Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Tuesday, February 21, 2012

NJAA YABISHA HODI TARAFA MAHENGE JIMBONI KWA PROF PETER MSOLA

Mahindi yakiwa yamekauka kutoka na juu kali linaloendelea kuwaka katika tarafa ya Mahenge wilaya ya kilolo
Gari la mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Bosco Ndunguru likipita jirani na mashamba hayo yaliyokumbwa na ukame

Hali ya ukame inayoendelea katika tarafa ya Mahenge katika jimbo la Kilolo linaloongozwa na Prof.Peter Msolla imeanza kutishia maisha ya wananchi wa tarafa hiyo kutokana na mazao yao kuanza kukauka .

Wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com wakazi wa tarafa hiyo wamesema kuwa pamoja na mazao yao kwa mwaka huu kuonyesha kustawi vizuri ila kutokana na mvua kusimama kunyesha kwa muda wa zaidi ya miezi miwili sasa hali ya mazao imeanza kuwa mbaya zaidi .

Hivyo walisema kuwa iwapo juu litaendelea kuwaka upo uwezekano wa mazao yao hasa mahindi kukauka kabisa na kuwa baadhi ya mashamba ya wakulima katika tarafa hiyo mahindi yamekauka kabisa na unaweza kuwasha moto ukawaka .

Mbunge wa jimbo la Kilolo Prof.Peter Msolla amesema kuwa njia pekee ambayo serikali imeanza kuitumia kwa ajili ya kuwanusuru wananchi hao na tatizo la uhaba wa chakula kwa mwakani ni kuwahamasisha kuutumia vema mfereji wa umwagiliaji uliojengwa na serikali toka mwaka 2006 kwa zaidi ya milioni 500.

Mbunge Msolla alisema kuwa tarafa hiyo ya Mahenge ni moja kati ya tarafa za mkoa wa Iringa ambazo zinaongoza kuwa na joto sana na kuwa si mara ya kwanza wananchi hao mazao yao kunyauka kwa jua.

Hata hivyo amesema kumekuwepo na mipango ya kuwapa chakula cha msaada kila wanapokumbwa na tatizo hilo .

Chanzo: Francis Godwin blod

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.