijengea uwezo watu wake ili waweze kuwekeza vya kutosha kwenye utafutaji wa maliasili na ndiyo maana bara hili limeendelea kubaki maskini.
“Ili kunufaika na sekta hii inabidi kuwekeza zaidi, kufanya tathmini ya maliasili mlizonazo, kuzipangia matumizi bora, kulinganisha matumizi ya sasa na kuangalia maisha ya baadaye yatakuwaje na kutunza akiba kutokana na maliasili mlizonazo,” alisema.
Naye Balozi wa Finland nchini, Bibi Sinikka Antila alisema hivi sasa Tanzania imevumbua maliasili nyingi zinazoweza kuiletea utajiri mkubwa lakini akasisitiza haja ya kusizimamia vizuri ili kuhakikisha kuwa zinawanufaisha wananchi wote.
Akitoa mfano wa kutokuwepo usimamizi katika rasilmali, Balozi huyo alisema uvunaji magogo haujatungiwa sheria kali na wala hautozwi kodi inavyostahili na matokeo yake, nchi inapoteza asilimia 90 ya mapato kutokana na mazao ya misitu. “Usimamizi endelevu wa misitu ndiyo msingi wa uchumi imara”, alisisitiza.
Mapema, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Prof. Joseph Semboja alisema taasisi hiyo imeandaa majadilianio hayo ili kutoa fursa kwa viongozi waweze kujadiliana na kubadilishana uzoefu kwenye masuala ya utunzaji maliasili.
Alisema kikao hicho ni mwanzo wa mikutano ambayo taasisi hiyo imejipanga kuifanya ili kuwapa nafasi viongozi wapate mbinu kuboresha utendaji kazi wao. Alisema mwezi ujao, taasisi yake itaandaa mkutano kwa ajili ya Wakuu wa Tume za Uchaguzi kutoka nchi 16 ili wabadilishane uzoefu katika eneo hilo.


Short URL: http://www.thehabari.com/?p=14022

Taifa la waliao, wakilia na kuliwa, nani atawafungua?

M. M. Mwanakijiji

LIPO taifa sitalitaja ambapo watu wake huliwa huku wanalia na wale wanaowala nao wanaliwa huku wakilia na kuliliana huku na wao wenyewe wakililiwa. Taifa hili - ambalo sitalitaja linaongozwa na watu wanaopenda kula sana.
Wanakula kila kilichopo mbele yao na wanakula kama wasiojua kushiba. Wanakula hata uji wa mgonjwa, wanakula hadi vya watoto!
Wanakula huku hakuna wa kuwauliza kwani hata wale ambao wanapaswa kuwauliza na wenyewe wanapiga mahesabu ya jinsi gani wataingia mezani nao kula! Ni taifa la walao na wale waliwao!
Mtu yeyote anapotembelea taifa hili nisilolitaja anaweza kuona mara moja tofauti kati ya wale wanaokula, wanaoliwa, wanaotaka kula na wale wanaolilia kutaka kula au wanalia wakiliwa au vya kwao vikichukuliwa kuliwa.
Wapo amba kwenye hili taifa lisilo na jina, wameshikilia masufuria na mabakuli makubwa ya kula wakilia kwa sauti za kukoroma (zenye mikwaruzo ya kuudhi) “ongeza ongeza!” wakiwalilia watu wasio na uwezo wa kuwapa cha nyongeza. Wafanyakazi na wakulima katika taifa hili wanaambiwa tena kwa kupigiwa kelele “fanyeni kazi kwa bidii na maarifa” ili pato liongezeke.
Wasichoambiwa maskini hawa wa Mungu ni kuwa wanaambiwa waongeze uzalishaji ili mabakuli ya walaji yazidi kuongezewa. Songombingo huja pale maskini hawa wenye kuliwa wanapoamua siku moja na wao waamue kudai nyongeza kidogo ya kula hata kama ni tumifupamifupa.
Walaji wakubwa huja juu; wanang’aka na wakati mwingine na vitisho! Nilisimuliwa kisa kilichotokea kwenye hiyo nchi nisiyoitaja pale kundi moja la walaji wadogo wadogo lilipojaribu siku moja kutishia kuacha kuwapikia walaji wakubwa!
Msimamizi mkuu wa walaji wakubwa alichukizwa sana na aliamua kuwapiga mkwara hadharani wale walaji wadogo na kuwaambia wasikubali kutumiwa na watu wabaya hata wakafika mahali wakakataa kuwapikia walaji wakubwa.
Katika mkutano wake na Wazee wa Walaji Mlaji yule mkubwa alizungumza kwa hasira sana na kuwaambia kuwa wakiendelea kutishia maslahi ya walaji watapigwa virungu. Maskini wa Mungu wale wapishi wakuu walibakia wanatetemeka hasa walipokumbushwa kisa cha ndege fulani, kisa ambacho kwa kweli kiliwalazimisha kufikiria mara mbili.
Walaji wakubwa waliendelea kula na kutafuna huku wakicheua mafuta, wakikumbatiana na kupongezana huku wakifanya mpango mwingine wa kujiongezea kula zaidi. Kilichowatibua wanaoliwa zaidi ni siku ile ambapo walaji wakubwa walipoamua kujiongezea ulaji zaidi huku wakiwaambia wananchi wa taifa lile nisilolitaja kuwa taifa lao liko kwenye hali mbaya ya uchumi. Wakaamua kujiongezea ulaji huku wakitetea kuwa walaji wote wakuu wamekubaliana kula!
Ndipo kundi jingine la watengeneza chakula cha walaji wakubwa lilipoamua na lenyewe kuomba kidogo liongezewe kwenye sinia lao la ulaji. Ndugu zangu hawa walikataliwa kwa mbinde na upinde, kejeli na dharau. Lilikuwa kosa ambalo walaji wakuu hawalikutarajia. Kwani wanaohudumia walaji wakubwa wakaamuka kugoma!
Kama utani hivi. Walaji wakuu walikuwa na uhakika wa kutosha tu kuwa walaji hawa wadogo hawana umoja na hawawezi kusimamia mgomo kwa muda mrefu. Oh, walijikuta wanashangazwa pale ambapo walaji wale walipong’ang’ana wakang’ang’ania!
Ndipo mmoja wa walaji wakubwa alipojitokeza kwenye runinga akiwa amekasirika na akiwa amezungukwa na walaji wengine mahiri wote wakiwa na nia moja kuwalazimisha wapishi warudi jikoni! “Msiporudi kutupikia mtajifukuzisha kazi” alitamka mlaji mkuu msaidizi. Kesho yake hakuna aliyerudia! Mambo yalianza kuwa mabaya kwenye taifa la lile nisilolitaja.
Waliokuwa wanaliwa sana na ambao walijikuta wanazidi kulia wakati mgomo ukiendelea walipoamua kufanya kweli. Wakajitokeza na kuandaa umati kuwapinga walaji wakubwa! Wakubwa wakashtuka kwani hilo hawakulitarajia. Walitarajia kuwa wakipiga mkwara, mabomu na vitisho basi wanaoliwa watanyamaza kwani kwenye taifa lile mikwara hufanya kazi sana.
Huku nyuma mlaji mkubwa akisema kitu basi watu hufyata mkia. Haikuwa hivyo safari hii. Wanaoliwa hawakuwa tayari kukaa kimya; waliamua kubanana na watawala wao kwenye taifa hili nisilolitaja.
Mambo yalipozidi kuwa magumu na wanaoliwa zaidi walipozidi kulia na kuanza kupiga mayowe ndipo walaji wakubwa walijikuta hawana jinsi bali kukaa na wapishi wao kujaribu kutafuta suluhu. Wakakubali kuwaongezea kidogo kwenye masinia yao. Lakini hawakuwa tayari kuwanyanganya ulaji walaji wenzao wakubwa!
Na uwezekano wa walaji wale wakubwa waliosababisha tafruku hiyo kuhamia na kupelekwa kwingine kula ni mkubwa kwani kwenye taifa la walaji hakuna anayenyang’anywa sahani! Wanahemishwa meza au viti! Ukihamishwa meza unaweza kupelekwa kwenye kula kwa kunyemelea lakini ukihamishwa kitu umehamishwa mkao wa kula tu! Kula kunaendelea!
Ni mpaka pale wale waliwao watakapoamua kukataa kuwa sababu ya kula kwa wale walao ndipo mabadiliko ya kweli yanaweza kuanza kutokea. Vijana wanaojitahidi kila siku kufanya kazi watakapokataa kuwa sehemu ya mfumo wa kuliwa ambao wenye kula hula wakirithisha hadi watoto wao kula watakapokataa kuwa watetezi wa mfumo huo wa ulaji ndipo vijana wa taifa hilo ambalo sijalitaja watakapoanza kutafuta sehemu yao katika maisha ya nchi yao.
Walaji watakapokataliwa kula au kujiongezea vya kula ndipo wale wanaoliwa nao watapata nafasi ya kutafuta chakula! Nje ya hapo, walaji wakubwa, watetezi wa walaji na chama chao kikuu chao ulaji wataendelea kula bila kuulizwa huku mamilioni ya wananchi wenzao wakiendelea kubakia kunawa mikono na kuitwa kuja kutoa vyombo!
Wale wengine ambao wamegundua kuwa nje ya chama cha walaji hakuna nafasi wanajikuta wanaamua kuanza kuimba wimbo wa kusifia walaji ili na wao hata kama hawatakula sana wawekwe mahali ambapo wanaweza kuambulia makombo! Kumbuka, makombo ya walaji wakubwa ni chakula tosha kwa maskini mwombaji aliyeko kwenye taifa lile nisilolitaja!

Tanzania daima

UREMBO IRINGA NI KWA MAMA WEEK-END SHOP PEKEE


Tembelea Mama Week-End Urembo Shop Iringa leo ujipatia urembo kwa ofa maalum ya Pasaka
Usisumbuke kuuliza ama kutafuta duka la urembo ndani ya mji wa Iringa fika leo Mama Week-End Urembo Shop lipo eneo la Miyombini jirani na Famari Store karibu kabisa na Zebra ya Msitiki wa Ijumaa
Pete na mapambo ya kila aina ndani ya Mama Week - End urembo shop
Cheni za aina mbali mbali kwa wanawake na wanaume zipo
Ama kweli mama Week- End Urembo Shop ni jibu kwa swali lake kwako unayependa kupendezaUsisumbuke kutafuta ama kuuliza duka la urembo wa ukweli uwapo mjini Iringa uliza mama week-End Urembo Shop ni jibu la swali lako ,tupo jirani na Famari Store mkono wa kushoto barabara kuu ya Uhuru kabla ya kufika Zebra ya Msikiti wa Ijumaa kama watokea Stendi kuu na kama watokea Mshindo ni baada ya kuvuka Zebra ya mtikiti wa Ijumaa ng'ambo ya pili yaani mkono wa kulia utaona bango letu hapa juu .

Tupigie simu 0715 961433 Tutakusikia tutakufikia

Barrick offers scholarships to university students


The Vice President (Corporate Affairs) of African Barrick Gold (ABG), Deo Mwanyika, hands over a bursary award to some of the recipients of ABG’s scholarships to mining students at the University of Dar es Salaam. PHOTO BY A
CORRESPONDENT.


Staff Writer
AFRICAN Barrick Gold (ABG) has signed an agreement with the University of Dar es Salaam (UDSM) to provide scholarships to students in a move aimed at producing more Tanzanian graduates with the necessary skills needed to manage the country’s fast-growing mining sector.
The announcement of the bursaries was made at UDSM’s campus on Monday by ABG’s Vice President of Corporate Affairs, Deo Mwanyika, and the varsity’s Vice Chancellor, Prof. Rwekaza Mukandala.
“I am proud to say that ABG has for the past 10 years progressively
increased its commitment to human resource development in Tanzania by providing bursaries to top undergraduate students and offering scholarships to UDSM’s academic staff to pursue postgraduate studies,” said Mwanyika.
The two-year agreement will benefit 12 UDSM students to cover the costs of pursuing studies related to the mining industry. Since ABG inagurated its bursaries programme, more than 70 UDSM students have been awarded much-needed scholarships that enabled them to complete their degree programmes.
Most of these students, who were the top academic performers in their
programmes, are usually employed by ABG’s four gold-producing mines when they complete their degrees.
“As Tanzania’s leader in the mining sector, ABG is committed to further
increase its investment in higher education,” said Mwanyika.
“At African Barrick Gold, we put a lot of emphasis on human capital
development. The steady growth of Tanzania’s mining sector over the past 10 years has generated demand for a local workforce of mining experts.”
More than 400 other UDSM students and academic staff members have also benefitted from practical training, final-year project work and site visits to mines funded by ABG over the past few years.
ABG also finances the purchase of laboratory equipment, student site
visits, accepts UDSM students for practical work experience at its mine
sites and helps supervise final year students on their project works.
The miner, as part of the Tanzania Chamber of Minerals and Energy (TCME) initiatives, is also spearheading the integrated Mining Technical Training with the long-term vision of developing enough skills within the country to meet the demands of the fast-growing mining sector.
Mwanyika challenged students at institutes of higher learning in Tanzania to apply the education and skills gained for the development of the nation.
On his part, Prof. Mukandala thanked ABG for providing scholarships to UDSM students and urged other investors to follow suit. He said UDSM would work closely with ABG to ensure Tanzania develops a strong workforce of skilled mining professionals.

 http://www.thehabari.com/?p=14028

MREMA NAYE AKATAA POSHO


Pamela Chilongola na Keneth Goliama
MWENYEKITI wa Chama Cha Tanzania Labour  Part (TLP ) Augustino Mrema amemtaka Spika wa Bunge, Anne Makinda kuwa  na uvumilivu na kiwango cha mshahara wa   wabunge wanachokipata.Akizungumza  na waandishi wa habari  ofisi kwake jana, Mrema alisema wabunge wanatakiwa kuogopa kutawaliwa na tamaa ya fedha katika kuongoza wananchi.

Mrema alisema wabunge hawahitaji kuwa mamilionea katika kuwasaidia wananchi bali kuna miradi mbalimbali kama mfuko wa jimbo na kufungua miradi ya maana katioka  kuinua uchumi wa wananchi.

“Ni kweli fedha  tunazolipwa hazitoshi lakini tunatakiwa kuvumilia na kuendelea kuongoza maana hata ukipewa Sh10 milioni  haziwezi kutosha iwapo mbunge hatakuwa na  matumizi ya mipango thabiti,” alisema.
Mrema alisema kinachoongelewa na Spika Makinda ni kweli lakini  mbunge anatakiwa kuweka bajeti katika  kuendesha jimbo lake.

Alisema  kama wabunge wanataka kuondoka kwa ajili ya kukosa posho na mishahara waende lakini kwa yeye  hawezi kuondoka  kutokana na kiwango hicho kumtosha sana.

 “Nimekaa zaidi ya miaka 20 bila kupata chochote, niliweza kuwasaidia wananchi wangu licha ya kujiuzulu uwaziri wangu, sasa kwanini leo niachie hata hiki kidogo siwezi kukiachia ng’oo! Haachii ngazi mtu hapa,” alisema mrema.
Alisema hakuna mbunge ambaye ataweza kuachia ngazi kwa ajili ya mshahara kuwa mdogo kutokana na kwamba kazi ya ubunge sio fedha bali ni kujituma kwa wananchi.

Marema alisema  Spika Makinda hatakiwi kulaumiwa kutokana na wabunge wachache waliongia bungeni kwa ajili ya kutafuta fedha  humfuata  na kumueleza matatizo yao.“Spika makinda ni  halalali kueleza kutokana yeye kuwa mama wa wabunge wote wa kupokea malalamiko na kuyafanyia kazi,” alisema.

Uteuzi wa mgombea Arumeru Wakatai huo huo chama cha TLP kimetangaza kusimamisha mgombea ubunge katika jimbo la Arumeru mashariki.

 Mrema alisema  chama kimempitisha Abraham Mhoza Chipaka kupeperusha Bendera ya TLP . Alisema kamati ya  halmashauri ya wilaya ya chama hicho ilimpitisha Mgombea huyo  kwa kuona nafaa kukiwakilisha chama.
“TLP tumejipanga kugombea Arumeru Mashariki tutaenda kugombea na sio kusindikiza kama wanavyofikilia”alisema na kuongeza:
 “Tumemsimamisha Abrahamu Chipaka ambaye ni mjasiliamali amepitishwa na kamati ya Halmashauri ya Wilaya Taifa”alisema Mrema. Mrema alisema anafurahishwa na migogoro inayoendelea ndani ya chama cha CUF na NCCR mageuzi kwa kile alichodai kuwa aliambiwa yeye ni dikteta na kufukuza viongozi katika chama alichokuwa akikiongoza.

“Uongozi ni mgumu wanatakiwa wajifunze kupitia vyama vingine wasibaki kushabikia na kuniona mimi ni dikteta kazi yangu ni kuwafukuza wanachama wenzangu,sasa kikowapi leo hii yamewageukia wao”alisema Mrema. Alisema suala la watu kumnyemelea ili kumuondoa uenyekiti hakubaliani nao kwa kuwa huyo anayetaka kuchukua nafasi hiyo anasifa yeyote kuwa mbunge.

HII NI JUZIJUZI KWENYE MTV MUSIC AWARD BIDADA JENIFER LOPEZ


Maganga one

Mh. Jerry Slaa aongoza Kongamano la umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Mjini magharibi,Zanzibar

Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Meya wa Ilala,Jerry Slaa akihutubia kwenye Kongamano la umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Mjini magharibi kuhusu maadili katika uchaguzi wa kuchagua viongozi wa jumuiya za chama hicho,halfla hiyo ilifanyika katika Ofisi kuu ya CCM Mjini Magharibi Zanzibar juzi.
Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi na Meya wa Ilala,Jerry Slaa (kulia) akimkabidhi cheti cha Shukrani katika kutumikia Chama,Katibu wa UVCCM wa Wilaya ya Mjini Unguja, Mohamed Ali Khalfani wakati wa ufunguzi wa Kongamano la umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Mjini magharibi kuhusu maadili katika uchaguzi wa kuchagua viongozi wa jumuiya za chama hicho,hafla hiyo ilifanyika katika Ofisi kuu ya CCM Mjini Magharibi Zanzibar juzi.
Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Mjini Unguja, Omary Justas Morris akihutubia kwenye Kongamano la Umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi kuhusu maadili katika uchaguzi wa kuchagua viongozi wa jumuiya za chama hicho,halfla hiyo ilifanyika katika Ofisi kuu ya CCM Mjini Magharibi Zanzibar juzi. Katikati ni Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi na Meya wa Ilala,Jerry Slaa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mjini Magharibi,Tauhida Cassian Galos. 
Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi na Meya wa Ilala,Jerry Slaa (kushoto),Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mjini Magharibi,Tauhida Cassian Galos (katikati) na Mjumbe wa halmashauri kuu,Hamadi Yusufu Masauni, wakipiga makofi wakati wa ufunguzi wa Kongamano la umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Mjini magharibi kuhusu maadili katika uchaguzi wa kuchagua viongozi wa jumuiya za chama hicho,halfla hiyo ilifanyika katika Ofisi kuu ya CCM Mjini Magharibi Zanzibar juzi.
Wanachama wa umoja wa vijana (UVCCM) wakimtunza Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mjini Magharibi,Tauhida Cassian Galos (katikati) baada ya Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi na Meya wa Ilala,Jerry Slaa (hayupo pichani) kufungua rasmi Kongamano la umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Mjini magharibi kuhusu maadili katika uchaguzi wa kuchagua viongozi wa jumuiya za chama hicho,halfla hiyo ilifanyika katika Ofisi kuu ya CCM Mjini Magharibi Zanzibar juzi.