Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Tuesday, February 21, 2012

Dkt. Bilal Naye Apewa Uchifu Nkasi


Makamu Wa Rais wa Jamhuti ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakiwa na mavazi ya asili ya kabila la Kikonongo baada ya kuvishwa na kutunukiwa uchifu wa Kabila la Kikonongo na machifu wa Kijiji cha Inyonga Wilaya ya Mpanda wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Rukwa na Katavi jana Februari 19, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea shamba la mahindi la Waziri Mkuu Mizengo Pinda, lililopo Kijiji cha Vilolo wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Katavi na Rukwa jana Februari 20, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea shamba ufugaji wa Nyuki wa kisasa la Waziri Mkuu Mizengo Pinda, lililopo Kijiji cha Vilolo wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Katavi na Rukwa jana Februari 20, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

 Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Baba mzazi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Exavery Kayanza Pinda, wakati alipokuwa akipita kuelekea Kijiji cha Mwamapuli akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi leo, Februari 20. 2012. Kulia nia Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Eng. Stella Manyanya
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mama Asha Bilal,akisalimiana na Mama mzazi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Albetina Kasanga, wakati wakiwa katika ziara ya Mkoa wa Katavi jana Februari 20, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
 
Chanzo: Mjengwablog

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.